Kuishi Maisha Tele. Katika mwanzo wa mwaka mpya, Niliwapa changamoto

Similar documents
John Lesson Eighteen Yohana Somo la Kumi na Nane

MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA KIRINYAGA YA KATI MWAKA WA 2013

Ujasiri wa Kimaadili. Mojawapo ya madhumuni ya maisha ya duniani

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF BOMAS OF KENYA

There is one God Mungu ni mmoja 1

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF

EVANGELISM FOR CHRIST UINJILISTI KWA AJILI YA KRISTO

Pre-Departure Program Swahili Unit 11 Worksheet UNIT 11: LOCATIVES, PREPOSITIONS, AND RELATIVE AND OBJECT INFIXES

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

NEW LIFE IN CHRIST MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO

Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtukufu Mtume

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

Je, Umesikia Juu Ya Kanuni Nne Za Kiroho?

ZABURI 91 mstari 1. KJV-lite VERSES

MALAIKA: WAJUMBE WA MUNGU

BARUA YA TATU KWA SHEIKH UBAYD AL-JÂBIRĪ [AULIZWA SHEIKH UBAYD] NA Sheikh Sālim at-twawîl (hafidhahullāh)

Kitabu Changu cha Mistari ya Biblia Swahili

DINI JE, DINI NI MUHIMU?

BARAZA LA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA (Mawasiliano yawasilishwe kwa MSAJILI)

HALI YA UISLAMU. Maelezo ya kumsaidia Mkristo aufahamu Uislamu

NEW INTERNATIONAL VERSION

Rainbow of Promise Journal

Imâm Al-Albâni, Katika Kumsifu Mwanafunzi Wake, Muheshimiwa Sheikh Ali Hasan 1

AHMAD AL-RAYSUNI. SWAHILI VERSION idara ya Lugha na ukalimani ya Chuo Kikuu cha waislamu cha Morogoro. IIIT Mfululizo wa Vitabu kwa Muhtasari

Tawasali. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags:

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MANDERA CENTRAL CONSTITUENCY, HELD AT RHAMU

Ukweli Uliopotea - Sehemu Ya Tatu

2002 Version of the Basic Talk on "Using African Proverbs, Sayings, Idioms, Riddles, Stories, Fables, Play

Gazeti la kwanza la Kiislam kutolewa kwa lugha ya Kiswahili - mwaka 1936

Published on Al-Islam.org ( Home > Mahari ya Damu > Mahari ya Damu. Mahari ya Damu

UWAJIBIKAJI NDANI YA JESHI LA POLISI

Vitendawili Vya Swahili

No. Book Name Category Type Price 1 AFYA MARIDHAWA -1 SWAHILI SUBSCRIPTION 2, AFYA NA UZIMA SWAHILI SUBSCRIPTION 8,500.00

Zanzibar itafutika-mwanasheria

Sura al-ahzaab. Tafsiri na Maelezo. Abdilahi Nassir

HAKIKA YA AHMADIYYA. Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania

TUMERITHI TUWARITHISHE

Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya

Khadija-tul-Kubra. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Published on Books on Islam and Muslims Al-Islam.org (

IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE.

Ukweli wa hadith ya karatasi

February 9, 2017 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 16 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY

WELCOME TO GOD S SERVICE A.C.K. ST. LUKE S PARISH UMOJA & TENA CHURCH QUOTE OF THE WEEK PRAYER OF THE DAY

The Lord be with you And with your spirit

HAKIBulletin RAIS AMTEUA PROF. JUMA KUWA JAJI MKUU WA TANZANIA. Ndani: JARIDA LA MAHAKAMA YA TANZANIA

NAIROBI CITY COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

NEW INTERNATIONAL VERSION

JUNE 4, Acts 2:1-12 and Offering...Pastor Maromy Samuel All Hail the Power of Jesus Name led by Haitian Congregation Worship Team

MOROGORO JARIDA LA. ISSN Toleo Na.4 Julai 2005 BODI ZA AFYA ZA WILAYA - SAUTI YA WANANCHI

YA AL HABBIB SAYYEID

Toleo la kwanza: June, 2007 (Jamaadi Aakhar, 1428) Vitabu ii.

