HAKIBulletin RAIS AMTEUA PROF. JUMA KUWA JAJI MKUU WA TANZANIA. Ndani: JARIDA LA MAHAKAMA YA TANZANIA

Similar documents
HAKIBulletin JAJI MKUU AWAASA WAHITIMU WA SHERIA KUJIENDELEZA KITAALUMA HALIUZWI! BENKI YA DUNIA USULUHISHI MUAFAKA MAHAKAMA MAWAKILI MAHAKAMA KUU,

HOTUBA YA JAJI MKUU MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA SIKU YA SHERIA, DAR ES SALAAM, TAREHE 1 FEBRUARI, 2018

BARAZA LA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA (Mawasiliano yawasilishwe kwa MSAJILI)

UWAJIBIKAJI NDANI YA JESHI LA POLISI

MOROGORO JARIDA LA. ISSN Toleo Na.4 Julai 2005 BODI ZA AFYA ZA WILAYA - SAUTI YA WANANCHI

Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya

John Lesson Eighteen Yohana Somo la Kumi na Nane

Ahadi za Serikali II. Zimekusanywa na HakiElimu Agosti 2007

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF BOMAS OF KENYA

TAARIFA YA HISTORIA YA MKOA WA MWANZA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA

AHMAD AL-RAYSUNI. SWAHILI VERSION idara ya Lugha na ukalimani ya Chuo Kikuu cha waislamu cha Morogoro. IIIT Mfululizo wa Vitabu kwa Muhtasari

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

Pre-Departure Program Swahili Unit 11 Worksheet UNIT 11: LOCATIVES, PREPOSITIONS, AND RELATIVE AND OBJECT INFIXES

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF

MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA KIRINYAGA YA KATI MWAKA WA 2013

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

TUMERITHI TUWARITHISHE

KITABU CHA MAFUNZO KWA WATOA DAWA KATIKA MADUKA YA DAWA MUHIMU

February 9, 2017 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 16 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY

Ripoti ya Warsha Ya Washikadau Ihusuyo Mpango wa Uendeshaji wa Mazingira Wilayani Rufiji Iliyofanyika Utete Rufiji Juni 2000

Imâm Al-Albâni, Katika Kumsifu Mwanafunzi Wake, Muheshimiwa Sheikh Ali Hasan 1

MALAIKA: WAJUMBE WA MUNGU

Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtukufu Mtume

HAKIKA YA AHMADIYYA. Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania

BARUA YA TATU KWA SHEIKH UBAYD AL-JÂBIRĪ [AULIZWA SHEIKH UBAYD] NA Sheikh Sālim at-twawîl (hafidhahullāh)

There is one God Mungu ni mmoja 1

Zanzibar itafutika-mwanasheria

DINI JE, DINI NI MUHIMU?

JINA KAMILI CHEO SIMU YA OFISINI Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwandishi Mwendesha Ofisi

Gazeti la kwanza la Kiislam kutolewa kwa lugha ya Kiswahili - mwaka 1936

Sura al-ahzaab. Tafsiri na Maelezo. Abdilahi Nassir

EVANGELISM FOR CHRIST UINJILISTI KWA AJILI YA KRISTO

Published on Al-Islam.org ( Home > Mahari ya Damu > Mahari ya Damu. Mahari ya Damu

Kuishi Maisha Tele. Katika mwanzo wa mwaka mpya, Niliwapa changamoto

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MANDERA CENTRAL CONSTITUENCY, HELD AT RHAMU

IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE.

Ukweli wa hadith ya karatasi

Ukweli Uliopotea - Sehemu Ya Tatu

ZABURI 91 mstari 1. KJV-lite VERSES

Tawasali. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags:

NEW LIFE IN CHRIST MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO

Khadija-tul-Kubra. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Published on Books on Islam and Muslims Al-Islam.org (

Bismillah ar-rahman ar-raheem SHAHADA 1 YALIYOMO

Ukoo Wake Na Kunasibika Kwake:

HALI YA UISLAMU. Maelezo ya kumsaidia Mkristo aufahamu Uislamu

NEW INTERNATIONAL VERSION

Rainbow of Promise Journal

Ujasiri wa Kimaadili. Mojawapo ya madhumuni ya maisha ya duniani

YA AL HABBIB SAYYEID

2002 Version of the Basic Talk on "Using African Proverbs, Sayings, Idioms, Riddles, Stories, Fables, Play

TAUS RETREAT NEWS LETTER # 1

Imam Mahdi katika Usunni Na Ushia

NGUO-NYINGI MKOTI: MWANZISHAJI WA MJI WA NGOJI (ANGOCHE)

NEW INTERNATIONAL VERSION

Toleo la kwanza: June, 2007 (Jamaadi Aakhar, 1428) Vitabu ii.

Kitabu Changu cha Mistari ya Biblia Swahili

Je, Umesikia Juu Ya Kanuni Nne Za Kiroho?

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS IJARA CONSTITUENCY AT IJARA BARAZA PARK

Uwezo Kenya National Learning Assessment 2014

WELCOME TO GOD S SERVICE A.C.K. ST. LUKE S PARISH UMOJA & TENA CHURCH QUOTE OF THE WEEK PRAYER OF THE DAY

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

2

TALKING ABOUT ONESELF TO ACT IN THE WORLD: A SWAHILI AUTOBIOGRAPHY (SHAABAN ROBERT, MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

Vitendawili Vya Swahili

NAIROBI CITY COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

VACATION BIBLE SCHOOL VBS. Newsletter. #Rebuilding through prayer, hard work & perseverance.

No. Book Name Category Type Price 1 AFYA MARIDHAWA -1 SWAHILI SUBSCRIPTION 2, AFYA NA UZIMA SWAHILI SUBSCRIPTION 8,500.00

Change Your Destiny CONFERENCE

MRADI WA METHALI (SANALASKUJA PROJEKTI)

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

REPUBLIC OF KENYA COUNTY ASSEMBLY OF KILIFI THE HANSARD. Wednesday, 29 th March, 2017

December 6, 2017 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 6 th December The House met at 9.30 a.m.

Preliminary Inventory to the William H. Friedland Collection, No online items

Yassarnal Quran English

6 10 November Welcome to Scripture Union s

JUNE 4, Acts 2:1-12 and Offering...Pastor Maromy Samuel All Hail the Power of Jesus Name led by Haitian Congregation Worship Team

In Search of Contact: Rhetorical Questions in the Communicative Frame of the Funeral Sermon

Ezra 3 Lessons Download or Read Online ebook ezra 3 lessons in PDF Format From The Best User Guide Database

WELCOME TO GOD S SERVICE ACK ST. LUKE`S PARISH UMOJA Theme: Endeavoring to touch the heart of God, (Matt 25:40). Kuazimia kumpendeza Mungu

Fifty Years of the Union: the Relevance of Religion in the Union and Zanzibar Statehood Debate

AND REACTION IN SWAHILI POETRY.

