BARUA YA TATU KWA SHEIKH UBAYD AL-JÂBIRĪ [AULIZWA SHEIKH UBAYD] NA Sheikh Sālim at-twawîl (hafidhahullāh)

Similar documents
John Lesson Eighteen Yohana Somo la Kumi na Nane

Imâm Al-Albâni, Katika Kumsifu Mwanafunzi Wake, Muheshimiwa Sheikh Ali Hasan 1

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF BOMAS OF KENYA

Ukoo Wake Na Kunasibika Kwake:

There is one God Mungu ni mmoja 1

Pre-Departure Program Swahili Unit 11 Worksheet UNIT 11: LOCATIVES, PREPOSITIONS, AND RELATIVE AND OBJECT INFIXES

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF

NEW INTERNATIONAL VERSION

Ukweli Uliopotea - Sehemu Ya Tatu

MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA KIRINYAGA YA KATI MWAKA WA 2013

Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtukufu Mtume

Tawasali. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags:

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

Ukweli wa hadith ya karatasi

MALAIKA: WAJUMBE WA MUNGU

BARAZA LA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA (Mawasiliano yawasilishwe kwa MSAJILI)

Bismillah ar-rahman ar-raheem SHAHADA 1 YALIYOMO

Sura al-ahzaab. Tafsiri na Maelezo. Abdilahi Nassir

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

ZABURI 91 mstari 1. KJV-lite VERSES

EVANGELISM FOR CHRIST UINJILISTI KWA AJILI YA KRISTO

Khadija-tul-Kubra. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Published on Books on Islam and Muslims Al-Islam.org (

Published on Al-Islam.org ( Home > Mahari ya Damu > Mahari ya Damu. Mahari ya Damu

DINI JE, DINI NI MUHIMU?

February 9, 2017 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 16 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY

HAKIKA YA AHMADIYYA. Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania

AHMAD AL-RAYSUNI. SWAHILI VERSION idara ya Lugha na ukalimani ya Chuo Kikuu cha waislamu cha Morogoro. IIIT Mfululizo wa Vitabu kwa Muhtasari

NEW LIFE IN CHRIST MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO

Zanzibar itafutika-mwanasheria

Imam Mahdi katika Usunni Na Ushia

Shaykh Muhammad b. Hādi al Madkhalī - As Recommended By The Kibār al Ulema

YA AL HABBIB SAYYEID

BRIXTON MASJID NEEDTO ISSUE ABAYĀN?!

Toleo la kwanza: June, 2007 (Jamaadi Aakhar, 1428) Vitabu ii.

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MANDERA CENTRAL CONSTITUENCY, HELD AT RHAMU

NEW INTERNATIONAL VERSION

Kitabu Changu cha Mistari ya Biblia Swahili

Rainbow of Promise Journal

Gazeti la kwanza la Kiislam kutolewa kwa lugha ya Kiswahili - mwaka 1936

Kuishi Maisha Tele. Katika mwanzo wa mwaka mpya, Niliwapa changamoto

Five Important Issues Regarding Jarḥ wa Ta dīl

WHO PRECEDED IMĀM AL- ALBĀNĪ REGARDING THE PROHIBITION OF FASTING ON SATURDAYS EVEN IF IT FALLS ON THE DAY OF ĀSHŪRĀ OR THE DAY OF ARAFAT?

ON REQUESTING OTHERS TO GET INVOLVED IN SCHOLARLY DISPUTES; JARH WA T- TA DEEL AND THE IMPORTANCE OF THE SCHOLARS VERIFYING REPORTS 1

Je, Umesikia Juu Ya Kanuni Nne Za Kiroho?

HALI YA UISLAMU. Maelezo ya kumsaidia Mkristo aufahamu Uislamu

Uwezo Kenya National Learning Assessment 2014

MOROGORO JARIDA LA. ISSN Toleo Na.4 Julai 2005 BODI ZA AFYA ZA WILAYA - SAUTI YA WANANCHI

UWAJIBIKAJI NDANI YA JESHI LA POLISI

IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE.