Uwezo Kenya National Learning Assessment 2014

Bismillah ar-rahman ar-raheem SHAHADA 1 YALIYOMO

HOTUBA YA JAJI MKUU MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA SIKU YA SHERIA, DAR ES SALAAM, TAREHE 1 FEBRUARI, 2018

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS IJARA CONSTITUENCY AT IJARA BARAZA PARK

Imam Mahdi katika Usunni Na Ushia

TALKING ABOUT ONESELF TO ACT IN THE WORLD: A SWAHILI AUTOBIOGRAPHY (SHAABAN ROBERT, MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI

KITABU CHA MAFUNZO KWA WATOA DAWA KATIKA MADUKA YA DAWA MUHIMU

MRADI WA METHALI (SANALASKUJA PROJEKTI)

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

NGUO-NYINGI MKOTI: MWANZISHAJI WA MJI WA NGOJI (ANGOCHE)

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

Ukoo Wake Na Kunasibika Kwake:

In Search of Contact: Rhetorical Questions in the Communicative Frame of the Funeral Sermon

WELCOME TO GOD S SERVICE ACK ST. LUKE`S PARISH UMOJA Theme: Endeavoring to touch the heart of God, (Matt 25:40). Kuazimia kumpendeza Mungu

TAUS RETREAT NEWS LETTER # 1

Ahadi za Serikali II. Zimekusanywa na HakiElimu Agosti 2007

VACATION BIBLE SCHOOL VBS. Newsletter. #Rebuilding through prayer, hard work & perseverance.

REPUBLIC OF KENYA COUNTY ASSEMBLY OF KILIFI THE HANSARD. Wednesday, 29 th March, 2017

TAARIFA YA HISTORIA YA MKOA WA MWANZA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA

HAKIBulletin JAJI MKUU AWAASA WAHITIMU WA SHERIA KUJIENDELEZA KITAALUMA HALIUZWI! BENKI YA DUNIA USULUHISHI MUAFAKA MAHAKAMA MAWAKILI MAHAKAMA KUU,

2

Ezra 3 Lessons Download or Read Online ebook ezra 3 lessons in PDF Format From The Best User Guide Database

MAOMBI YA QUR'AN TUKUFU SHEIKH MUZAFFAR AHMAD DURRANI

HOLY COMMUNION ACCORDING TO THE KENYAN RITE

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

Mashairi ya Masaibu ya Karbala

(Cell) (Cell) (Cell) (Landline) (Cell)

Ripoti ya Warsha Ya Washikadau Ihusuyo Mpango wa Uendeshaji wa Mazingira Wilayani Rufiji Iliyofanyika Utete Rufiji Juni 2000

December 6, 2017 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 6 th December The House met at 9.30 a.m.

AND REACTION IN SWAHILI POETRY.

Where is Africa? 2. What is African heritage? 3. What is the African heritage in the Bible? 6. What are African ways of worship?

Yassarnal Quran English

Immaculate Conception Church

Youth and Faith A collection of texts on the subject A collaborative Magazine Content

3 rd of 3 files Appendix and References

ATONEMENT IN AFRICAN PLURALISTIC CONTEXT: EXAMPLES FROM THE LUHYA OF WESTERN KENYA

Song of Peace. Verse 2, Part II: Dona nobis pacem, pacem. Dona nobis pa cem. Do na nobis pacem. Dona nobis pacem. Do na no_bis_pacem

MASHAIRI YA WAADHI "VERSES OF ADMONITION": the people of Mombasa rebuked by P J. L Frank! and Yahya Ali Omar

A COLLECTION OF 100 MAKONDE (KENYA) PROVERBS AND WISE SAYINGS

Wisdom Heaven. from. Martin Luther College Choir

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

Immaculate Conception Church

I Peter 4:12-19 Suffering with a Blessing

Praying Our Way Forward

I Peter 2:9-12 Who Are You?

REPUBLIC OF KENYA COUNTY ASSEMBLY OF KILIFI THE HANSARD. Wednesday, 3 rd October, 2018

Compassionate Together:

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MANDERA CENTRAL CONSTITUENCY, HELD AT ELWAK

This book belongs to:

Transcription:

