YA AL HABBIB SAYYEID

Similar documents
Pre-Departure Program Swahili Unit 11 Worksheet UNIT 11: LOCATIVES, PREPOSITIONS, AND RELATIVE AND OBJECT INFIXES

John Lesson Eighteen Yohana Somo la Kumi na Nane

NEW INTERNATIONAL VERSION

There is one God Mungu ni mmoja 1

Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtukufu Mtume

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF BOMAS OF KENYA

Published on Al-Islam.org ( Home > Mahari ya Damu > Mahari ya Damu. Mahari ya Damu

MALAIKA: WAJUMBE WA MUNGU

BARUA YA TATU KWA SHEIKH UBAYD AL-JÂBIRĪ [AULIZWA SHEIKH UBAYD] NA Sheikh Sālim at-twawîl (hafidhahullāh)

NEW INTERNATIONAL VERSION

Sura al-ahzaab. Tafsiri na Maelezo. Abdilahi Nassir

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF

Imâm Al-Albâni, Katika Kumsifu Mwanafunzi Wake, Muheshimiwa Sheikh Ali Hasan 1

Ukweli wa hadith ya karatasi

Ukweli Uliopotea - Sehemu Ya Tatu

MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA KIRINYAGA YA KATI MWAKA WA 2013

Khadija-tul-Kubra. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Published on Books on Islam and Muslims Al-Islam.org (

Kitabu Changu cha Mistari ya Biblia Swahili

Toleo la kwanza: June, 2007 (Jamaadi Aakhar, 1428) Vitabu ii.

ZABURI 91 mstari 1. KJV-lite VERSES

Tawasali. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags:

HAKIKA YA AHMADIYYA. Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania

DINI JE, DINI NI MUHIMU?

Bismillah ar-rahman ar-raheem SHAHADA 1 YALIYOMO

NGUO-NYINGI MKOTI: MWANZISHAJI WA MJI WA NGOJI (ANGOCHE)

BARAZA LA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA (Mawasiliano yawasilishwe kwa MSAJILI)

Gazeti la kwanza la Kiislam kutolewa kwa lugha ya Kiswahili - mwaka 1936

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

Ukoo Wake Na Kunasibika Kwake:

Imam Mahdi katika Usunni Na Ushia

EVANGELISM FOR CHRIST UINJILISTI KWA AJILI YA KRISTO

February 9, 2017 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 16 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY

2002 Version of the Basic Talk on "Using African Proverbs, Sayings, Idioms, Riddles, Stories, Fables, Play

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MANDERA CENTRAL CONSTITUENCY, HELD AT RHAMU

IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE.

Zanzibar itafutika-mwanasheria

NEW LIFE IN CHRIST MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO

HALI YA UISLAMU. Maelezo ya kumsaidia Mkristo aufahamu Uislamu

AHMAD AL-RAYSUNI. SWAHILI VERSION idara ya Lugha na ukalimani ya Chuo Kikuu cha waislamu cha Morogoro. IIIT Mfululizo wa Vitabu kwa Muhtasari

Rainbow of Promise Journal

Uwezo Kenya National Learning Assessment 2014

Kuishi Maisha Tele. Katika mwanzo wa mwaka mpya, Niliwapa changamoto

Je, Umesikia Juu Ya Kanuni Nne Za Kiroho?

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS IJARA CONSTITUENCY AT IJARA BARAZA PARK

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

JUNE 4, Acts 2:1-12 and Offering...Pastor Maromy Samuel All Hail the Power of Jesus Name led by Haitian Congregation Worship Team

Ujasiri wa Kimaadili. Mojawapo ya madhumuni ya maisha ya duniani

Mashairi ya Masaibu ya Karbala

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

MOROGORO JARIDA LA. ISSN Toleo Na.4 Julai 2005 BODI ZA AFYA ZA WILAYA - SAUTI YA WANANCHI

2

NAIROBI CITY COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

TUMERITHI TUWARITHISHE

Vitendawili Vya Swahili

HAKIBulletin RAIS AMTEUA PROF. JUMA KUWA JAJI MKUU WA TANZANIA. Ndani: JARIDA LA MAHAKAMA YA TANZANIA

MANIFESTATION OF COMMON MAN LANGUAGE IN EPIC POEMS: A CASE STUDY OF UTENDI WA SIRI LI ASRARI

TALKING ABOUT ONESELF TO ACT IN THE WORLD: A SWAHILI AUTOBIOGRAPHY (SHAABAN ROBERT, MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

Ahadi za Serikali II. Zimekusanywa na HakiElimu Agosti 2007

WELCOME TO GOD S SERVICE A.C.K. ST. LUKE S PARISH UMOJA & TENA CHURCH QUOTE OF THE WEEK PRAYER OF THE DAY

Yassarnal Quran English

In Search of Contact: Rhetorical Questions in the Communicative Frame of the Funeral Sermon

HOTUBA YA JAJI MKUU MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA SIKU YA SHERIA, DAR ES SALAAM, TAREHE 1 FEBRUARI, 2018

UWAJIBIKAJI NDANI YA JESHI LA POLISI

HAKIBulletin JAJI MKUU AWAASA WAHITIMU WA SHERIA KUJIENDELEZA KITAALUMA HALIUZWI! BENKI YA DUNIA USULUHISHI MUAFAKA MAHAKAMA MAWAKILI MAHAKAMA KUU,

Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya

Ezra 3 Lessons Download or Read Online ebook ezra 3 lessons in PDF Format From The Best User Guide Database

MRADI WA METHALI (SANALASKUJA PROJEKTI)

TAUS RETREAT NEWS LETTER # 1

HOLY COMMUNION ACCORDING TO THE KENYAN RITE

No. Book Name Category Type Price 1 AFYA MARIDHAWA -1 SWAHILI SUBSCRIPTION 2, AFYA NA UZIMA SWAHILI SUBSCRIPTION 8,500.00

WELCOME TO GOD S SERVICE ACK ST. LUKE`S PARISH UMOJA Theme: Endeavoring to touch the heart of God, (Matt 25:40). Kuazimia kumpendeza Mungu

The Lord be with you And with your spirit

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

REPUBLIC OF KENYA COUNTY ASSEMBLY OF KILIFI THE HANSARD. Wednesday, 29 th March, 2017

To Masjid Al-Aqsa (in Jerusalem) and the 7 heavens. Which prophet was sent to Ad?