In Search of Contact: Rhetorical Questions in the Communicative Frame of the Funeral Sermon

Ujasiri wa Kimaadili. Mojawapo ya madhumuni ya maisha ya duniani

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS IJARA CONSTITUENCY AT IJARA BARAZA PARK

HAKIBulletin RAIS AMTEUA PROF. JUMA KUWA JAJI MKUU WA TANZANIA. Ndani: JARIDA LA MAHAKAMA YA TANZANIA

TUMERITHI TUWARITHISHE

2002 Version of the Basic Talk on "Using African Proverbs, Sayings, Idioms, Riddles, Stories, Fables, Play

WELCOME TO GOD S SERVICE A.C.K. ST. LUKE S PARISH UMOJA & TENA CHURCH QUOTE OF THE WEEK PRAYER OF THE DAY

REPUBLIC OF KENYA COUNTY ASSEMBLY OF KILIFI THE HANSARD. Wednesday, 29 th March, 2017

Mashairi ya Masaibu ya Karbala

NGUO-NYINGI MKOTI: MWANZISHAJI WA MJI WA NGOJI (ANGOCHE)

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

HOTUBA YA JAJI MKUU MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA SIKU YA SHERIA, DAR ES SALAAM, TAREHE 1 FEBRUARI, 2018

What Shaykh Hamad al-ansaari 1 said. About Knowledge 2. Compiled & Translated. Abbas Abu Yahya

Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya

NAIROBI CITY COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

TALKING ABOUT ONESELF TO ACT IN THE WORLD: A SWAHILI AUTOBIOGRAPHY (SHAABAN ROBERT, MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI

JUNE 4, Acts 2:1-12 and Offering...Pastor Maromy Samuel All Hail the Power of Jesus Name led by Haitian Congregation Worship Team

MAOMBI YA QUR'AN TUKUFU SHEIKH MUZAFFAR AHMAD DURRANI

HOLY COMMUNION ACCORDING TO THE KENYAN RITE

DID IMĀM AL-ALBĀNĪ JUMP TRAFFIC LIGHTS IN HIS CAR?

Our Dawah (parts excerpted from the dawah of AI-' Allaamah Muqbil Ibn Haadee ai- Waadi'ee and others from the A'immah of the SaIaf)

Foundations of The Creed of Ahl as-sunnah wal-jamā ah Part 1

2

KITABU CHA MAFUNZO KWA WATOA DAWA KATIKA MADUKA YA DAWA MUHIMU

TAUS RETREAT NEWS LETTER # 1

Vitendawili Vya Swahili

ON THE RULING OF WOMEN DRIVING 1

In defence of the two Sheikhs: Ahmed Bazmool & Muhammad al-anjari (May Allah preserve them) الدفاععنالشيخين:أحمدبازمولومحمدالعنجريحفظهماهللاتعالى

A SECOND LETTER TO DR MUHAMMAD BIN H D AL- MADKHAL 1

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

The Virtues of The Qur ān and The Types of Abandonment of It

THM Sadaqa Group, INC. Working together is a part of the puzzle!

Muslim School Oadby Shabaan 1436

MASHAIRI YA WAADHI "VERSES OF ADMONITION": the people of Mombasa rebuked by P J. L Frank! and Yahya Ali Omar

Day 5 - Bite Size Ramadan A.H. - Miraath Publications

Al-Aqidah Al-Tahawiyyah [Sharh Al-Maydani] Introduction, Part Three Monday 7pm 9pm. Course link:

HAKIBulletin JAJI MKUU AWAASA WAHITIMU WA SHERIA KUJIENDELEZA KITAALUMA HALIUZWI! BENKI YA DUNIA USULUHISHI MUAFAKA MAHAKAMA MAWAKILI MAHAKAMA KUU,

Ahadi za Serikali II. Zimekusanywa na HakiElimu Agosti 2007

VACATION BIBLE SCHOOL VBS. Newsletter. #Rebuilding through prayer, hard work & perseverance.

WELCOME TO GOD S SERVICE ACK ST. LUKE`S PARISH UMOJA Theme: Endeavoring to touch the heart of God, (Matt 25:40). Kuazimia kumpendeza Mungu

No. Book Name Category Type Price 1 AFYA MARIDHAWA -1 SWAHILI SUBSCRIPTION 2, AFYA NA UZIMA SWAHILI SUBSCRIPTION 8,500.00

MRADI WA METHALI (SANALASKUJA PROJEKTI)

ADVICE TO THE BROTHERS IN EUROPE TO BENEFIT FROM SHAYKH HAYTHAM SARH N AND NOT TO TURN TO AHMAD

Till death do us part...!

Chapter 9 WHY THE SALAFIS ARE NOT A TERROR PROBLEM

Ezra 3 Lessons Download or Read Online ebook ezra 3 lessons in PDF Format From The Best User Guide Database

The Advice. A caution against some newly invented methodologies that have arisen under the banner of Salafiyyah!