UJUMBE WA URAIS WA KWANZA, JANUARI 2012 Na Rais Thomas S. Monson Kuishi Maisha Tele Katika mwanzo wa mwaka mpya, Niliwapa changamoto Watakatifu wa Siku za Mwisho kote kufanya uchunguzi muhimu wa kibinafsi na mkamilifu kwa kile ninachokiita maisha tele maisha yaliyojawa na wingi wa mafanikio, wema, na baraka. Kama vile tulivyosoma herufi za ABC katika shule, natoa ABC yangu ili kutusaidia kupokea maisha tele. Kuwa na Mtazamo Halisi A katika ABC zangu inamaanisha mtazamo. William James, mwanzilishi Mwamerika mwanasaikolojia na mwanafalsafa, aliandika, Mapinduzi makuu ya kizazi chetu ni ugunduzi kwamba wanadamu, kwa kubadilisha mtazamo wao wa ndani, wanaweza kubadilisha hali ya nje ya maisha yao. 1 Mengi sana katika maisha yanategemea mtazamo wetu. Jinsi tunavyochagua kuona mambo na kujibu wengine huleta tofauti zote Kufanya vyema tuwezavyo na kuchagua kuwa na furaha juu ya hali zetu, zozote zile, kunaweza kuleta amani na utoshelevu. Charles Swindoll mwandishi, mwalimu, na mchungaji Mkristo alisema: Mtazamo, kwangu, ni muhimu sana kuliko... yaliyopita,... kuliko pesa, kuliko hali zote, kuliko kutofaulu, kuliko kufaulu, kuliko kile watu wengine wanafikiria au wanavyosema au wanavyofanya. Ni muhimu zaidi kuliko umbo, kipaji, au ujuzi. Itajenga au kubomoa kampuni, kanisa, na nyumba. Jambo la ajabu ni kwamba kila siku tuna nafasi ya kuchagua mtazamo ambao tutachukua kwa siku hiyo. 2 Hatuwezi kuelekeza upepo, ila tunaweza kugeuza tanga. Kwa furaha tele, amani, na utoshelevu, acha tuweze kuchagua mtazamo halisi. Jiamini wewe Mwenyewe B Ni kwa kujiamini mwenyewe, katika wale walio pamoja nawe, katika kanuni za milele. Kuwa mwaminifu kwako mwenyewe, kwa wengine, na kwa Baba yako wa Mbinguni. Mmoja ambaye hakuwa mwaminifu kwa Mungu hadi alipokuwa amechelewa sana alikuwa Kadinali Wolsey ambaye, kulingana na Shakespeare, alikaa maisha marefu katika kuwatumikia wafalme watatu na kufurahia utajiri na mamlaka. Hatimaye, aliondolewa mamlaka yake na mali na mfalme aliyekosa subira. Kadinali Wolsey alilia: Laiti ningemtumikia Mungu wangu kwa nusu ya ari Nilimtumikia mfalme wangu, Hangeweza katika umri wangu Kaniacha mimi uchi kwa maadui wangu 3 1