Junior Soldiers. The Global Salvation Army. Unit 6 : Lesson 4

Youth and Faith A collection of texts on the subject A collaborative Magazine Content

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

Cultural Considerations Tanzania Excursion

MAOMBI YA QUR'AN TUKUFU SHEIKH MUZAFFAR AHMAD DURRANI

Welcome to The Tuggeranong Salvation Army

ATONEMENT IN AFRICAN PLURALISTIC CONTEXT: EXAMPLES FROM THE LUHYA OF WESTERN KENYA

Mashairi ya Masaibu ya Karbala

CHRISTIAN-MUSLIM RELATIONS IN TANZANIA: A THREAT TO FUTURE STABILITY AND PEACE?

Modern Swahili: the integration of Arabic culture into Swahili literature

The Lutheran World Federation 2015 Membership Figures Summary

Christian-Muslim Relations in Tanzania: A Threat to Future Stability and Peace?

(Cell) (Cell) (Cell) (Landline) (Cell)

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MANDERA CENTRAL CONSTITUENCY, HELD AT ELWAK

MEMBERS WORLD COMMUNION OF REFORMED CHURCHES

2

Group Stamp. Group Stamp

The Growing of Islamic Fundamentalism in Tanzania: Are the rising religious tensions ripping Tanzania apart?

Transcription:

HAKIBulletin JARIDA LA MAHAKAMA YA TANZANIA ISSN: 00000054 Toleo Na. 1 Julai - Septemba, 2017 RAIS AMTEUA PROF. JUMA KUWA JAJI MKUU WA TANZANIA Ndani: MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA WAKUTANA TANZANIA KWA MARA YA KWANZA JAJI MKUU AZIPONGEZA MAHAKAMA ZA CHINI MAHAKAMA YAENDELEA KUJIZATITI KUBORESHA HUDUMA CHUKUENI HATUA KULINDA IMANI YA WANANCHI MLUNDIKANO WA KESI MAHAKAMANI SASA BASI MAHAKAMA YAIMARISHA HAKI ZA WATOTO KWA VITENDO KITUO JUMUISHI CHA UTOAJI HAKI CHAZINDULIWA MBEYA www.judiciary.go.tz

1. FEBRUARY 5 TH - 16 TH MARCH 2018 IN THE COURT OF APPEAL OF TANZANIA AT DAR ES SALAAM COURT CALENDAR FOR THE YEAR 2018 DAR ES SALAAM APPEALS AT DAR ES SALAAM FEBRUARY 5 TH - 23 RD FEBRUARY 2018 MBEYA APPEALS AT MBEYA TABORA APPEALS AT TABORA DAR ES SALAAM APPEALS AT DAR ES SALAAM FEBRUARY 26 TH - 16 TH MARCH ARUSHA APPEALS AT ARUSHA DODOMA APPEALS AT DODOMA 2. MARCH 24 TH - 2 ND APRIL 2018 EASTER VACATION APRIL 9 TH - 4 TH MAY 2018 APRIL 9 TH - 20 TH APRIL 2018 DAR ES SALAAM APPEALS AT DAR ES SALAAM TANGA APPEALS AT TANGA MWANZA APPEALS AT MWANZA APRIL 23 RD - 4 TH MAY 2018 DAR ES SALAAM APPEALS AT DAR ES SALAAM IRINGA APPEALS AT IRINGA MTWARA APPEALS AT MTWARA 3. MAY 21 ST - 1 ST JUNE 2018 MAY 21 ST - 1 ST JUNE 2018 DAR ES SALAAM APPEALS AT DAR ES SALAAM IRINGA APPEALS AT IRINGA 4. JUNE 18 TH - 13 TH JULY 2018 JUNE 18 TH - 13 TH JULY 2018 MWANZA APPEALS AT MWANZA ARUSHA APPEALS AT ARUSHA DODOMA APPEALS AT DODOMA TABORA APPEALS AT TABORA 5. AUGUST 13 TH - 31 ST AUGUST 2018 AUGUST 13 TH - 31 ST AUGUST 2018 DAR ES SALAAM APPEALS AT DAR ES SALAAM BUKOBA APPEALS AT BUKOBA TABORA APPEALS AT TABORA 6. SEPTEMBER 17 TH - 6 TH OCTOBER 2018 SEPTEMBER 17 TH - 6 TH OCTOBER 2018 DAR ES SALAAM APPEALS AT DAR ES SALAAM ARUSHA APPEALS AT ARUSHA MWANZA APPEALS AT MWANZA 7. OCTOBER 22 ND - 2 ND NOVEMBER 2018 OCTOBER 22 ND - 2 ND NOVEMBER 2018 DAR ES SALAAM APPEALS AT DAR ES SALAAM TANGA APPEALS AT TANGA 8. NOVEMBER 19 TH - 14 TH DECEMBER 2018 NOVEMBER 19 TH - 14 TH DECEMBER 2018 ZANZIBAR APPEALS AT ZANZIBAR ARUSHA APPEALS AT ARUSHA MWANZA APPEALS AT MWANZA MBEYA APPEALS AT MBEYA 15 TH DECEMBER, 2018-31 ST JANUARY, 2019 - X-MAS & NEW YEAR VACATION AT DARES SALAAM 26 TH SEPTEMBER, 2017... J.R. KAHYOZA REGISTRAR COURT OF APPEAL i HAKIBulletin Julai - Septemba 2017

iv NENO TOKA KWA MHE. JAJI MKUU 01 YALIYOMO RAIS AMTEUA PROF. JUMA KUWA JAJI MKUU WA TANZANIA 09 10 CHUKUENI HATUA KULINDA IMANI YA WANANCHI MLUNDIKANO WA KESI MAHAKAMANI SASA BASI 03 05 MAJAJI NA MAHAKIMU WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA WAKUTANA TANZANIA KWA MARA YA KWANZA JAJI MKUU AZIPONGEZA MAHAKAMA ZA CHINI 13 MAHAKAMA YAIMARISHA HAKI ZA WATOTO KWA VITENDO 07 MAHAKAMA YAENDELEA KUJIZATITI KUBORESHA HUDUMA 16 KITUO JUMUISHI CHA UTOAJI 18 HAKI CHAZINDULIWA MBEYA HABARI KATIKA PICHA Bodi ya Wahariri Mwenyekiti: Bw. Nurdin Ndimbe Katibu: Bi. Mary Gwera Wajumbe: Mhe. Amir Msumi Mhe. Warsha Ng humbu Mhe. Mustapher Siyani Mhe. Beda Nyaki Bw. Samson Mashalla Bi. Lydia Churi Walengwa: Watumishi wa Mahakama, Wadau na Wananchi kwa ujumla. Sera ya Uhariri: Madhumuni ya Jarida hili ni kuhabarisha na kuelimisha Watumishi wa Mahakama ya Tanzania juu ya masuala mbalimbali. Jarida hili hutolewa na: Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Mahakama ya Tanzania, 26 Kivukoni Avenue/Ohio, S.L.P. 9004, Dar es Salaam Tanzania. Simu: +255 22 2124187, Nukushi: +255 22 2116 654 Barua-pepe: info@judiciary.go.tz, Blogu: tanzaniajudiciary.blogspot.com, Tovuti: www.@judiciary.go.tz HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 ii