TAARIFA YA HISTORIA YA MKOA WA MWANZA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Celebrating Milad e Mustafa

Fiqh Of Worship. By Sheikh Muhammad Salih Ibn Al-Uthaymeen

Was al-isrā wa al-mi rāj a bodily or spiritual journey?

Transcription:

BARUA YA TATU KWA SHEIKH UBAYD AL-JÂBIRĪ [AULIZWA SHEIKH UBAYD] NA Sheikh Sālim at-twawîl (hafidhahullāh) 8 December, 2014 Posted by Salafibayaan ClarificationsRefutations 1223 views Nauliza suali: Muheshimiwa Sheikh Ubayd, Allâh Akuafikie kwa kila kheri, unamfanyia tabdi Sheikh Sālih bin Abdul Azîz Āli Sheikh, na ukamuorodhesha na Jam iyyah Ihyā ut-turāth? Jee, Sheikh Sālih ametumbukia kwenye uzushi? Jee kuhusu safari za mara kwa mara za Sheikh AbdurRazzāq kuwazuru Jam iyyat Ihyā ut-turāth?... kwa kujiegemeza juu ya fatwa za Shaykh AbdulMuhsin al- Abbād, unamfanyia naye tabdi? Muheshimiwa Sheikh, tafakari na uzingatie kuhusiana na hali ya Sheikh, al- Allāmah Sālih bin Fawzān al-fawzān, aliyekuzidi umri na ilmu ewe muheshimiwa sheikh. Angali, juu ya yote hayo, hatumuoni wala kumsikiya akijiingiza kwenye matukio ya Libya, fitna za Yemen, akimfanyia mtu yoyote kutoka Kuwait - tabdi, au akitoa amri yakwamba mwanamke katika nchi ya Emirates asusiwe au akimuhusisha mtu yoyote awe ndiye msimamizi juu ya wengine katika nchi za Uropa. Muheshimiwa Sheikh, sisi twasubiri jawabu kutoka kwako juu ya masuali haya matano, kwani wale wanaojinaki nafsi zao kuwa ni supper Salafi wameshindwa kuyajibu. Kila Sifa njema zinamstahiki Allâh peke Yake, na swala na salamu zimshukie yule ambaye baada yake hapana mtume mwengine; Ammâ ba d: 1

Hii ni barua ya tatu ninayomuandikia muheshimiwa Sheikh Ubayd bin Abdullāh al- Jābirī, Allâh Amuhifadhi na amtengezee niya yake na kizazi chake. Namuomba Allâh aifanye iwe na manufaa kwa muandishi na mwenye kuisoma. Nasema ndani ya barua hiyo: BISMILLÂHIR RAHMÂNIR RAHÎM Kutoka kwa Sālim bin Sa d at-twawîl, Imfikie Muheshimiwa Sheikh Ubayd bin Abdullāh al-jābirī, Allāh akuafikie katika kila kheri. Amma ba d: Baadhi ya ndugu kutoka nchini Kuwait wamejaribu kuwatahadharisha watu kutokamana na da wah yetu na mafunzo yetu na wakauzuiya wao peke yao U- salafiyyah asiingie mwengine. Wamejisifu nafsi zao kwa sifa ambazo kulingana na ninavyojua mimi hapajawahi kutokea tangu zama zilizopita, wakajiita wao wenyewe ma-salafi khaswa na ma-salafi imara. Amesema Allâh kwenye Kitabu Chake: Wala musijisifu nafsi zenu; Yeye ndiye anayewajua anayemcha Yeye. [an-najm (53): 32] ;(سبحانه وتعالى) Na akasema Allâh Wewe hujawaona wale ambao wanajitakasa nafsi zao? Bali, Allâh anawatakasa awatakao. [an-nisā (4): 49] Twamuomba Allâh atulinde. Watu wa kawaida katika kundi hili dogo ni vijana wenye umri mdogo, wana fahamu za kijinga, na wanaongozwa na mfanyi biashara fulani asiyekuwa na haja ya kutafuta ilmu na zaidi ni kwamba hakuna kujitosheleza kwao. Kwahiyo, yeye anatafuta msaada kutoka kwa watu wengine, mara kwa ndugu Ahmad Bāzmūl, na mara nyengine kwa Shaykh Muhammad bin Hādī, na mwisho kutoka kwako wewe binafsi, muheshimiwa. Kwa masikitiko, wameweza kusababisha ufisadi mkubwa baina yetu na baina ya Mashekhe kwa kusambaza uvumi ambao uliowafanya wakawa mashuhuri isipokuwa kwa idadi chache kama alivyokadiria Allâh. Nimemkumbusha kuhusu Allâh kwa mara nyingi na nikamnaswihi na kumpa dalili kutoka katika Kitâb na Sunnah kuhusiana na uharamu wa kueneza uvumi, licha ya yote hayo, yeye aliendelea tu kukaidi kwenye madhambi haya makubwa, twamuomba Allâh atuhifadhi. Namuomba Allâh aturuzuku na toba ya kihakika kabla ya mauti. Na uwajibikaji wa kisheriya ambao aliotufaridhia Allâh ni kwamba tunapaswa kuthibitisha habari za uvumi ili hukmu yetu isimame wima, au hali sio hivyo muheshimiwa Sheikh? Msambazaji mkubwa wa uvumi amedai yakwamba mimi nina mafungamano na Jam iyyat Ihyā ut-turāth na kama yalivyo matokeo yake, akanizungumza kwako na kutokana na maneno yake nawe ukanizungumza, Eeh Sheikh 2