AND REACTION IN SWAHILI POETRY.

Was al-isrā wa al-mi rāj a bodily or spiritual journey?

(Cell) (Cell) (Cell) (Landline) (Cell)

Student Workbook 3 - Tārikh. Lesson 2 Building the Ka bah

The Noble Qur an. Medium H/B 1098pp 8.95 Product code: 1.01A. P/B 1104pp 7.95 Product code: 1.01B. The Noble Qur an

MAOMBI YA QUR'AN TUKUFU SHEIKH MUZAFFAR AHMAD DURRANI

MAWLANA OSMAN WALI ABD-U L-KARIM

Salih And Ibrahim (Stories Of The Prophets Of Islam) By Abdul Rahman Rukaini

5. Did Prophet Muhammad (S) come to the people Arabia only? No Allah (SWT) sent him to the entire humanity.

FRIDAY SERMON. Dua ; The Mukmin s weapon. Ustaz Ellyeen Amineen bin Mohd Salleh Pegawai Hal Ehwal Islam Pusat Islam Universiti Teknologi Malaysia

11 / PROPHET MUHAMMAD S.A.W. AND THE UNITY OF UMMAH USTAZ IBRAHIM KHALIL BIN ABDULLAH

UNIVERSITY GRANTS COMMISSION NET BUREAU

Hadith Hadith Sciences

IMAM ALI A.S. (Part 1) Power point realised by a Kaniz-e- Fatima Fi Sabilillah French version approved by Mulla Nissar Radjpar (Reunion Island)

Where is Africa? 2. What is African heritage? 3. What is the African heritage in the Bible? 6. What are African ways of worship?

knowledge devotion service

Past Paper Questions May/June 2009 to Oct/Nov 2016

Al-Huda Schools are proud to present the 15 th annual. Islamic Knowledge Contest Grade 2

The Event of Mubahila

Islamic Shia Ithna-Asheri Association of Edmonton

Al-Huda Schools are proud to present the 15 th annual. Islamic Knowledge Contest Grade 1

THE TRIALS OF DAJJAL

Sharh Arba'een an Nawawî COMMENTARY OF FORTY HADITHS OF AN NAWAWI By Dr. Jamal Ahmed Badi

Transcription:

YA AL HABBIB SAYYEID

. NA Yamefasiriwa kwa Kiswahili na: Al habbib Sayyeid Umar Bin Sayyeid Abdallah (Mwinyi Baraka). First addition. 03 Sept, 2005. 28 Rajab, 1426. HR. i

MANAQIB YA AL-MAARUF Baada ya yote haya ni Manaqibu ya Walii Mkubwa kabisa aliyetajwa kwa jina hapo juu, yaliandikwa na mmoja katika makhalifa wake wakubwa Sayyid Ahmad bin Abdul Rahmani Ibn Sultan Alawi. Yalifasiriwa na Al Allama Sayyid Kaab Ibn Sayyid Ahmad Zakiy Al-Masalah. Sasa inafasiriwa kwa Kiswahili na mtoto wa ndugu yake Walii huyo, Omar Abdallah Bin Sheikh Ahmad ambaye hujulikana kwa jina la Mwinyi Baraka. Huyu mfasiri kwa Kiswahili ameazimia dua zote aziache bila kufasiriwa kwani muhimu ni kulumiwa kama zilivyopokewa. ii.

MAISHA YAKE. Sasa naanzia: Utajo wa kuzaliwa kwake Mwenyi Ezi Mungu atakase siri yake Bwana Al-Maarufu alizaliwa mwaka Saf 1270 Hijra katika mtaa wa Bajanani, Moroni Ngazija. Alizaliwa katika nyumba iitwayo "Shashanyongo". Baba yake ndiye aliyemlea. Alisoma kuran Ngazija akawa anasoma kwa Tajwidi. Baadaye Baba yake alimpeleka Zanzibar si kwa jingine lolote ila kutafuta ilmu. Alikaa Unguja kiasi ya miaka mine, takriban akazijua vilivyo fani za Tajwidi, Fiqih, Nahw na kiasi cha kutosha katika ilmu za hadithi na kuran. Ilmu zote hizi alizichukua kutokana na mjomba wake Sayyid Ali Bin Sultan Ahmad. Wakati wa safari yake, Babu yake upande wa mama yake Sultan Ahmad alimwambia; "Tutafutie ilmu ya haqiq (undani wa mambo yaliyohusiana na Uungu) kwani sisi hatujui vilivyo". Baada ya kusoma ilmu hizo alirejea Ngazija, akashughulika kukunjua ilmu zote hizi na kuita watu kwa Mwenyi Ezi Mungu katika msikiti wa Ijumaa. Alianza kusomesha katika tafsiri ya kuran Jalalain katika wanafunzi wake waliosoma kwake fanni ni mwalimu wake wa Tajwidi Musa Bin Ahmad. Muhimu: Baba yake Sayyid, Mungu amuie Radhi ilikuwa hakupata mtoto mwanaume. Basi alipohiji akakusudia Madina kumzuru babu yake, Rehema ya Mwenyi Ezi Mungu na Amani yake ziwe juu yake, alimuomba Mwenyi Ezi Mungu katika Quba la mtume (SAW) amruzuku mtoto mwanaume kwa mke wake mlahirifu Mwana mkuu Bint Sultan Ahmad. Aliweka nadhiri hapo ikiwa Mwenyi Ezi Mungu kamruzuku mtoto mwanamme 1.