Thomas Fuller, muumini wa Kiingereza na mwanahistoria aliyeishi katika karne ya 17, aliandika ukweli huu: Haamini, kile ambacho hakiishi kulingana na imani yake. 4 Usijikane na usiruhusu wengine kukushawishi kwamba wewe una upungufu katika kile unachoweza kufanya. Jiamini wewe mwenyewe halafu uishi ili uweze kufikia ahadi zako. Unaweza kupata kile unachoamini unaweza. Tazamia na amini na uwe na imani Kabiliana na Changamoto kwa Ujasiri Ujasiri unakuwa maadili ya maana na muhimu inapotambulika sio sana kama hamu ya kufa kiume bali kama azimio la kuishi kwa wema. Alisema mwandishi Mwamerika wa insha na mshairi Ralph Waldo Emerson: Chochote ufanyacho, unahitaji ujasiri. Njia yoyote uamuayo kwenda, kila mara kuna mtu atakayekuambia kwamba umekosea. Kila mara kuna ugumu unaotokea ambao unakujaribu uamini kwamba wakosoaji wako ni sahihi. Ili kubuni mpango wa utendaji na kuufuata mpaka mwisho, kunahitaji kiasi cha ujasiri kama ule mwanajeshi anaohitaji. Amani ina ushindi wake, lakini inahitaji wanaume na wanawake wenye ujasiri ili kushinda. 5 Kutakuwa na nyakati ambapo utaogopa na kufadhaishwa. Unaweza kuhisi kwamba umeshindwa. Uwezekano wa kupata ushindi unaweza kuonekana kuwa vigumu. Wakati mwingine unaweza kuhisi kama Daudi anayejaribu kupigana na Goliathi Lakini kumbuka Daudi alishinda! Ujasiri unahitajika ili kufanya msukumo wa kwanza wa lengo apendalo mtu, lakini pia ujasiri mkuu unahitajika wakati mtu anapojikwaa na lazima tena aweke juhudi ya pili ili kufaulu. Kuwa na azimio la kufanya bidii, uthabiti wa kutenda lengo jema, na ujasiri sio tu wa kupitia changamoto ambazo lazima zije lakini pia kufanya bidii ya pili, ikiwa itahitajika. Wakati mwingine ujasiri ni sauti kimya katika mwisho wa siku inayosema, Nitajaribu tena kesho. 6 Na tuweze kukumbuka hizi ABC tunapoanza safari yetu kwenye mwaka mpya, tukikuza mtazamo halisi, imani kwamba tunaweza kutimiza malengo na maamuzi yetu, na ujasiri wa kupitia changamoto zozote zinazoweza kuja katika njia yetu. Halafu maisha tele yatakuwa yetu. MUHTASARI 1. William James, katika Lloyd Albert Johnson, comp., A Toolbox for Humanity: More Than 9000 Years of Thought (2003), 127. 2. Charles Swindoll, katika Daniel H. Johnston, Lessons for Living (2001), 29. 3. William Shakespeare, King Henry the Eighth, act 3, scene 2, lines 456 58. 4. Thomas Fuller, katika H. L. Mencken, ed., A New Dictionary of Quotations (1942), 96. 5. Ralph Waldo Emerson, in Roy B. Zuck, The Speaker s Quote Book (2009), 113. 6. Mary Anne Radmacher, Courage Doesn t Always Roar (2009). KUFUNDISHA KUTOKA KWA UJUMBE HUU Fikiria kumwalika mwanafamilia ili kushirikisha uzoefu wa kibinafsi wakati ambapo mtazamo halisi, kujiamani kwao wenyewe, au ujasiri ulipowasaidia. Au waalike ili wapate mifano ya kanuni hizi tatu katika maandiko. Pengine unaweza kujitayarisha kufundisha kwa kufikiria kwa maombi kuhusu maandiko na uzoefu wako mwenyewe. VIJANA Ujasiri wa Kuepuka Dhoruba Na Maddison Morley Kwenye usiku wangu wa pili wa kambi ya Wasichana, tulikuwa na mvua kubwa na kimbunga. Kata yangu ilikuwa na karibu wasichana 24 waliohudhuria kambi pamoja na viongozi wao wawili, na sote ilibidi tuingie ndani ya moja ya vibanda viwili ili kujikinga. Mvua ilikuwa inanyesha kwa nguvu, na upepo ulikuwa unaendelea kuwa mbaya sana. Ilibidi nijikumbushe kila mara kuhusu maombi ya usalama ambayo rais wetu wa kigingi aliopeana awali. Kata yetu pia ilitoa ombi letu la kikundi katika kibanda chetu, na nilitoa maombi yangu ya kibinafsi. Wasichana wengi walipatwa na uoga, na ilikuwa rahisi kuona ni kwa nini. Kibanda chetu hakikuwa chenye nguvu, na tulikuwa karibu na mto. Karibu dakika 20 dhoruba ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba ilibidi kigingi kizima kukimbia kutoka kwa vibanda vyao vya kata hadi kwa vibanda vya washauri ambavyo vilikuwa kwenye mwinuko. Rais wangu wa kigingi alitoa ombi lingine, na tukaimba nyimbo, nyimbo za Msingi, na 2

nyimbo za kambi katika jaribio la kujifariji wenyewe. Ndio, tuliogopa, lakini tulihisi kwamba kila kitu kingekuwa sawa. Nusu saa baadaye hali ilikuwa SAWA kutuwezesha kurudi tena kwenye vibanda vyetu. Baadaye tuligundua kilichofanyika kwa kimbunga usiku huo. Kiligawanyika na kuwa dhoruba mbili. Moja ilituzunguka kulia na nyingine kushoto. Tuliyokumbana nayo hata haikuwa mbaya zaidi! Najua kwamba Mungu alisikia maombi yetu usiku huo na kwamba alitulinda dhidi ya dhoruba mbaya. Ni kwa nini kimbunga kigawanyike isipokuwa Mungu atake kigawanyike? Najua kwamba katika dhoruba za maisha, tunaweza kuomba kwa Mungu Baba wa Mbinguni na atasikia na kutujibu, kutupatia ujasiri na ulinzi tunaohitaji ili kufaulu kwa usalama. WATOTO Kapteni Moroni Kapteni Moroni alikuwa na ujasiri alivyokuwa akikabiliana na changamoto. Alipenda ukweli, uhuru, na imani. Alijitolea maisha yake kwa kuwasaidia Wanefi kuhifadhi uhuru wao. Unaweza kuwa kama Kapteni Moroni kwa kupitia changamoto zako kwa ujasiri. Pia unaweza kujitengenezea bendera yako ya uhuru kwa kuandika kwenye kijikaratasi mambo ambayo ni muhimu kwako na kwa familia yako. Mahali pa Kupata Mengi Zaidi Alma 46:11 27: Bendera ya uhuru Alma 48:11 13: Sifa za Moroni 2012 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa Imechapishwa USA Kiingereza kiliidhinishwa: 6/11. Tafsiri iliidhinishwa: 6/11. Tafsiri ya First Presidency Message, January 2012. Swahili. 10361 743 3