Ubayd, Allâh akusamehe wewe na wazazi wako. Vilevile akanifungamanisha mimi na wao kutokana na baadhi ya maneno niliyowahi kuandika kwenye makala ambapo nilipoyataja majina ya baadhi ya Mashekhe wa Jam iyyat Ihyā ut-turāth kwa wema. Kwa uhakika, sifa tu ya kawaida kwa Muislamu hailazimu kufukuzwa kutoka katika U- Salafiyyah au kutoka katika Sunnah. Kwahivyo mfumo huu ni kutia chumvi tu na hili huwenda likasababisha msukosuko kwa mwenye kufanya hivi, lakini Wallâhi, muheshimiwa Sheikh, mimi sitamani kusababisha msukosuko kwako. Lakini hata hivyo, ndugu wenye upendeleo, wanaojiita wao wenyewe kuwa ni ma-salafi imara, hao ndiwo waliokutumbukiza wewe kwenye msukosuko huu. Mimi niliwauliza baadhi ya masuali, lakini walishindwa kuyajibu, na kwa sababu hiyo nimeyaleta masuali hayo kwako wewe, ewe Muheshimiwa Sheikh, Allâh akuafikiye. Huwenda nikasoma na wewe kutokamana na jawabu lako utakaponikirimu kunitumia au unaweza kuyasambaza majibu yako kila mahali ili ipatikane faida zaidi; Suali La Kwanza: Sheikh Sālih bin Abdul Azeez Āli Shaykh alifanya ziyara katika nchi ya Kuwait, yeye ni Waziri wa Waqf [na mas ala ya Uislamu] katika mamlaka ya Ufalme wa Saudi Arabia, Allâh amuhifadhi. Lengo kubwa lilikuwa ni kuizuru Jam iyyat Ihā ut-turāth na alikuwa pamoja na Sheikh Abdullāh al-manī,, Allâh amuhifadhi. Sheikh Sālih alizungumza maneno kuihusu Jam iyyat Ihyā ut-turāth na haya ndiyo aliyoyasema: Bismillāh ir-rahmān ir-rahîm, Kila sifa njema zinamstahiki Allâh, Mola wa Ulimwengu wote; Nashuhudia yakwamba yakwamba hapana mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh Peke Yake asiyekuwa na mshirika. Nashuhudia yakwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume, swala na salamu zimshukie yeye, jamii yake na maswahaba zake kwa salamu za zaidi, amma ba d: Mimi niko katika upeo wa furaha kwa kuwepo miongoni mwa ndugu zangu na vipenzi wangu hapa kwenye Jam iyyah hii iliyobarikiwa ambayo kwa kawaida sisi twaiona kuwa ni moyo unaopiga kwa kazi ya hisani ya ki-salafi kote ulimwenguni. Natumai yakwamba Allâh ataifanya masiku yake ya mbeleni yawe mazuri zaidi kuliko masiku yake yaliyopita, na atubariki sisi sote na ikhlâs na ukweli katika mazungumzo yetu na vitendo vyetu, na awathibitishe wasimamizi wake kwa usawa usiokuwa na hitilafu na awalipe wema kwa waliyoyafanya. Mwisho wa Nukuu Suali hapa ni kwamba: Muheshimiwa Sheikh, Allâh akuafikiye katika kila kheri, umemfanyia tabdi Sheikh Sālih bin Abdul Azeez Āli Shaykh na ukamuweka pamoja na Jam iyyah Ihyā ut-turāth? Jee, Sheikh Sālih ametumbukia ndani ya uzushi? Sisi twangoja jawabu lako muheshimiwa Sheikh, nakukumbusha kuhusu matamshi yako ya hapo awali:... msingi walio nao Ahlul ilm ni kwamba mwenye mafungamano na watu wazushi na asiwakanye na asiwasaidie wenye kuwakabili hao anafaa achukuliwe kuwa ni miongoni mwao. Hii ni hata kama atakua dhahiri yake anaonekana kuwa ni mtu mwema kutekeleza mambo yake kulingana na Sunnah kwani hili halimuokoi yeye kutokamana na kutumbukia kwenye uzushi yeye mwenyewe. Sisi tumeyazungumza kuhusu kundi la Ihya ut-turāth kwenye vikao vingi katika nchi ya Kuwait na hapa vilevile tumewazungumza kama inavyopaswa, kwahivyo yoyote apendae anaweza 3