atapeleka pesa kidogo kwenye kuba la Mtume (SAW) kwa matumizi ya watumikiao alipolala Mtume. Mwenyi Ezi Mungu alipokea dua yake. Baada ya kurejea Ngazijah, mkewe alishika mimba akamzaa anayeandikwa habari zake hapa. Baba yake alimwita MA'ARUF. Na akapeleka zile pesa Madina kutekeleza nadhiri yake. Nasabu yake tukufu yeye ni Bwana wangu (Mwenyi Ezi Mungu atakase siri yake kubwa), Muhammed Bin Sheikh Ahmad Bin Sayyid Abubakar Bin Sayyid Ahmad Bin Sayyid Abubakar Bin Sayyid Abdallah Bin Sayyid Salim Bin Sayyid Ahmad Bin Sayyid Abdallah Bin Sayyid Ali Bin Alfakhir Ash- Sheikh Abubakar Bin Salim, Aliyetawafu Einat katika Hadhramaut. Hii ni kwa upande wa Baba yake, na kwa puande wa Mama yake, yeye ni mtoto wa Mwana Mkuu Bint Sultan Seyyid Ahmad na yeye ana nasibika na Abubakar Bin Salim. Ama mabibi zake wataharifu, mama yake baba yake Wamwinyi Bint Sayyid Eidarus anaye jukuliwa na Abubakar Bin Salim na mama yake ni Sayyidat Khadija Bin Sheikh Salim; na yeye vile vile anajukuliwa na Abubakar Bin Salim. Basi imejulikana kuwa nasabu yake amezungukwa na Sheikh Abubakar Bin Salim upande wa mabababa na upande wa mamama Mwenyi Ezi Mungu atunufaishe na yeye na wazee wake Amin. Wake zake watahilifu na utajo wa kubariki baba yake. Mke wake wa mwanzo ni mtoto wa ndugu yake mama yake Sayyidat Sittinaa Bint Sultan Sayyid Omar Bin Sayyid Hassan katika kabila ya Almasaiha BA-ALAWI ambaye baba yake ndie aliemposea na akamuoza baba yake mkewe Sultan Sayyid Omar alietajwa hapo juu kwa mahari ya wanawake mfano wake aliingia nyumbani hapo Moroni. Siku ya Tisa tangu kuingia nyumbani baba yake alifariki (Faida; Ijumaa ya mwanzo baada ya kuingia nyumbani Sayyidina Muhammed Bin Sheikh alimtuma mtu akamtakie Jokho kwa baba yake ili avae kwenda kuhudhuria sala. Sheikh Ahmad alimjibu "Mwambie mwanangu asubiri kwani Jokho hilo litakuwa lake baada ya siku chache. Siku hizo hizo mzee akafariki.- Nyongeza hii ni ya Mfasiri). Bibi huyu yaani Sayyidat Sittinaa alizaa nae watoto watatu Khadija, Hawdhat na Shama. Baadaye alimuoa Maryam Bint Beja, akazaa naye Sayyid Ahmad. Tena alimuoa Bint Sayyid Aqil na mwishoni kwa Ngazijah alimuoa bibi Halimah Bint Ilyas. 2.

Unguja alimuoa Bibi Khadijah Bint Ali aliezaliwa Ngazija na mama yake ni Mngazija alizaa naye Sayyid Ali na Sayyidat Batul. Baadaye alimuoa Bint Naqib Assayf Al-Kisadi akazaa naye Sayyidat Sharifah na Ismail ambaye alikufa mtoto hata baba yake hakuwahi kumuona ama Sharifah alikufa baada ya kufariki baba yake. Safari zake: Mwanzo alikwenda Unguja kutafuta elimu kama ilivyotajwa kabla katika safari zake. (Mwenyi Ezi Mungu amuilie radhi na amwidhishe). Ni safari ya Makka tukufu alikwenda kuhiji pamoja na mama yake na ukhti yake Sayyidat Alawiyya na waliyofuatana nae alipokuwa Makka alikutana na mmoja katika Mawalii wakubwa akawa humtukuza akamuusia achukue Tarika ya AL IMAM ASH-SHADHIL akampa khabari kuwa kufunguliwa kwake kumo katika Tarika hiyo mambo yakawa kama alivyomkhubiria Walii huyo, katika baadhi ya mikusanyiko yake na Walii huyo huyu Walii alimuuliza "Umekuja kwa sababu ya yule mgonjwa wa akili ambaye anazunguka Ngazija?" Na ilikuwa niya ya As-Sayyid ni kumuombea dua, yule walii alimkashif. Jawabu yake ilikuwa: "Naam". Akamjibu keshapona. Aliporejea kamkuta kweli keshapona kama alivyomwombea, Mwenyi Ezi Mungu atanufaishe kwa siri zao. Katika safari hii alikusudia Madina iliyojazwa Nuru ili kumzuru babu yake (S.A.W) huko alipokea vilitokea kwa Mungu kuletewa mbele ya Muhammed. Alikaa Madina siku kadha wa kadha katika baadhi ya ziara zake ndani ya Kuba la Mtume takatifu aliingia yeye na mama yake. Mama yake aliona ndani ya Kuba Mtu anapendeza, mzuri, anatabasam. Mama yake alimuuliza mtoto wake "Nani huyu? As-Sayyid Alimuashiria mama yake anyamaze. Walipo rejea huko walikoshukia alimwambia mamake "Yule mtu uliyemuona ni Mtume (S.A.W) mwenyewe kwani mahali pale haingii mtu. Alipomaliza ibada zake za hija na ziara aliingia Anzwani pamoja na mama yake na ukhti yake wakakaa huko siku kadha wa kadha yeye ndie wa mwanzo kuwapelekea Maulid ya Barzanji alikuwa anapenda kuyasoma na kuyahudhuria kwa taadhim na heshima kubwa alikuwa akikataza kucheka na kucheza na kutafuna tambuu wakati wa kuyasoma kwa kumuadhimisha mjumbe wa Mwenyi Ezi Mungu (S.A.W). Baada ya hapo alirejea kwenye watani wake hali ya kuwa ni 3