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA TANGAZO YAH: MAONI YA WANANCHI JUU YA MABORESHO YA UTOAJI HUDUMA WA MAHAKAMA YA TANZANIA 1. MAHAKAMA YA TANZANIA NI MIONGONI MWA TAASISI INAYOLALAMIKIWA NA WANANCHI HUSUSANI JUU YA UTARATIBU MZIMA WA UTOAJI HUDUMA ZAKE. 2. MAHAKAMA INAKUSANYA MAONI YA WANANCHI, MASHIRIKA YA SERIKALI NA YASIYO YA KISERIKALI, WADAU, MAKAMPUNI NA WATUMIAJI WENGINE WA HUDUMA ZA MAHAKAMA. 3. ILI KUFANIKISHA AZMA TAJWA HAPO JUU NA KUFUATIA MALALAMIKO HAYO, MAHAKAMA YA TANZANIA IMEKUWA KATIKA MABORESHO MBALIMBALI YA UTENDAJI KAZI LENGO LIKIWA NI KUBADILI TASWIRA YA MAHAKAMA KWA KUBORESHA HUDUMA ZAKE. 4. MABORESHO HAYO YANALENGA KATIKA KUIMARISHA HUDUMA YA UTOAJI HAKI NCHINI IKIWA NDIO KAZI KUU YA MHIMILI HUU MUHIMU. KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZAKE MAHAKAMA INAHITAJI USHIRIKIANO PAMOJA NA WADAU WAKE IKIWA NI PAMOJA NA WANANCHI AMBAO NDIO WATEJA WAKE WAKUU. 5. KWA MANTIKI HII, TUNATOA FURSA KWA WOTE NA KWA YEYOTE KUELEZA MAENEO MUHIMU AMBAYO YANAHITAJI KUBORESHWA ILI KULETA UFANISI KATIKA UTENDAJI KAZI WA MAHAKAMA. AIDHA, MAONI YANAWEZA KUTUMWA KWA UJUMBE MFUPI (SMS) KUPITIA NAMBA YA SIMU +255 784 821 170 AU KWA BARUA PEPE: info@judiciary.go.tz IMETOLEWA NA: MTENDAJI MKUU, MAHAKAMA YA TANZANIA iii HAKIBulletin Julai - Septemba 2017

Neno Toka kwa MHE. JAJI MKUU Jarida hili limeanzishwa rasmi na Mahakama kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi juu ya masuala mbalimbali ya msingi kuhusu utoaji na upatikanaji wa haki, pamoja na kutangaza huduma mbali mbali zinazotolewa na Mahakama. Kwa toleo hili, Jarida litazungumzia zaidi namna Mahakama ya Tanzania inavyojipanga kimkakati kupeleka huduma bora za utoaji haki na kuzifikisha karibu zaidi na wananchi kwa haraka zaidi. Pamoja na ukweli kwamba Mihimili mingine ya Dola ina wajibu mkubwa wa kuiwezesha Mahakama kwa rasilimali watu, fedha na miundombinu, Mahakama yenyewe ina jukumu zito zaidi la kuhakikisha huduma za Mahakama zinawafikia wananchi kule walipo. Wakati alipozindua Mpango Mkakati wa Mahakama wa Miaka Mitano (2015/2016 2019/2020 mwezi Septemba 2016, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa alisisitiza umuhimu wa Mahakama kuwa na Mkakati wake alipotamka kuwa Mpango huo utasaidia uboreshaji wa huduma zinazotolewa na Mahakama katika ngazi zote nchini na kuzisogeza karibu na wananchi. Hii si tu kwamba ni muhimu kwa Mahakama, bali pia ni kwa faida kubwa kwa Serikali na Watanzania wote kwa ujumla. Utayarishwaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama ulikuwa shirikishi, na ulizingatia MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU 17 (SDGs). Huduma za utoaji haki ni sehemu muhimu ya MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU NA. 16: vkuendeleza Jamii Jumuishi na yenye Amani kwa ajili ya Maendeleo endelevu, kutoa haki kwa wote na kujenga taasisi imara zenye kuwajibika katika nyanja zote. Ninayo heshima kubwa kuwasilisha Mpango huu wa kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia 2015/2016-2019/2020; na pia kutambua juhudi kubwa za uongozi na watumishi wote wa Mahakama, wakiongozwa na Mtendaji Mkuu na Msajili Mkuu wa Mahakama katika maandalizi ya Mpango huu. Ninaamini kabisa Jarida la Mahakama litakuwa kiunganishi muhimu katika kutoa habari kwa wananchi na wadau wetu. Tunaweza kutumia jarida hili kupata mrejesho toka kwa wananchi na wadau wetu juu ya huduma zinazotolewa na Mahakama ya Tanzania. Naamini kuwa mabadiliko na Maboresho yanayofanyika katika mhimili huu wa Mahakama utaleta mabadiliko chanya na kuchangia katika ukuaji wa Tanzania ya viwanda. Kwa ujumla, lengo kuu la Mahakama kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ni kuhakikisha kuwa azma ya utoaji huduma inayomlenga mwananchi inafanikiwa. Kufikiwa kwa azma hii kutahitaji mabadiliko ya kifikra, maadili, malengo ya kazi na uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa Mahakama. Ni matumaini yangu kwamba watumishi wote wa Mahakama na wadau watashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mpango na hatimaye kufikia malengo tuliyojiwekea. Prof. Ibrahim Hamis Juma Jaji Mkuu HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 iv