kuirejelea hiyo, Jum iyyah hiyo [Ihyā ut-turāth] imo miongoni mwa vigawanyo vya Ikhwânul Muslimîn. Sasa utasema nini, ewe Muheshimiwa Sheikh? Kwani Sheikh Sālih bin Abdul Azeez Āli Shaykh hajui na hafahamu ukweli wa mambo? Au ana dhana njema juu yao akayakataa ya kutoka kwao? Juu ya yote hayo, ufahamu wangu ni kwamba mimi sikubaliani na njia ambayo Sheikh Sālih alivyowasifu Jam iyyat Ihyāt ut-turāth. Suali La Pili: Nilisikiya rikodi itokayo kwako hapa, imeulizwa; Mimi nina suali kuhusu hali ya baadhi ya Mashekhe, Sheikh AbdurRazzāq al- Abbād al- Badr? Jawabu: [kutoka kwa Sheikh Ubayd]: Mtu huyu ni mtu wa Sunnah, walillâhil-hamd; ni maarufu sana. Sijafikiwa na habari za uharibifu kwenye misingi, wala hukmu za nguzo kutoka kwake. Suali langu kwako, Ewe Muheshimiwa Sheikh Ubayd: Jee, kuhusiana na safari za Sheikh AbdurRazzāq za mara kwa mara kwenda Jam iyyat Ihyā ut-turāth, na amewahi kuwa na maandalizi yenye kujulikana mno na wao? Ni kwanini hukmu zako zilizotangulia zisihusishwe kwa Sheikh AbdurRazzāq bin AbdulMuhsin al- Abbād al- Badr? Jee, Sheikh AbdurRazzāq ametumbukia kwenye uzushi? Au yeye ana hali maalum isiyoshirikishwa kwa wengine? Haya yote, ingawaje mimi namzingatia Sheikh AbdurRazzāq kuwa ni mtu aliyebarikiwa, na wala mimi simsifu mtu yoyote zaidi ya Allâh, Allâh ameleta faida kubwa sana kutokana na ziyara zake katika nchi ya Kuwait, UAE na Bahrain, Allâh amzidishie katika kheri. Sisi twangoja jawabu lako, Ewe Muheshimiwa Sheikh Ubayd, Allâh akuhifadhi. Suali La Tatu: Labda Sheikh Ubayd wewe wamjua Sheikh, Dr Muhammad bin Umar al- Bāzmūl, ambaye mimi namzingatia kuwa ni mtu wa kheri. Ameshafanya ziyara katika nchi ya Kuwait zaidi ya mara moja na amejihusisha na Jam iyyat Ihyā ut-turāth zaidi ya mara moja. Kwa hakika, yeye ana mafungamano na baadhi ya Ikhwânul Muslimîn walioko Kuwait. Baadhi ya ndugu fulani wametafuta usaidizi wa ndugu yake, Dr Ahmad bin Umar Bāzmūl, ambaye aliyewahi kutangaza yakwamba Jam iyyat Ihyā ut-turāth ni wazushi. Suala langu ni: Ni nini hukmu ya Shaykh Muhammad Bāzmūl kuhusu safari zake za kwenda Jam iyyat Ihyā ut-turāth na kushirikiana nao kwenye baadhi ya harakati zao na kutowafanyia tabdi? Tukiwa twajua yakwamba haya yamethubutu kwa njia ya mawasiliano ya sauti na kuona. Sisi twangoja jawabu lako, Ewe Muheshimiwa Sheikh Ubayd, Allâh akuhifadhi. Ikiwa katika fahamu zako kwamba wale vijana wanaojiita ma-salafi imara au masalafi khaswa, wameshindwa kulijibu suala hili, labda huwenda wakapata jawabu kutoka kwako? Namuomba Allâh Akuafikie kwenye haki. Suali La Nne: Ndugu Muhammad bin Uthmān al- Anjarī alipokuwa amefuatana na Ahmad bin Husayn as-subay ī alijitolea kwa Mashekhe wawili, Dr Falāh Ismā īl Mandikār na Dr Abū Anas Hamad al- Uthmān, na mimi nikiwa mtu wa tatu, yakwamba tujifungamanishe pamoja na Jam iyyat Ihyā ut-turāth, tupate kushindana nao katika upigaji wa kura ili tupate kushinda na kuweza kutumia nyadhifa za baraza lao katika usimamizi wake na halmashauri ya kifedha, kama wanavyodai, ati kuusaidia U- Salafiyyah. Yeye [Muhammad al- Anjarī] alitaka kutafuta usaidizi wa binamu yake, 4