mwenye kutizamwa kwa jicho la kusaidiwa na kutengenezewa kutokana na bwana Muumbaji khalafu alisafiri kwenda Zanzibar akakutana na Sheikh Uways na akachukua Tarika ya Qadiria kutokana naye akarejea Ngazija baadaye akenda Nzwani wakati huo anadhikri kwa Tarika ya Qadiriya wala hakumpa yeyote Ijaza ya Tarika hiyo, bali baadhi ya nyakati alikuwa hujitenga faragha akadhikiri peke yake baadae hurejea kwa wapenzi wake. Aliporejea Ngazija haikuchukua muda mrefu ila alifika Sheikh Abdallah Darwesh alikuwa kafuatana na ndugu yake Sayyid Abdal Rahman Bin Sheikh na mama yake Sayyidat Mwana Mkuu wakaja katika jahazi moja. Sayyid alikutana na Sheikh Abdallah Darwesh alie mchukulia amana na pakapatikana baina yao mahaba kwa mtizamano wa mwanzo. Hayo yalitokea kwa hekima ya Mwenye Ezi Mungu aliyeumba akatengeneza kila jambo na vipawa vya kukusudiwa. Sheikh Abdallah alitelemka kwenye kisiwa cha Ngazija akaingia katika vingi katika vijiji vyake. Alipokuwa anazunguka katika vijiji hivyo aliona katika baadhi ya njia zake ndege wawili, mmoja akatoa ubait huu: شرتث شراب السر مه خمر الصفاء Wapili nae akatoa ubait huu: فسكرت لو حقا ومالي منا زعا Sheikh akaongeza juu ya ubait huu Abyat nyingine kama ilivyo katika kasida ijulikanayo Ubait wa mwanzo wa qasida hiyo ni: سقاء في سعاىاالحثية فلم ارى سواه علي اال طالقا فىاكون المع mpaka mwisho. Baadae Sheikh Abdallah alifanya makazi mahali alipozaliwa. Itsandaa mjini (Huko ndiko alipozaliwa mrithi wa Ahwal za Mawalii na Maqamat yao Seyyidna Al-Habib Omar Bin Ahmad Bin Sumeit رضوان هللا عايو na baba yake alizaliwa huko huko, babu yake Al-Habib Abubakar ndiye aliyetoka Shibam Hadhramaut kuja Ngazija- Mfasiri). Huko kwao Itsandaa Sheikh Abdallah alifungua chuo cha kusomesha watoto kur-an tukufu na baadhi ya vyuo vidogo vidogo. Baadhi ya watoto walikua wakikhitimu kuran takatifu kwa muda wa chini ya miezi sita kwa baraka zake hata wengi 4

katika watu wa Moroni waliwapeleka watoto wao ili awasomeshe vile vile alifungua Daira ya Dhikri huko aliwapa watu ijaza katika Tarika ya Shadhili Yashrutii khabari ilifika Moroni Bwana wangu (anakusudia Al Ma`aruf ) akakusudia Itsandaa kwa kutaka Ijaza akapewa Ijaza na Ukhalifa katika Tarika Shadhiliyya Yashrutyya. Sanad yake katika Tarika (NjiaTarika iliyomfikilia kutokana na Mtume (S.A.W) Alichukua Tarika kutokana na Abu Saith Arif Billah (amjuaye Mungu) Sheikh Abdallah Bin Said ajulikanae kwa jina la Darwesh yeye huyu akapokea kutokana na Ustadh mkamilifu kabisa Sayyid Ali Al-Yashruti (Bwana huyu alitoka Afrika ya kaskazini akaja Akka katika Flastin akafanya makazi Sheikh Abdalllah Darweshi katika mzunguko wake kumtafuta Khutbu Al Ghawth alifika huka Akka, akakaa chini na Sayyidina Ali Al-Yashruti kwa miaka hata akapata Al Fat-hu Al Akbar. Akapewa ruhusa arejee Ngazija kama wasita baina ya Sayyidina Ali na Sayyidina Al Ma`aruf, yeye Sheikh Abdallah Darwesh alipompa Al Ma`aruf amana yake alimwambia Hii kazi yenu nyinyi Ahl- Bait Rasulillah. Mfasiri). Yeye Sayyidina Ali Al-Yashruti alipokea kwa khutbu wa zama zake As Sayyid Muhammed Bin Hamza Dhafir Al-Madani kutokana na Sharif Al Husainy baba yake Ahmad Al Arab Addarqawi kutokana na Ali Al-Imran kutokana na Al Arab Bin Ahmad Bin Abdallah kutokana na baba yake Ahmad Bin Abdallah kutokana na Qassim Al Khassas kutokana na Abdul Rahman Al fasi kutokana na Muhammed Bin Abdallah Al Kabir baba yake Sayyidina Ahmad na wao wote wawili kutokana na Yusuf Al Fasi kutokana na Abdul Rahman Al Majdhub kutokana na Ali As-Sanhaji, kutokana na Ahmad Zarruq (Bwan huyu ni katika nguzo kubwa kabisa za Silsila hii alikusanya kila namna za elimu hata Falsafa, Mantiq (Logic) Sayansi na Mathematic. Kasema maneno makubwa makubwa kama alivyosema Sultan Al Awliyaa Seyyidina Abdul Qadir Jailan- Mfasiri) Zarruq alikuwa khalifa wa Ahmad Bin Uqba Al Hadhrami bwana huyu alilelewa Tarim Hadharamawt na Seyyidna Abdallah Bin Abubakar Al-Aidarus akafikilia daraja kuwa katika Uwalii Mwenyi Enzi Mungu akamchagua awe mmoja katika Mqutbu wa Silsila hii ya Shadhili akampeleka Misri akalazimiya na Yahya Al-Qadiri alipofariki huyo alirithiwa na Al Hadhrami Mfasiri). 5.