RAIS AMTEUA PROF. JUMA KUWA JAJI MKUU WA TANZANIA Na Lydia Churi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zana za kazi Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma mara baada ya kumwapisha kushika wadhifa huo Septemba 11, 2017, Ikulu jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kufanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya Watanzania na kupambana na vitendo vya Rushwa. Akizungumza wakati wa kumuapisha Jaji Mkuu wa sita Mzalendo kwenye sherehe zilizofanyika, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amemtaka kiongozi huyo kufanya kazi kwa bidii licha ya changamoto zinazoikabili Mahakama ya Tanzania na kuwa Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na Mhimili huo. Mungu amekuchagua, katumikie watanzania kwa kuongozwa na maslahi yao, alisema Rais Magufuli na kuongeza kuwa tatizo la rushwa ni kubwa na liko karibu katika kila Taasisi ya Serikali hivyo alimtaka kiongozi huyo kupambana nalo. Akizungumzia kuhusu uteuzi wa Jaji Prof. Juma, Rais alisema pamoja na kuwepo kwa Majaji wengi ambao ni watendaji wazuri, aliamua kumteua Prof. Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kwa kuwa dhamira yake imemkubali kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kupambana na vitendo vya Rushwa. Akizungumza baada ya kuapishwa kushika wadhifa wa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema hakuna mgongano baina ya mihimili yote mitatu ya dola kwa kuwa yote inafanya kazi ya kuboresha maslahi ya wananchi wa Tanzania na kuwa Katiba ya nchi inalazimisha ushirikiano baina ya mihimili yote. Jaji Mkuu alisema, Mahakama imejiwekea utaratibu wa kuondoa uwezekano wa kutokea kwa migongano baina ya mihimili kwa kuzipa kipaumbele kesi zinazohusiana na kazi zinazofanywa na Serikali kama vile ujenzi wa reli au barabara, migogoro ya wakulima na kesi mbalimbali za uhujumu uchumi. Aidha, Prof. Juma alimshukuru Rais kwa kumteua kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania na kuahidi kutimiza wajibu wake kikamilifu kwa kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati kwa kuwa hiyo ndiyo kazi kubwa ya Mahakama ya Tanzania. Kuhusu Mpango Mkakati wa Miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/16-2019/20), Jaji Mkuu alisema Mahakama ya Tanzania inatekeleza wajibu wake kwa kuzingatia nguzo tatu za Mpango huo ambazo ni Utawala Bora na Usimamizi wa Rasilimali, Upatikanaji wa Haki kwa Wakati na Urejeshaji wa Imani ya Wananchi kwa Mahakama. Alizitaja baadhi ya changamoto ndani ya Mahakama alizokabiliana nazo akiwa Mhe. Jaji Mkuu na pia atakazokabiliana nazo kama 1 HAKIBulletin Julai - Septemba 2017

Jaji Mkuu kuwa ni upungufu wa majengo ya Mahakama hasa Mahakama za Mwanzo nchini. Alisema Tanzania ina kata zaidi ya 3000 ambapo kati ya hizo, ni kata 976 pekee ndizo zenye Mahakama za Mwanzo. Ili kutatua changamoto ya upungufu wa majengo ya Mahakama, kufikia mwaka 2020 jumla ya majengo 100 ya Mahakama za Mwanzo, 48 Mahakama za Wilaya, 14 Mahakama za Hakimu Mkazi, 13 Mahakama Kuu na moja la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania yatajengwa. Wakati huo huo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Jaji Mkuu katika majukumu yake ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata haki kwa wakati. Waziri huyo wa Katiba na Sheria pia alimpongeza Rais Magufuli kwa kumteua Prof. Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania kwa kuwa ni mchapa kazi, mtii na muadilifu. Kabla ya uteuzi huo, Prof. Juma alikuwa Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania toka Januari 18, 2017 na kuteuliwa rasmi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Septemba 10, 2017. Majaji wengine waliowahi kushika wadhifa wa Jaji Mkuu wa Tanzania ni Raphs Windham (1961-1964), P. Telford Georges (1965-1970), Augustino Said- Jaji wa kwanza Mzalendo (1971-1977), Francis Lucas Nyalali (1977-2000), Barnabas Albert Samatta (2000-2007), Augustino Ramadhani (2007-2011), Mohamed Chande Othman (2011-2017) na Prof. Ibrahim Hamis Juma wa sasa. Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiapa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Septemba 11, 2017, Ikulu jijini Dar es salaam HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 2

Majaji na Mahakimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Wakutana Tanzania kwa Mara ya Kwanza Rushwa yatajwa kuwa kikwazo cha Upatikanaji wa Haki Na Lydia Churi na Magreth Kinabo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameziasa Mahakama za nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kupambana na rushwa ili kuzifanya Mahakama hizo kuwa huru zinapotekeleza jukumu lake la msingi la utoaji haki. Akifungua mkutano wa mwaka wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa nchi za Jumuiya ya Madola kilichofanyika kwa mara ya kwanza nchini kuanzia Septemba 25 hadi 27 mwaka huu, Makamu wa Rais alisema kuwepo kwa vitendo vya rushwa ndani ya Mahakama husababisha Mahakama kutokuwa huru na kukosekana kwa utawala wa sheria. Alisema nchi hizo zinapaswa kuwa na Mahakama huru na zinazowajibika ili kujenga msingi wa Demokrasia. Akizungumzia Tanzania, Mhe. Makamu wa Rais alisema Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha Mahakama ya Tanzania inapambana na vitendo vya rushwa ili kuimarisha uhuru wake. Naamini kuwa nia ya kujenga Mahakama bora na yenye kuwajibika kwa Tanzania haiwezi kutenganishwa na juhudi za Serikali Katika kupambana na kuondoa umaskini na rushwa, alisema Makamu wa Rais. Makamu wa Rais alisema amefurahishwa kuona Majaji na Mahakimu wa Jumuiya ya Madola wanakutana ili kujadili masuala mbalimbali yatakayosaidia nchi zao kuendana na kauli mbiu ya Mkutano huo inayotaka kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji. Naye Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza kwenye Mkutano huo alisema njia pekee ya kuifanya Mahakama kuwa shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji ni kupitia utekelezaji wa Mpango Mkakati. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa mwaka wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) uliofanyika Septemba 25-27, 2017 jijini Dar es Salaam. Ni mwaka wa pili sasa tangu Mahakama ya Tanzania ianze kutekeleza Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (2015/2016-2019/2020) ambao msingi wake ni kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama na kuhakikisha upatikanaji na utoaji wa haki kwa wote unapatikana wakati. Nina uhakika kuwa mkutano huu muhimu utatusaidia kubadilishana uzoefu juu ya umuhimu wa Mpango Mkakati katika kusaidia Mahakama zetu za Jumuiya ya Madola ili ziwe thabiti, zinazowajibika na shirikishi alisema Jaji Mkuu wa Tanzania. Alisema kuwa Mahakama ya Tanzania kupitia Sheria ya Usimamizi wa Shughuli za Mahakama namba 4 ya mwaka 2011 iliwaondolea Majaji na Mahakimu majukumu ya kiutawala na majukumu hayo kuanza kufanywa na Watendaji wa Mahakama. Mabadiliko hayo yamesaidia kuifanya Mahakama kuwa inayowajibika zaidi katika kutoa haki kwa wakati. Prof. Juma alisema kupitia Mpango Mkakati wa miaka mitano, Mahakama ya Tanzania, inakusudia kusogeza huduma kwa wananchi kwa kuongeza idadi ya Majengo. Kufikia mwaka 2020 jumla ya majengo 100 ya Mahakama za Mwanzo, 48 Mahakama za wilaya, 14 Mahakama za Hakimu 3 HAKIBulletin Julai - Septemba 2017