Mishārī bin Jāsim al- Anjarī, ambaye kwa wakati huo alikuwa ni Mbunge! Sisi tukaikataa nafasi hii kabisa, na kila sifa njema inamstahiki Allâh, na mimi ndiye niliyekuwa mkali zaidi katika kuikataa fikra hii isiyofaa, kwani sisi ni wanafunzi wa kiilimu na lililotuhusu sisi zaidi lilikuwa ni kuilingania dini ya Allāh, kufundisha na kusoma. Sisi hatushughuliki na kujipatia wadhifa na michango, na wala hatujiingizi kwenye upigaji wa kura, tunaloliomba sisi ni kuwa na msimamo hadi kufa. Suala langu, Ewe Muheshimiwa Sheikh Ubayd ni: kama ambavyo huyu ndugu Muhammad bin Uthmān al- Anjarī, hakutangaza toba yake kutokamana na maombi haya [ya kujiingiza kwenye uongozi wa upigaji wa kura kwenye wadhifa wa usimamizi wa Jam iyyat Ihyā ut-turāth], ambao hakufaulu kuupata, na wala hakuonyesha majuto yoyote sasa jee, hukmu yako iliyotangulia uliyoitaja inafaa kutumiwa kwake? Suali La Tano: Ewe Muheshimiwa Sheikh Ubayd, Allâh akuafkie kila la kheri, iwapo baadhi ya wanafunzi wa ki-ilimu watakapokuwa ni wenye kutafuta hukmu kutoka kwa Sheikh wako, Muhaaddith, al- Allāmah Shaykh AbdulMuhsin al- Abbād al-badr kuhusiana na hukmu ya kushirikiana na Jam iyyat Ihyā ut-turāth, bila ya shaka atawaruhusu. Sasa kwa msingi wa fatwa ya Shaykh AbdulMuhsin al- Abbād, jee, wewe unamfanyia tabdi kwa hilo? Muheshimiwa Sheikh, sisi twasubiri majibu ya masuali haya matano, kwani wale wenye kujiita yakwamba wao ni ma-salafi- halisi au ma-salafi-imara wameshindwa kuyajibu. Wale ambao walioutawala U-Salafi wao peke yao, na wala sio Waislamu wengine... Muheshimiwa Sheikh Ubayd, Allâh akuafkie na akuinue daraja yako, mimi nitataja baadhi ya mas ala muhimu kwako, ambayo natumai utafungua kifua chako uyasikize: La Kwanza: Natumai Muheshimiwa Sheikh yakwamba unaheshima kubwa juu ya ma-imâm waheshimiwa wanaokumbukwa pindi inapokuja mas ala ya kutoa naswiha na kutubia kuliko kukatana, kutahadharisha, kuwatoa watu na kuonya! Miongoni mwa watu katika zama zetu, aliyetoa naswiha nyingi sana kwa Ummah alikuwa ni Baba Muheshimiwa, al- Allāmah Shaykh Abdul Azîz bin Bāz (rahimahullāh). Alikuwa akiwanaswihi viongozi, wanavyuoni, walinganizi na wanafunzi wa ki-ilimu, ewe Muheshimiwa Sheikh, bila ya kufanya unayoyafanya wewe ya tabdi, tadlîl, amri ya kususia na kujitenga. Mifano ya naswaha kutoka kwa Sheikh Abdul Azîz bin Bāz (rahimahullāh) ni mingi, tena iliyo mshuhuri sana hata haina haja ya kusimuliwa, kwani Dini ni Naswiha, na wale wenye kutoa naswiha hawana mafungamano na wale ambao wanaowapa naswiha hizo, kwa maana yakwamba wanawaamrisha wao wazikubali naswaha hizo na lau kama hali si hivi, basi patakuwa na tafauti gani baina ya kutoa naswiha na hukmu ya Qâdhi au kiongozi aliye na mamlaka?! La Pili: Muheshimiwa Sheikh, hebu tafakari na uzingatie juu ya hali ya Shaykh, al- Allāmah Sālih bin Fawzān al-fawzān aliyekuzidi wewe kwa umri na ilmu, Muheshimiwa Sheikh. Juu ya yote hayo, hatumuoni wala kumsikia akijiingiza kuhusu matukio ya Libya, fitna za Yemen, kumfanyia tabdi mtu yoyote kutoka Kuwait, au kuamrisha yakwamba mwanamke wa Emirates asusiwe au kumuwakilisha mtu yoyote awe na mamlaka juu ya wengine katika nchi ya Ulaya. 5