UJUMBE WA MWALIMU MTEMBELEZI, JANUARI 2012 Kutunza na Kuhudumu kupitia Ufunzaji wa Mwalimu Mtembelezi Soma kifaa hiki, na kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe. Imani Familia Usaidizi fadhili [umaanisha] zaidi Usana kuliko hisia ya huruma, alifunza Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza. Ufadhili huzaliwa na imani katika Bwana Yesu Kristo na ni zao la Upatanisho Wake. 1 Kwa kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, ufunzaji wa ualimu tembelezi unaweza kuwa ufadhili katika matendo, njia muhimu ya kufanya imani yetu kwa Mwokozi. Kupitia kwa ufunzaji wa ualimu tembelezi, tunaweza kutoa utunzaji kwa kuwasiliana na kila dada, kushiriki ujumbe wa injili, na kutafuta kujua mahitaji yake na ya familia yake. Ualimu tembelezi umekuwa kazi ya Bwana tunapoweka mwangwi wetu kwenye watu badala ya takwimu anaelezea Julie B. Beck, rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Kwa kweli, ualimu tembelezi hauwezi kumalizika kamwe. Zaidi ni njia ya maisha badala ya shughuli. Kuhudumu kwa uaminifu kama mwalimu mtembelezi ni ushuhuda wa ufuasi wetu. 2 Tunapotoa utunzaji wa daima na wa maombi, tunajifunza jinsi ya kuhudumu vyema kwa na kukidhi mahitaji ya kila dada na familia yake. Kuhudumu kunaweza kuchukua maumbile mengi mengine makubwa na mengine sio makubwa sana. Mara nyingi vitendo vidogo vya huduma ndio tu kinachohitajika kuinua na kubarikiana: swala kuhusu familia ya mtu, maneno ya upesi ya kutia moyo, pongezi za kweli, kijibarua kidogo cha shukrani, simu ya muda mfupi, alifunza Rais Thomas S. Monson. Kama tutakuwa waangalifu na macho, na kama tutatenda kulingana ushawishi unaotujia sisi, tunaweza kukamilisha mengi mazuri.... Visivyohesabika ni vitendo vya huduma vinavyotolewa na jeshi kubwa la waalimu tembelezi wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. 3 Kutoka kwa Historia Yetu Mnamo 1843, washiriki wa Kanisa katika Nauvoo, Illinois, waligawanyishwa katika kata nne. Julai ya mwaka huo, viongozi wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama waliwateua kamati tembelezi la dada wanne kwa kila kata. Majukumu ya kamati tembelezi yalijumlisha kukadiria mahitaji na kukusanya michango. Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ulitumia hii michango kwa kusaidia wenye mahitaji. 4 Ingawaje waalimu watembelezi hawakusanyi michango tena, wanalo jukumu la kukadiri mahitaji ya kiroho na kimwili na kushughulika kukimu mahitaji hayo. Eliza R. Snow (1804 87), rais mkuu wa pili wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alieleza: Mwalimu... anafaa kuwa hasa na Roho wa Bwana sana, anapoingia katika nyumba ili kujua ni roho gani atakutana nayo hapo.... Omba mbele za Mungu na Roho Mtakatifu ili upate [Roho] ili kwamba uweze kutosheleza roho ambayo iliopo katika nyumba hio... na uweze kuhisi kuzungumza maneno ya amani na faraja, na kama utapata dada anayehisi baridi, mchukue hata kwenye moyo wako kama unavyomfanya mtoto kwenye kifua chako na kumchangamsha. 5 MUHTASARI 1. Henry B. Eyring, The Enduring Legacy of Relief Society, Liahona, Nov. 2009, 124. 2. Julie B. Beck, Relief Society: A Sacred Work, Liahona, Nov. 2009, 114. 3. Thomas S. Monson, Three Goals to Guide You, Liahona, Nov. 2007, 120 21. 4. Ona Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 105. 5. Eliza R. Snow, katika Daughters in My Kingdom,108. Kutoka kwa Maandiko Yohana 13:15, 34 35; 21:15; Mosia 2:17; Mafundisho na Maagano 81:5; Musa 1:39. 1

Ninaweza Kufanya Nini? 1. Ninafanya nini ili kuwasaidia kina dada zangu kuhisi kwamba mimi ni rafiki aliye na upendo na anawajali? 2. Ninaweza vipi kuwatazama na kuwatunza wengine vyema? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye reliefsociety.lds.org. 2012 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa Imechapishwa USA Kiingereza kiliidhinishwa: 6/11. Tafsiri iliidhinishwa: 6/11. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, January 2012. Swahili. 10361 743 2