Mkazi, 13 Mahakama kuu na moja la makao makuu ya Mahakama ya Tanzania yatajengwa. Wakati huo huo, Majaji na Mahakimu wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola wameshauriwa kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao yakiwemo masuala ya mlundikano wa kesi Mahakamani, maadili na matumizi sahihi ya rasilimali. Akifunga mkutano huo kwa niaba ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi-Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman alisema nchi za Afrika hazina budi kuungana ili kukabiliana na changamoto nyingine za vitendo vya kigaidi, biashara ya usafirishaji wa binadamu na dawa za kulevya, Aidha Waziri huyo, alisema, Majaji na Mahakimu wanatakiwa kufuata maadili ya taaluma zao na kuzingatia taratibu na sheria ili kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama. Aliongeza kuwa ili kukabiliana na tatizo la ucheleweshaji wa kesi, watumishi wa Mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu hawana budi kuwajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao. Kwa mujibu wa Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), Mhe. Jaji Ignas Kitusi, Wajumbe wa mkutano huo walikubaliana kuwa Majaji na Mahakimu wa nchi za Jumuiya ya Madola waendelee kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na miiko ya kanuni zao za utendaji kazi ili kutekeleza jukumu la msingi la utoaji haki kwa wananchi. Katika Mkutano huu, tumejadiliana masuala mbalimbali jinsi ya kusikiliza kesi kwa namna moja, pamoja na hilo pia tumekubaliana kuendelea kutekeleza jukumu la utoaji haki kwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi yetu, alisema Mhe. Kitusi. Jumla ya washiriki 354 ambao ni Mahakimu na Majaji kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Madola walihudhuria Mkutano huo. Nchi hizo ni Uingereza, Australia, Kanada, Uganda, Kenya, Scotland, Ushelisheli, New Jersey, Guyana na Ghana. Nchi nyingine ni Trinidad&Tobago, Nigeria, Afrika ya Kusini, na Tanzania. Nchi nyingine ni Cayman Islands, Marekani, Gambia, Bermuda, Papua New Guinea, Lesotho, Malawi, Bahamas, Malaysia, Wales, Turks & Caicos, Sri Lanka, Singapore, New Zealand, India, Rwanda, Burundi, Sudani ya Kusini na Cameroon. Nyingine ni Botswana, Zanzibar, Zambia, Mauritius, Brazil, Msumbiji, Swaziland, na Namibia. Aidha, Mkutano huo umekuwa ni wa kihistoria kufanyika hapa nchini kwa kuwa Tanzania imekuwa mwenyeji kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Umoja huo mwaka 1970. Katika bara la Afrika mkutano huu umefanyika kwa mara ya pili. Mkutano ujao unatarajiwa kufanyika mwakani nchini Australia. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa mwaka wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) uliofanyika Septemba 25-27, 2017 jijini Dar es Salaam. HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 4

JAJI MKUU AZIPONGEZA MAHAKAMA ZA CHINI Na Mary Gwera, Manyara Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amezipongeza Mahakama za Mwanzo na zile za Wilaya kutokana na kasi ya uondoshaji wa Mashauri inayofanywa na Mahakama hizo za ngazi ya chini nchini. Akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Manyara Mei 8, 2017, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma aliwapongeza Mahakimu wote nchini kwa kazi nzuri wanayoifanya hasa baada ya kuongeza kasi katika kuondosha mashauri katika Mahakama za ngazi za chini licha ya idadi kuonekana kuwa kubwa. Aidha, hadi kufikia Desemba mwaka 2016, mlundikano wa mashauri kwenye Mahakama mbalimbali nchini ulishuka kutoka wastani wa asilimia 46 mwaka 2013 na kufikia wastani wa asilimia 21 kwenye mahakama ya Rufani na kutoka wastani wa asilimia 33 mwaka 2013 na kufikia wastani wa asilimia 9 kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania. Katika Mahakama za Hakimu Mkazi/Mkoa, idadi ya mlundikano wa mashauri ya zamani ilipungua na kufikia wastani wa asilimia 3 kutoka wastani wa asilimia 9 mwaka 2013. Mlundikano wa mashauri kwenye Mahakama za Wilaya ulishuka kutoka wastani wa asilimia 9 mwaka 2013 na kufikia wastani wa asilimia 3 mwaka 2016 wakati kwenye Mahakama za Mwanzo mlundikano ulishuka kutoka wastani wa asilimia 2 mwaka 2013 hadi kufikia kesi sifuri (0) au kutokuwa na mashauri hayo kabisa hivi sasa. Mahakama ya Tanzania haina budi kujivunia mafanikio haya makubwa hasa kwa Mahakama za chini ambako asilimia 80 ya kesi zinazofunguliwa na wananchi zipo kwenye ngazi hizo. Mahakama pia imefanikiwa kupunguza mlundikano wa mashauri yenye zaidi ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma na Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Theresia Mahongo wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo, Karatu. Uwekaji wa jiwe hilo la msingi uliohudhuriwa na Watumishi wa Mahakama, Wananchi, Viongozi wa dini, Maafisa kutoka serikalini n.k, anayeshuhudia wa kwanza kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi. Ujenzi wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo Karatu mjini ulianza Novemba Mwaka 2012 kwa nguvu za wananchi kwa kuhamasishwa na Mkuu wa Wilaya pamoja na Hakimu wa Wilaya Mfawidhi. Aidha, thamani ya mradi huo wa umaliziaji wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Karatu Mjini ni kiasi cha Shilingi Milioni 137,275,540/ 5 HAKIBulletin Julai - Septemba 2017

miaka miwili kutoka mashauri 10,832 yaani sawa na asilimia 10 mwaka 2012 hadi kufikia mashauri 2,702 sawa na asilimia (5%) tano mwaka 2016. Akizungumza na Watumishi wa Mahakama Mkoani Manyara, Mhe. Jaji Prof. Juma alisema kuwa wananchi wengi bado wana Imani na Mahakama yao, na hili linajidhihirisha kwa kuwa idadi kubwa ya mashauri imeendelea kufunguliwa katika Mahakama zetu hususani Mahakama za Chini ambazo ni Mahakama za Mwanzo na Mahakama za Wilaya. Kwa takwimu tulizo nazo Mahakama kwa mwaka jana, asilimia 71 ya mashauri yalifunguliwa katika Mahakama za Mwanzo, huku Mahakama za Wilaya zikiwa na asilimia 14 ya kesi zilizofunguliwa kwa mwaka jana, Mahakama za Hakimu Mkazi asilimia 7, Mahakama Kuu asilimia 5 na Mahakama ya Rufani ikiwa na wastani ya asilimia 0.5, alieleza Mhe. Jaji Mkuu. Aliendelea kusema kuwa takwimu hizo zinaonesha dhahiri kuwa wananchi bado wana imani kubwa na Mahakama zetu na hivyo kuwataka Mahakimu na watumishi wengine wote wa Mahakama kwa ujumla kuongeza bidii katika kuwatumikia wananchi. Mbali na pongezi hizo, Mhe. Mhe. Jaji Mkuu aliwataka Watumishi wa Mahakama-Manyara kufanya kazi kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Mahakama ambao ndio dira itakayowawezesha kufikia azma ya kuwa Mahakama bora yenye kutoa huduma bora kwa wananchi. Wengi wenu mnafahamu kwa sasa, Mahakama ipo katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wake wa miaka mitano, wenye lengo la kuboresha maeneo mbalimbali Mahakamani ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma ya utoaji haki nchini pamoja na kurejesha imani ya wananchi kwa chombo hiki, aliwaambia watumishi hao akiwataka kila mmoja kushiriki kikamilifu katika utekelezaji huo. Aidha, Mhe. Jaji Mkuu aliwataka pia watumishi wa Mahakama kujikita katika Matumizi ya TEHAMA ili kurahisisha utendaji kazi huku akitilia mkazo kwa Watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi. Awali akisoma hotuba yake mbele ya Mhe. Jaji Mkuu, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara, Mhe. Devotha Kamuzora alisema kuwa Mahakama katika mkoa huo zimekuwa zikifanya kazi ya uondoshaji mashauri kwa jitihada ili kuhakikisha kuwa inaondokana na mlundikano wa mashauri. Mhe. Jaji Mkuu, kwa upande wetu, Mahakama Mkoa wa Manyara tumejiwekea mkakati wa kuhakikisha kuwa kesi yoyote inayoletwa katika Mahakama ya Mwanzo/Wilaya isizidi miezi mitatu mpaka kukamilishwa kwake, na hili tunalisimamia kuhakikisha tunaondokana na mlundikano wa mashauri katika Mahakama zetu, alisema Mhe. Kamuzora. Ziara ya Mhe. Jaji Mkuu ililenga katika kuangalia utendaji kazi wa Mahakama hizo, mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo na hatimaye kushughulikia changamoto hizo kwa ustawi wa Mahakama. Katika ziara yake, Mhe. Jaji Mkuu alitembelea Mahakama kadhaa mkoani humo ikiwa ni pamoja na Mahakama ya Wilaya Babati, Mahakama ya Mwanzo/Wilaya Hanang, pia kukagua Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara na baadaye alifanya ziara katika Mkoa wa Arusha. HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 6