Yahya Al-Qadiria alipokea Ali Wafaa na yeye aliwapokea kutokana na baba yake Bahr Safa kutokana na Daud Al-Bakhili kutokana na Ahmad Bin Attaillah Assakandari kutokana Abi Al- Abbas Al Mursi (Huyu kaitwa Al Mursi kwa sababu alizaliwa Mercia, Spain wakati Spain ilikuwa ya kiislam baada ya waislamu kukaa huko kwa miaka wakatia misingi ya kila namna ya masomo na ustaarab huko ulaya. Al-Mursi alikuwa anakwenda kuhiji Jahazi ilivunjika wakazama watu wote akaokotwa hapo alipokuwa Qutba mkubwa kabisa Sayyidina Abdul Hassan Ash-Shadhili alimlazimu bwana huyu hata akawa yeye ndiye khalifa wake mkubwa kabisa - Mfasiri). Seyyidina Al-Imam Abdul Hassan alimrithi Abdu Ssalaam Bin Mashish na yeye alipokea kwa Abdulrahman Al Madani Azzayyat kutokana na Taqiyyuddin Al Fuqayyir kutokana na Al Qutb Fakhruddin kutokana na Qutb Nuruddin Abdul Hassan kutokana na Al Qutb Tajuddin kutokana Al Qutb Shamsuddin Assiwasi kutokana na Al Qutb Zainuddin Al Qazwimi kutokana na Al Qutb Abi Is-Haq Ibrahim Ali Bisry kutokana na Al Qutb Abu Qassim Ahmad Al Marwany kutokana na Qutb Abu Muhammed Said kutokana na Al Qutb Saad kutokana na Al Qutb Fathu Suud kutokana na Al Qutb Said Al Qazzani kutokana na Al Qutb Abi Muhammed Jabir kutokana na Qutb wa mwanzo Sayyiduna Al Hassan kutokana na baba yake Sayyidina Ali Bin Abi Twalib na yeye kapokea kwa Bwana wa mwanzo na wa mwisho Bwana wetu Muhammed S.A.W. Hapa Silsila imemalizika. Sheikh Abdallah alimwambia Al Maaruf "Chukueni kazi yenu hii nyinyi Ahl Bait Rasulillah. Sisi ni watumishi wenu katika kazi hii". Al Maaruf alipopewa ukhalifa alirejea Moroni akasimamisha Daira na akawa anawapa watu Ijaza wakakusanyika kwake watu namna nyingi Sheikh Abdallah alikuwa huja Moroni na kuhudhuria Daira pamoja naye hata bwana wangu (Siri yake imetakaswa alimchukua Sheikh Abdallah nyumbani kwake ili awape Ijaza watu wa huko nyumbani Sheikh Abdallah akampa ijaza mama yake Assayid na ndugu zake wanawake Sayyidat Alawiyyah, Sayyidat Batul, Sayyidat Fatuma na Sayyidat Ihsan ndugu zake baba mmoja mama mmoja aliendelea Sheikh Abdallah kwenda Moroni na kurudi Itsandaa. 6

Siku moja alipikiwa chakula Moroni, akasema: "Mwenye kula chakula hiki ataingia peponi, na mwenye kukila kwa nia yoyote atapata muradi wake". Akachukua kila mmoja katika walio kuwepo tonge tonge akawachukulia watu wa nyumbani. Palikuwa na mwanamke Tasa akala kwa nia Mwenyi Ezi Mungu ampe mtoto na Mungu akampa na hekaya hii inajulikana Ngazijah na imeenea kwenye watu wa huko. Baadaye alimpelekea Assayyid khabari asafiri aende Hinzwani Sayyid akamjibu kuwa, "hapana marikebu inayokwenda huko". Akamjibu "Andaeni safari kwani nyinyi mtasafiri kesho inshaallah". Wala hapakuwa merikebu pwani ilipokuja siku aliyowaambia kuwa safari yao itakuwa, alisikia mjini kuwa pamedhihiri jahazi ya matanga pwani lakini jahazi hiyo haikusogea mjini watu walitoka kuiangalia wakaikuta kama ilivyosemwa. Paliteremshwa Ngalawa kutoka Jahazini wakateremka baadhi ya waliokuwa na katika wao alikuwa mwenye Jahazi, Muhammed Bin Silim yeye alikua ana mke na marafiki Moroni ilipita kuwazuru tu. Assayyid alimuuliza mnaendea wapi? " akajibu Muwali" akasema "Sisi tunataka kusafiri pamoja na nyinyi" Jawabu ilikuwa kwa mapenzi na Ukarim akasafiri siku hiyo pamoja na Sheikh Abdallah Ali fundi na Ahmad Bin Nakhodha hata wakafika Muwali wakateremka baadae walisafiri kwenda Hinzwani katika Jahazi nyingineyo wakateremka Bamoni wakapita njia ya barabara hata wakifika Mtsamudu. Siku hiyo ilikuwa Ijumaa Mwezi 24 mfungo Tisa mwaka 1299 Hijriyya walipofika hapo alikutana na Ssayyid Ahmad Al-Kabir Muhammed Al Arab na Muhammed Abood na Abdu-Rab na wote wakawa katika Muridi wa Kishadhili. Baadaye Sayyid alijiweka kuwapa Ijaza kila alietaka wakachukua Ijaza kutokana naye watu namna nyingi, alikuwa husimamisha Daira msikiti wa Ijumaa kila usiku baada ya sala ya Isha. Watu wa msikitini walimwambia: "Ungeligura ukenda mahali pengine ingelikuwa bora kwani sisi tunashawishika ikisimamishwa Daira hapa na sisi tuna nyiradi hatuwezi kuzisoma". Kwa hiyo alihamia Masjid Ar-rhmani hakuwa akisimamisha Daira msikiti wa Ijumaa ila baada ya sala ya Ijumaa na sikukuu zote mbili. Baadae alielekea Wani ili kutoa Ijaza akakaa huko kiasi ya wiki walichukua Ijaza kwake aghlabu ya watu wa huko akampa Sheikh Muhammed Bin Abubakar Ukhalifa juu yao. 7