La Tatu: Muheshimiwa Sheikh Ubayd, Allâh akuhifadhi, suali kutoka kwa ndugu wa Uropa yamenifikia, ambayo na mimi nayafikisha mbele yako, kwani huwenda ukatufaidisha kwa ilmu yako kutokana na jawabu lako; Anauliza muulizaji: Baadhi ya ndugu fulani wanawatisha wenzao kwa Mashekhe wakiwaambia: Tutayatuma maneno yako na vitendo vyako kwao, hata pia pale unapokwenda, unaemsikiza, [mgeni yoyote] unaempokea, unaemkaribisha, ili watoe hukmu kukuhusu wewe, au tahadhari ili tukutupilie mbali, na tutasubiri kauli ya ma- Ulamaa kukuhusu wewe. Suali ni kwamba; Jee, huku kuwaogopa Mashekhe ni kumshirikisha Allâh? Allāhul-Musta ān, kweli huu ndio U-Salafiyyah ambao Allāh alomtumiliza nao Mtume (SwallAllāhu alayhi wassallam)? Twasubiri kauli yako Muheshimiwa Sheikh. La Nne: Muheshimiwa Sheikh Ubayd, Allâh akuafkie kila la kheri, tahadhari na watu wa Namîmah, jitahadhari na orodha hiyo ya watu hata kama wao unawaona kuwa wanadhihirisha islahi na wakadai kuwa ni ma-salafi khaswa na ma-salafi Imara. Jitahadhari nao hata kama unaona wanadhihirisha kujali maslahi yako ndani ya nyoyo zao na maslahi ya Da wah. Jitahadhari nao hata kama wao ni katika watu wenye mkuruba zaidi na wewe. Amesema Allāh وتعالى) (سبحانه katika kumuonya Mtume Wake chafu, kutokamana na watu wenye tabia hii (صلى اهلل عليه وسلم) Wala usimtwi i kila muapaji sana, aliye dhalili, msengenyaji (msemaji watu), aendaye akitia fitina, azuiaye kheri, anayedhulumu viumbe wenziwe, anayemu asi Allâh. [Al-Qalam (68): 10-12] Amesema Ibn Kathîr kuhusu maneno ya Allâh yasemayo; Aliye dhalili, msengenyaji (msemaji watu). Ni yule anayetembea baina ya watu na na kusababisha ufisidifu baina yao na kusambaza maneno ili apate kuharibu uhusiano wao... La Tano: Zimenifikia mimi habari yakwamba mtu fulani mwenye asili ya Pakistan, mwenye hati ya uraiya wa Uingereza na anaishi kwenye Mji wa Birmingham (Uingereza) aitwae AbdulWāhid kwa kunya lake Abu Khadijah amedai yakwamba amejipatia fatwa au jukumu kutoka kwako wewe ili awe ni msimamizi wa mas ala ya ndoa na talaka, na kwamba yeye ndiye mwenye mamlaka wa mambo hayo?! Sasa, awapo yeye [Abu Khadijah] ni mtu mrongo, basi wewe utahitajika ujitokeze uthibitishe kutoka kwake, Yâ Sheikh Ubayd, upate kumuuliza kuhusu tabia yake ya dhulma anayoitekeleza dhidi ya wenye kwenda kinyume naye. Ni ndoa ngapi alizozivunja, na ni 6