MAHAKAMA YAENDELEA KUJIZATITI KUBORESHA HUDUMA Na Lydia Churi Mahakama ya Tanzania imepanga kutoa huduma bora ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao za msingi kwa wakati. Lengo hili linatekelezwa kupitia Mpango Mkakati wa miaka mitano (5) wa Mahakama wake wa miaka mitano unaotekelezwa katika kipindi cha 2015/16-2019/20. Mpango Mkakati huu ni dira na mwelekeo wa Mahakama katika kufikia lengo lake la kuwa Mahakama iliyo karibu na inayofikiwa na wananchi katika kutoa huduma bora za utoaji wa haki. Aidha, Mpango Mkakati huu unalenga kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2025 ya kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati. Mpango huu umejikita katika nguzo tatu ambazo ni Utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, Upatikanaji wa Haki kwa wakati pamoja na uimarishaji wa Imani ya wananchi kwa Mahakama pamoja na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za Mahakama. Katika nguzo ya kwanza ya Mpango Mkakati huu, Mahakama imeanzisha vikao maalum vya kutathmini kazi ya uendeshaji wa mashauri na kazi za Mahakama kwa ngazi za Mahakama ya Rufani, Majaji Wafawidhi wa Kanda za Mahakama Kuu pamoja na kamati tano za kumshauri Jaji Mkuu za Kanuni, Mafunzo, Takwimu, Tehama, Ufuatiliaji na Maboresho. Aidha Mahakama pia inasimamia suala zima la utendaji kazi kwa malengo kwa kada zote ndani ya Mhimili huo. Matumizi ya TEHAMA ndani ya Mahakama Akiwasilisha Taarifa ya utendaji kazi wa Mahakama ya Tanzania kwa Waziri wa Katiba na Sheria hivi karibuni, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga alisema Mahakama imeanza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kurahisisha utendaji kazi wake pamoja na kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Mahakama tayari imeanzisha mfumo wa ukusanyaji wa takwimu za mashauri kwa njia ya kielekitroniki kuanzia ngazi ya Mahakama za Wilaya, Mkoa, Kanda na Taifa. Mbali na mfumo huu, hadi kufikia mwisho wa mwaka huu wa fedha 2017/2018, Mahakama itakuwa imeanza kutumia Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (katikati) akimkabidhi Mkataba wa kazi, Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Mwangu, Mikataba hii ya kazi ilisainiwa na Wakuu wote wa Idara ndani ya Mahakama, lengo likiwa kufanya kazi kwa wakati kulingana na Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania. Aliyesimama kushoto ni Msajili wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. John Kahyoza 7 HAKIBulletin Julai - Septemba 2017

mitandao kwenye usajili wa kesi. Aidha, Mahakama iko kwenye mpango wa kuweka kwenye mtandao na kuingiza mkongo wa taifa kwa Mahakama zote za wilaya, Hakimu Mkazi/Mkoa, na Mahakama Kuu. Tayari majengo ya Mahakama Kuu Mbeya na la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha yameshawekewa. Ili kutekeleza nguzo ya pili ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania, taratibu, kanuni na sheria zinazokwamisha na kuchelewesha kesi mahakamani na zile zilizopo nje ya Mahakama zinapitiwa upya, na mamlaka husika kushauri ipasavyo. Mpango huu utasaidia kupunguza hatua za usikilizaji wa kesi za madai kutoka 68 na kufikia mpaka 21. Aidha, Mtendaji Mkuu alisema Mahakama pia imeandaa Mpango maalum na endelelevu katika ngazi zote za Mahakama kwa lengo la kuondosha mashauri ya zamani na kuzuia mashauri mapya kupevuka. Mpango huo pia utapelekea uimarishaji wa menejimenti ya mashauri kwa kuyabaini mashauri yote mapya na kisha kushirikisha wadau kupitia vikao mbalimbali. Mahakama pia itaimarisha upatikanaji wa nakala za hukumu na mienendo ya kesi zikiwemo njia za kupeleka kwa wateja kwa njia ya posta na njia nyingine za kielektroniki. Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Miundombinu ya Mahakama Katika kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi, Mtendaji Mkuu alisema Mahakama inao mpango wa miaka mitano wa Maendeleo ya Miundombinu ya Mahakama kuanzia mwaka 2015/2016 hadi 2019/2010 ambapo malengo kupitia ni kujenga jengo moja la Mahakama ya Rufani, majengo 30 ya Mahakama Kuu, majengo 24 ya Mahakama za Hakimu Mkazi, majengo 109 ya Mahakama za Wilaya na majengo 150 ya Mahakama za Mwanzo. Hata hivyo, bado kutakuwa na upungufu mkubwa wa Mahakama za Mwanzo kwa kuwa kuna Kata zaidi ya 3000 na Mahakama za Mwanzo zilizopo ni 960. Lengo ni kuwa na Mahakama ya Mwanzo kwenye kila Kata. Aidha, kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara, ni mikoa 14 tu ndiyo yenye Mahakama Kuu. Baadhi ya mikoa, wananchi wake wamekuwa wakilazimika kufuata huduma za Mahakama Kuu kwenye mikoa mingine, kwa mfano, wananchi wa mkoa wa Singida hawana budi kupata huduma hizo katika mkoa wa Dodoma ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Kanda ya Dodoma. Wananchi wa Kigoma pia wamekuwa wakifuata huduma hizo katika mkoa wa Tabora ambapo ndiyo Makao Makuu ya Kanda ya Mahakama Kuu Tabora. Mikoa yenye Mahakama Kuu ni Dar es salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, Moshi(Kilimanjaro), Tanga, na Bukoba (Kagera). Mikoa mingine ni pamoja na Iringa, na Songea (Ruvuma). Mikoa mingine ni Tabora, Mbeya, Sumbawanga (Rukwa), Mtwara na Shinyanga. Hivi sasa Mahakama ya Tanzania inajenga majengo ya mfano katika utafiti wa Teknolojia ya gharama nafuu na ya muda mfupi iitwayo Moladi katika maeneo ya Kigamboni, Mkuranga, Bagamoyo, Kinyerezi, Kawe pamoja na jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha. Aidha, jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha limekamilika na kuzinduliwa rasmi Septemba mwaka jana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa na tayari limeanza kutumika. inaendelea Uk. 11 HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 8