Alirejea tena Mtsamudu, lakini hakukaa hapo mda mrefu akatakiwa kwenda Bombo akaenda pamoja na baadhi ya Muridi, akakaa huko siku kadha wa kadha aliwapa Ijaza huko watu wengi akafanya khalifa juu yao Sayyid Jaafar baadae alirejea Mtsamudu akadumu katika Masjid Ar hmani katika kumtaja Rabbu wake. Hakuwa akienda msikiti wa Ijumaa ila siku ya Ijumaa. Kupingwa na Sheikh Fadhil na Jawabu ya Sayyid na yaliyopita baina yao kwa ufupi. (Mungu awalie Radhi wote wawili na atunufaishe kwa wote) katika muda huu Sheikh Fadhili alimpinga Sayyid katika kuwapa Ijaza ya Tarika watu wa Hunzuwani pamoja na kuwa wao si Ahli kama alivyodai yeye hali ya kutoa Dalili kwa hadithi "Msiwape hekima wasiostahiki msije mkadhulumu" na katika hadithi nyingine au utimilifu wa hii au hadith khutba na mimi ndie Mufti wa Sawahil yote tangu Ras hafun mpaka Ras torfi na mimi nimezuia dhikri juu yenu au kuisoma mbele yangu. Seyyid alisimama akasema "Huna njia ya kuzuia dhikri", wakati huo zogo lilizuka kwa wingi msikitini watu walisimama na kelele zikaja juu. Kila mmoja akakamata silaha yake, Sayyid nae alinyanyua upanga wake Sayyid Abdallah Bin Sheikh alitoa nje upanga wake Sayyid Abdallah Bin Omar Khajar lake akelekea kwa Sayyid Abdallah Bin Omar aliyeitwa Abood Bin Muhammad Bin Omar, mtoto wa nduguye Abdallah Bin Omar ni katika Muridi wa Sayyid. Hapo hapo alimpiga kofi Ami yake kwa sababu ya wivu juu ya Sheikh wake hivi ndo anavyokuwa Muridi. Sultan Abdallah alikuwapo msikitini askari wake wakamzunguka Sayyid akatoka nje ya msikiti akanadi anaetaka Ijaza na ahudhurie wakahudhuria mbele yake wengi na yeye pamoja waliokua pamoja naye wanataka jina la Mwenyi Ezi Mungu. Baadae alitoa sauti akatoa nje upanga wake mbele ya Sultan Abdallah. Askari walipoona upanga walikimbia, Sayyid alimshika Sultan mkono akamwambia: "Sema Allah" akawa anasema pamoja naye wakafuatana nyumbani na waliokuwapo waliwafuata na wote wanataja jina tukufu mpaka Sultan akaingia nyumbani kwake. Assayyid alielekea Mirontsi na kikundi katika Muridi wake walimfuata lakini hawakufika pamoja naye kwenye msikiti wa 8.