jamii ngapi alizozitawanya? Iwapo ni kweli yakwamba alipata tazkiya kutoka kwako, basi Wallâhi mimi sijui, iliwezekanaje kwako wewe kumpa majukumu kama hayo?! Mimi natumai yakwamba wewe kujatoa ruhusa kwa mtu asiyejulikana aliposoma mahali gani. Allāhu Musta ān.[1] [1]: Sheikh anayeheshimika na Muhaddith anayefundisha katika Haram al-makki, Sheikh Wasiullāh Abbās, vilevile alituma mashtaka kama hayo dhidi ya mtu huyu wakati alipofanya ziyara katika nchi ya Uk. Muhusika azungumzwaye hapa, hatahivyo, amekanusha kuhusika katika mas ala ya majukumu ya kuozesha watu. La Sita: Nimezipata habari kuhusu ulivyonisema mimi yakwamb: Aliyeyasema maneno haya, mimi nimemjua kwa muda wa miaka 21, yeye ni mtu wa kutoka Kuwait, aliwahi kuwa na sisi kisha akachukuliwa na hili lililompotosha. Sasa mimi nasema. Ewe Muheshimiwa Sheikh; Mimi nilikuwa wapi? Ni lini hapo? Ilikuwaje? Jee, sisi tumo ndani ya Hizb au ta sisi? Jee, sisi tumefanya bay ah au kula kiapo? Maneno yako yananishangaza sana kunihusu mimi na wengine, labda unaweza kuyachuja maneno yako, ewe muheshimiwa Sheikh, natumai pengine uliteleza ulimi wako. Muheshimiwa Sheikh Ubayd, Allâh na akuhifadhi, mimi nitakukumbusha kuhusu maneno ya Allâh; Hata anapofikia baleghe yake na akawa mwenye umri wa miaka arubaini, (Mtoto mwema) husema: - Ee Mola wangu! Niwezeshe nishukuru ne ema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu, na niwezeshe nifanye vitendo vizuri unavyovipenda, na unitengenezee watoto wangu; kwa yakini ninatubu kwako; na hakika mimi ni miongoni mwa waliosilimu (walionyenyekea). [al-ahqāf (46): 15] Amesema Allâh;...na akawa mwenye umri wa miaka arubaini... Muheshimiwa Sheikh, sasa hivi wewe umekurubia umri wa miaka thamanini, na Mtume ( ) amesema: Umri wa Umma wangu ni baina ya siti na sabiini, na wachache mno wataishi zaidi ya hapo. Imepokewa na at-tirmidhi, kutoka katika hadith ya Abu Hurairah ( ) No. 3550 na ikaorodheshwa kuwa Hasan na Sheikh al- Albâni. Muheshimiwa Sheikh, wewe ni miongoni mwa wachache kama alivyokuwa akisema Sheikh al-albâni kujihusu yeye mwenyewe, kwahivyo wacha ukumbusho wako mzuri na ndugu zako na watoto wako miongoni mwa Ahlus Sunnah ambao uliowasifu kwa matamshi mabaya kama vile, huyu ni mpotofu, na yule ni ikhwânî, na huyo amepotea na kadhaalika. Si jambo la kufichika kutoka kwako yakwamba rifq (sifa 7

ya upole) haipatikani kwa yoyote isipokuwa humrembesha, na haiondolewi kutoka kwa yoyote isipokuwa humuharibu. Neno jema ni swadaka kwahivyo wanaswihi ndugu zako na watoto wako na waombee du â wapate taufiki na usawa kwani wao wanakumpenda na itakuwa ni uzito kwao wao iwapo utakatana nao. Namuomba Allāh aniongoze mimi, wewe na Ahlus Sunnah, atuunganishe kauli yetu, azifungamanishe nyoyo zetu pamoja, atusuluhishie hali zetu na atusaidie dhidi ya wale ambao wenye kutupinga sisi. Na kila sifa njema zinamstahiki Allâh, katika mwanzo wake, mwisho wake, na katika dhahiri yake na siri yake, na twaomba swala, amani na baraka zimshukie Mtume Muhammad اهلل عليه وسلم),(صلى âli zake na Maswahaba zake wote. Sheikh Sālim at-twawîl, Wa Aydhan Risālah Lam Yahmiluhā al-bareed ilā Fadeelat ish- Shaykh Ubayd bin Hādī al-jābirī hafidhahu Allāh, 3-3. [Na vilevile barua ambayo isiyoweza kutumwa kwa Posta kwa Sheikh Ubayd al-jābirī, Allâh Amuhifadhi, Brua ya 3 rd katika 3]. Tarehe 2 Safar 1436 AH/23 November 2014 CE, Angalia kwenye : http://www.saltaweel.com/articles/374 Imefasiriwa na AbdulHaq al-ashanti Tafsiri kwa Kiswahili: Abu Farida Muhammad Basawad The Qur an And Sunnah Society od East Africa. [QSSEA] Mombasa, Kenya 8