Mironts ila watu kumi katika hao ni nduguye Sayyid Ali. Hapakupita ila dakika chache mara ukawafikia mwito kutokana na askari wa Sultan Abdallah, waliokuwa wamemzunguka wakamwambia amnilikie Sultan, yeye akajibu " Ndivyo".Alipotoka Msikitini wale askari walitaka kuchukua upanga wake na yeye akajizuia. Nduguye Sayyid Ali akamwambia: "Hii ni amri ya Sultan anahitajia tuitii". Hapo akawapa upanga baadae alichukuliwa pamoja na aliokua nao kutoka Morots na huko wanapigwa na kutolewa maneno na msukumo mkubwa hata mwisho Sayyid alitupwa baharini akatupiwa mawe. Baharini palikuwa Jahazi ya baadhi ya wahindi Sayyid alipanda akabaki humo siku saba baadae akasafiri pamoja nao mpaka Nusbee. Ijumaa ya mwanzo baada ya vituko hivyo walikuja watu wake kutoka Bambao na katika hao ni Sayyid Jaafar na Sayyid Salim Bin Sultan Abdallah wakamkuta kesha safiri wakahudhuria Sala na wakasimamisha Daira. Waliapa kuwa ataewaingilia watamuuwa. Hapana aliewaingilia., Daira ilidumu kama ilivyokuwa katika Masjid Ar rahmani kila Ijumaa na sikukuu mbili ilikuwa ikisimamishwa Msikiti wa Ijumaa. Sayyid alirejea kutoka Nusbee akateremka Maote alimuamrisha Sayyid Ahmad Bin Abdulrahman na Abood Bin Muhammad warejee Hinzwan na yeye mwenyewe alielekea Ngazijah pamoja na nduguye Sayyid Ali na Muhammad Al arab. Alipofika Ngazijah alipokelewa na Sheikh Abdallah Darwesh na alikuwa pamoja nae kwa namna iliokuwa njema kabisa kuliko walivyopata kuwa. Baadae alimpeleka nduguye Hinzwani ili afanye upya mfungano wao na Tarika akampa Ijaza. Yeye alikaa Hinzwani miezi. Siku yane na ya tano ya kufika kwake Hinzwani alifariki Sheikh Fadhil ( Mungu amrehemu). (Sayyid alitoa amri asomewe wadhifa aombewe dua. Haya yanaonyesha kuwa Sheikh Fadhil hakumpinga Sayyid kwa inadi bali jitihada. Alijitahidi akakosana, na Sayyid akamuombea Dua aghufuriwe - Mfasiri) Sayyid Ali alirejea Ngazija akamkuta Sheikh Abdallah Darwesh kasafiri kwenda Zanzibar baada ya kufariki Sayyidat Alawiyya. Bibi huyo alikuwa na cheo kikubwa kwa Bwana ambae maisha yake yanaandikwa. Hapa mauti yalipomhudhuria alikuwa anataja jina tukufu la Mwenyi Ezi Mungu. Sayyid alimwambia: "Msalie Mtume" Bibi alijibu "Huyu hapa Mjumbe 9

wa Mwenyi Ezi Mungu ananiamrisha nitaje Ismul-Jalala". Sayyidat Alawiyya huyu ndiye ambaye Sheikh Abdallah Darwesh alisema katika kumtaja kumpa cheo chake: "Wangegawika Muridi mimi ningekuwa pamoja na kikundi alichomo Sayyidati Alawiyya". Katika siku hizo alikwenda Sayyid kwenye Bustani ya mama yake ijulikanayo kwa jina la Buzini akakaa huko siku nyingi awemo ndani ya Khalwa (Muepukano na kila kitu kwa kushughulika na Mwenyi Ezi Mungu) Hapo ilimjilia kwa daraja kubwa hali wapatao Mawalii wakubwa ilirejea nayo Mironi akaingia nyumbani kwa Sheikh Abdallah Bin Himid, akabaki pamoja naye huko siku tatu bila ya kuingia huko nyumba yoyote. Baada ya hapo alitoka Sheikh Abdallah Bin Himid na Sayyid akapanda juu ya sakafu ya nyumba akafika ukingoni akaanguka, nduguye Sayyid alimchukua mpaka nyumbani kwa mama yake akabaki nyumbani kiasi ya miezi sita na Ahwal zake zikizidi hatuwezi kukisia aliyoyapata katika yajayo kutoka na Mwenyi Ezi Mungu pamoja na yanayoteremka na miminio alipokuwa katika hali hiyo mara yumo ndani ya صحو mara nyingine محو pengine huwa عينةkatika na pengine katika (Maneno haya hayafasirika kwani ni Istilahi za Mabwana حضور Masufi. Hayana maana ya lugha wenyewe wanatambua kwa Dhawq. Kuyaonja na ekspiriense. - Mfasiri). Aliendelea hata akapata ambayo hatwezi kuyatambua vilivyo na tunahemewa na kudiriki hakika yake. Jadhba hii ni mash-hur Ngazija kwa Muridi wote. Yeye Sayyid alisema wakati katika Jadhba yake "Mimi ni kitu Azizi mimi ni kitu kilichotokana na Mtume (S.A.W) na ni hasha Mtume kumpa baba yangu kitu kidhalilifu". Alisema: (Mwenyi Ezi Mungu atunufaishe kwa baraka zake ) "Ingekuwa bahari ni wino na miti kalamu ili kudhibiti niliyoyaona bahari ingekwisha na miti ingemalizika kabla ya kumalizika mambo niliyoyaona katika Jadhba yangu hii". Baada ya hapo alirejea kukaa na watu kama ada yake ya mwanzo akasafiri kwenda Hinzwani akateremka Mtsamudu. Sultan Abdallah alikuwa Bambao alimtaka Sayyid aende huko na yeye akenda pamoja na baadhi ya Muridi. Sultan Abdallah akampokea kwa taadhima na mtukuzo, na yeye alikuwa akijihisabu kuwa ni katika jumla ya Muridu. Katika baadhi ya 10.

siku alimwonyesha mkono Sayyid kwa kutaka kumpa mapesa. Sayyid alisema: "Nimepokea zawadi yako, lakini sasa sina haja ya kitu basi kaa nayo mpaka wakati wa haja". Baadae alifika Sheikh Abdallah bin Himid kutoka Ngazija akakutana na Sayyid akampa khabari ya kifo cha Sayyidat Fatuma Bint Sheikh Ahmad. Ukhti yake Sayyid baba mmoja mama mmoja, alimuomba arejee Ngazija. akakubali akasafiri pamoja. Hii ndio safari ya mwisho ya Hinzwani hakurejea tena. Baada ya kufika Ngazija, watu wa huko walikhtalifiana na mfalme wao Sultan Sayyid Ali Bin Sultan Sayyid Omar Al-Masily walimtaka Sayyid awe pamoja nao na walimkhubiri kuwa watamuuzulu Sayyid Ali. Wakati huo ada ilikurubia kutoa kabisa hukumu za sheria iliyo tahirishwa jambo ambalo haridhii nalo Mwenyi Ezi Mungu na Mjumbe wake. Sayyid mara nyingi alikuwa akiyataja lakini hakumpata wa kunusuru sheria kwa hiyo alipotakiwa awe pamoja na alietaka kumuuzulu Sultan Sayyid Ali, waliomtaka walimpa miadi madhubuti kuwa watabatilisha ada yenye kwenda kinyume na sheria, watasimamisha sheria imara. Aliwakubalia na ikawa sababu kubwa ya kusalimika Sulatn Sayyid Ali nafsi yake kwani wale waliotaka kumuuzulu, walikusudia kumuua, lakini Sayyid hakuwaachia bali alibaki anawarairai na anawachukua kwa upole na kuwalainishia maneno kwa kumuonea huruma mtoto wa ndugu mama yake (Hakika ya mambo alihisi kuwa kisharia hakustahiki kuuliwa. Ingelikuwa sii hivyo angeliwaachia wakamuua kwani yeye ni wa mbele katika ambao hawatizami mhusiano mbele ya sheria ya Mungu - Mfasiri). Azma ya kumuuzulu iliposhika nguvu walimuamrisha khatibu asimtaje katika khutba ya Aljumua na yeye alukhutubu pasina kumuombea dua, ilipothibiti kwa Sultan Sayyid Ali kuwa waliloliazimia na jambo la matatizo alisafiri kwa kujificha mpaka Muali, na kutoka huko mpaka Maote akaifikishia dolla ya kifaransa yaliyomfika. Dola ya kifaransa iliandalia marikebo ikachukua idadi ya askari marekebo iliingia Ngazija ikateremsha 11.

askari ambao walitafuta baadhi ya watu wajulikanao wakawachukua baadhi yao. Walimtafuta As-Sayyid lakini yeye alijificha hawakuweza kutambua alipokuwa. Mitsamhuli ilikuwapo jahazi inakwenda Zanzibar, Sayyid alipanda usiku wakati ambao wanaomtafuta wameghafilika walipokuwa hawakumpatasayyid, nchi kavu wazungu walipanda kwenye jahazi ili watizame ikiwa hajajificha humo jahazini. Walipoingia jahazini wakaanza kupekua, palivuma upepo mkali na mawimbi yakachafuka, hapo hapo waliteremka bila ya kumuona, "Na wapi jicho pofu litaona jua?" wakati huo mnyororo uliofungiwa jahazi na nanga ulikatika na Jahazi ikaingia baharini matanga yakapandishwa na jahazi ikatweka kuelekea Zanzibar. Imewachukua Sayyid na Muridi wake wawili Ahmad Nakhodha na Abdul-R-rabb jahazi ilipokuwa mbali na nchi kavu Sayyid alisimama juu ya sitaha akababaika mmoja katika muridi wake akasema: "Eeh bwana wangu, umejitokeza watu watakuua iwe sababu ya sisi kuangamia", akajibu "Usihuzunike na sisi kwa kupenda Mwenyi Ezi Mungu baada ya salat aljumaa tutaingia Zanzibar. Safari yake ilikuwa jioni ya jumanne. Ikatokea vile vile kama alivyosema kwani waliingia Zanzibar baada ya salat aljumaa. Aliishi Sayyid Unguja hata mpaka alipotolewa Sultan Sayyid Ali Ngazija Dola ya kifaransa ndio iliyomtoa. Hapo alirejea Ngazija na hakusafiri kamwe. Hakuondoka huko hata Mwenyi Ezi Mungu akamchukua hali ya kuwa yeye Sayyid karidhia na karidhiwa. منا فيو رض هللا عنو 12.

Mtoto wa Al habbib Sayyeid Muhammed Al Ma`aruf aliyezaliwa Zanzibar. 13.

14

Al habbib Sayyeid Muhammed Bin Sayyeid Alliy Al Ma`aruf. 15.

16

Mfasiri kwa Kiswahili mtoto wa ndugu yake Sayyeid Al Ma`aruf. Al habbib Nassib Sayyeid Umar Bin Sayyeid Abdallah Mwinyibaraka. 17

Khalifa wa mwanzo wa Majaalis-el ulaa Mwinyi Baraka- Uwesia Qa-diriyya. Al Faqeer Sheikh Ahmad Bin Sheikh Muhammed Msiha. 18

Vitabu vilivyokwishatoka ni: *1. Maana halisi ya Imaan. (i) (1 st, 2nd & 3rd addition). *2. Njia nyepesi ya kuijua nafsi yako. *3. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya uongofu. *4. Knowledge vision & ecstacy. *5. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa kiislamu. *6. Waislamu na Sayansi - Ulu-m. *7. Kuhifadhi Burda. *8. Maana halisi ya Imaan (ii). *9. Muhammad SAW katika ulimwengu wa ghayb. *10. Siri ya Balaa. *11. El makhlouq (Viumbe) *12. Njia nyepesi ya kujua juu ya uongofu. (2nd addition) *13. Manaqib ya Al habbib Sayyeid Al Ma`aruf. Vitabu ambavyo tunategemea kuvitoa muda si mrefu (Insha Allah) ni: *1. Waislamu na Sayansi - Ulu-m. (2nd addition) *2. Njia nyepesi ya kuijua nafsi yako. (2nd addition). *3. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa kiislamu ( 2nd. add). *4. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya Uongofu. *5. Some aspects of concepts of facility in medevial Islamic Philosophy by Mwinyibaraka. Kwa maulizo kuhusu vitabu wasiliana nasi: Majaalis El Ulaa-MwinyiBaraka-Uwesia- El Qadiriyya Sinza, P.o. Box 15170, Tel: 0747483553 Tel: 0748595958. Tel: 0744 023703. Tel: 0741 235091. Tel: 0744 299597. Dar es salaam.