CHUKUENI HATUA KULINDA IMANI YA WANANCHI Na Sheiba Bulu Wizara ya katiba na Sheria Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (kulia), Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revokati (kushoto), na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju (katikati ) wakisikilikiza taarifa ya Tume yautumishi wa Mahakama iliyokuwa ikiwasilishwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeitaka Tume ya Utumishi ya Mahakama kuendelea kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa watumishi wa Mahakama watakaobainika kukiuka maadili na kuvunja sheria ili kuendelea kujenga na kurejesha imani ya wananchi kwa mhimili wa Mahakama. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichoikutanisha Kamati hiyo ya Bunge, Tume ya Utumishi wa Mahakama na Uongozi wa Mahakama ya Tanzania, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge Mhe. Najma Murtza Giga alisema ni muhimu kwa Tume ya Utumishi wa Mahakama kuchukua hatua stahiki kwa watumishi wote wanaofanya kazi bila kufuata Sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa. Katika kikao hicho kilichofanyika mjini Dodoma, Tume ya Utumishi wa Mahakama iliwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria taarifa yake ya Utekelezaji kwa mwaka 2016/2017. Kikao hicho kilihudhuriwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revokati na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju. Aidha, Mhe. Giga aliiomba Tume ya Utumishi wa Mahakama na Mahakama kwa ujumla kuendelea kuimarisha utendaji kazi wao ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa karibu na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa pamoja na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwani kufanya hivyo kutaimarisha imani ya wananchi kwa huduma zitolewazo na Mahakama. Awali akiwasilisha taarifa hiyo, Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Bibi Enziel Mtei alisema katika kusimamia maadili na nidhamu za watumishi wa Mahakama kwa mwaka wa fedha 2016/2017 tume hiyo ilijadili na kufanya maamuzi juu ya masuala 76 ya nidhamu kwa watumishi wa kada mbalimbali ambapo 72 walifukuzwa kazi na wengine wanne walirejeshwa kazini. Akizungumzia changamoto katika kushughulikia suala la ukosefu wa mafunzo kwa kamati za maadili, Bibi Mtei alesema wamefanya mazungumzo na wadau mbalimbali ili kuona uwezekano wa kushirikiana nao katika eneo hilo. Aliongeza kuwa wanaendelea kuzungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya wenye mamlaka ya kuendesha Kamati za Maadili za Mahakimu ili watenge fedha na kutoa elimu kwa Umma juu ya uwepo wa kamati hizo. 9 HAKIBulletin Julai - Septemba 2017

MLUNDIKANO WA KESI MAHAKAMANI SASA BASI Na Mary Gwera Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali amewaagiza Majaji wote nchini kuhakikisha wanamaliza kesi zote za muda mrefu Mahakamani ifikapo Desemba 15, 2017 ili kuendana na azma ya Mahakama ya kutoa haki kwa wote na kwa wakati. Jaji Kiongozi alitoa maagizo hayo alipokuwa akifungua Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania uliofanyika Septemba 15 na 16, 2017 jijini Arusha. Alisema kuwa Kanda zote za Mahakama Kuu nchini tayari zimeainisha idadi ya kesi zote za kuanzia miaka miwili na kuendelea (kesi za mlundikano) ambazo zitafanyiwa kazi. Nawaagiza Majaji wote nchini kuendelea na zoezi la kusikiliza kesi hususan kesi za muda mrefu Mahakamani, na zoezi hili lianze kufanyika Oktoba 16, mwaka huu na kazi hii ikamilike kufikia Desemba 15, mwaka huu, alisisitiza. Aidha, Mhe.Jaji Kiongozi alizitaja Kanda za Mahakama Kuu ambazo zinaonekana kuelemewa na mzigo wa mashauri, kuandaa orodha ya mashauri causelist wanayohitaji kusaidiwa. Mahakama hizo ni Mahakama Kuu-Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama Kuu-Kanda ya Mwanza, Mahakama Kuu-Kanda ya Bukoba, Mahakama Kuu-Kanda ya Mbeya, Mahakama Kuu-Kanda ya Shinyanga, Mahakama Kuu-Divisheni ya Ardhi na Mahakama Kuu-Divisheni ya Kazi. Aidha, Jaji Wambali pia aliagiza zoezi la uandaaji wa orodha ya mashauri yatakayosikilizwa lifanyike ndani ya wiki moja kuanzia Septemba 18 ili kuwezesha kufahamu uhitaji wa msaada wa Majaji kutoka Kanda nyingine watakaoenda kusaidia kusikiliza na kumaliza mashauri hayo katika maeneo tajwa. Wakati huo huo, Mhe. Jaji Kiongozi amewataka Majaji Wafawidhi kuitisha vikao na Wadau wa Mahakama ili kuwashirikisha katika zoezi hili maalum la kusikiliza na kumaliza kesi zote za muda mrefu Mahakamani. Akifunga Mkutano huo, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma aliwataka Majaji na Watumishi wa Mahakama kwa ujumla kufanya kazi kwa kuzingatia nguzo tatu za Mpango Mkakati wa Mahakama ili kutekeleza majukumu kimkakati na hatimaye kupata matokeo chanya. Majaji Wafawidhi ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa Mpango Mkakati hususan katika nguzo namba mbili ambayo ni Upatikanaji na utoaji wa Haki kwa wakati, kupitia Majaji na Mahakimu waliopo chini yao alisema Mhe. Jaji Mkuu. Akizungumzia jukumu kuu la utoaji haki nchini, Mhe. Jaji Mkuu alisisitiza juu ya kuwa na kumbukumbu sahihi za takwimu za mashauri zilizopo katika Mahakama husika hali ambayo itawezesha kutambua msaada unaohitajika. Aidha; Mhe. Jaji Mkuu alisisitiza juu ya matumizi ya TEHAMA katika uendeshaji wa kesi ili kuendana na kasi ya Teknolojia hali ambayo itawezesha huduma ya haki kuwafikia wananchi kwa wakati. Mambo mengine aliyoyasisitiza Mhe. Jaji Mkuu alipokuwa ni pamoja na ufanyaji kazi kwa ushirikiano kwa Watumishi wote wa Mahakama na kubadili mtazamo hasi change of attitude na kuzingatia maadili katika utendaji kazi. Mkutano wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, uliofanyika kwa siku mbili (2), Septemba 15 na 16 ni mwendelezo wa vikao mbalimbali ambavyo vimekuwa vikifanyika mara kwa mara vyote vikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa azma ya Mahakama ya Tanzania ya kutoa haki kwa wakati inaonekana kutekelezeka. Licha ya agizo lililotolewa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania la kumalizika kwa mlundikano wa kesi za muda mrefu zilizopo Mahakamani, bado Mahakama imejiwekea mikakati yake ya kumaliza kesi ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati. Mahakama na Mikakati ya kumaliza kesi kwa wakati Mikakati iliyowekwa na Mahakama katika kukabiliana na changamoto ya mlundikano wa kesi za muda mrefu kwenye Mahakama mbalimbali nchini ni pamoja na kuandaa Mpango Mkakati wa miaka mitano unaotekelezwa katika kipindi cha 2015/16-2019/20. Mpango huu ni dira na mwelekeo wa Mahakama katika kufikia lengo lake la kuwa Mahakama iliyo karibu na inayofikiwa na wananchi katika kutoa huduma bora za utoaji wa haki. Aidha, Mpango Mkakati huu unalenga kufikia malengo ya dira ya maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2025 ya kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati. Ili kutekeleza suala la kumalizika mapema kwa kesi zilizoko Mahakamani, Mahakama ya Tanzania HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 10

Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye Mafunzo kwa ajili ya kuboresha huduma zinazotolewa na Mahakama ya Tanzania ikiwa na pamoja na kuweka mikakati ya kumaliza mlundikano wa Mashauri Mahakamani. Mafunzo hayo yaliyofanyika April 3-7, 2017 jijini Arusha. imepanga muda maalum wa kumalizika kwa kesi katika mahakama zake mbalimbali kwa mfano, katika Mahakama Kuu kesi inatakiwa kumalizika ndani ya kipindi cha miaka miwili, Mahakama za Mikoa na Wilaya kesi zinatakiwa kumalizika ndani ya miezi 12 wakati katika mahakama za Mwanzo kesi zinatakiwa kusikilizwa na kumalizika ndani ya miezi sita tu. Katika kufikia lengo hili Majaji na Mahakimu wamepangiwa idadi maalum ya mashauri wanayotakiwa kumaliza kwa mwaka. Mkakati mwingine uliowekwa na Mahakama ili kumaliza kesi kwa wakati ni ule wa kufanya vikao na wadau ili kujadili namna ya kumaliza kesi kwa wakati kwa kuwa kitendo cha kuchelewa kwa kesi hakisababishwi na Mahakama pekee bali wadau wa Mahakama pia wanahusika. Aidha; kwa asiyefahamu utaratibu mzima wa uendeshaji wa kesi mahakamani, ni rahisi kwake kuelekeza tuhuma kwa Mahakama kuwa ndiyo inayosababisha kesi kuchukua muda mrefu mpaka kumalizika ikiwemo na dhana ya upokeaji wa rushwa kwa baadhi ya watumishi wa Mahakama wasio waaminifu. Dhana hii inaweza kuwepo lakini isiwe mara zote inahusika. Wengine wamekuwa wakidhani kuwa Mahakama inachelewesha kesi zake bila sababu za msingi. Aidha; kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kutoka kwa Wananchi na Wadau mbalimbali wa Mahakama ya kuwa Mahakama inachelewesha kesi zake bila sababu za msingi, malalamiko haya yamekuwa yakitolewa kwa njia mbalimbali kama Magazeti, runinga, mitandao ya kijamii, Makongamano n.k. Ieleweke kuwa kesi inapofika Mahakamani, inapitia taratibu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanyiwa kazi kwa pamoja karibu na wadau wake mfano: - Wapelelezi, Waendesha Mashtaka, Polisi, Mkemia Mkuu wa Serikali kwa baadhi ya kesi n.k kabla ya kesi hiyo kusikilizwa na hukumu/uamuzi kutolewa na Jaji/ Hakimu. Taratibu/Miongozo ya kufuata katika utoaji wa Haki Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. John Kahyoza anasema kuwa Mahakama zote muhimu zimeanzishwa na Sheria na kuwekewa utaratibu na miongozo ya kufuata ili kutenda haki. Mojawapo ya miongozo hiyo ni kuwa kama refa wa mpira wa miguu, refa hatakiwi kusaidia upande wowote wakati anachezesha mpira kwa hiyo kama ambavyo Refa hawezi kupiga mpira golini hata kama mpira utamfikia refa akiwa eneo zuri la kufanya hivyo. Hali hii pia inafanyika hata kwa Jaji/Hakimu, hata akisikia au kuona kupitia Runinga (TV) kuwa mshtakiwa fulani awe amekutwa na kithibitisho hawezi kumtia hatiani, na utaratibu wa Mahakama kuwa lazima isubiri kuletewa ushahidi mahakamani, alifafanua Mhe. Kahyoza. Aliongeza kuwa Mahakama haijui wala haitakiwi kujua kama mshtakiwa kakutwa na vielelezo au la, wajibu wa Mahakama ni kutoa nafasi sawa kwa pande mbili kuleta mashahidi na vielelezo ili kuweza kutoa haki pasipo shaka yoyote. Kwa upande wake Mwanasheria wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Peace Mpango anasema Kwa mujibu wa Sheria ya Ushahidi Sura ya sita (6) ya mwaka 1967 kifungu cha 110 (1) na kifungu cha 114 (1) vinaeleza kwamba mtu ambaye anashitaki, amefungua shauri, 11 HAKIBulletin Julai - Septemba 2017

anaiomba au kuitaka Mahakama itoe uamuzi au hukumu katika mashitaka au shauri kwa manufaa yake, analazimika kuwasilisha mahakamani ushahidi unaojenga hoja kuthibitisha madai au tuhuma anazozitoa dhidi ya mtuhumiwa au mshitakiwa. Kiwango cha uthibitishaji wa tuhuma, dai au hoja katika kesi ya jinai ni kutoacha shaka yoyote. Hata hivyo pamoja na juhudi za Mahakama ya Tanzania za kuhakikisha inaondosha mashauri yaliyokaa muda mrefu mahakamani, bado Majaji wa Mahakama ya Rufani na wale wa mahakama kuu waliamua kujitolea kuacha likizo zao wanazoenda kati ya mwezi Desemba na Januari ili kusikiliza mashauri mbalimbali ukiwa ni mkakati wao waliojiwekea ili kupunguza mlundikano wa mashauri yaliyoko mahakamani. Kwa maana hiyo katika kesi za jinai anayefungua mashtaka ni waendesha mashtaka (prosecution) kwa niaba ya Serikali akisaidiana na Polisi na hivyo wao ndio wanaowajibika kuleta ushahidi Mahakamani. Ushahidi huo unapaswa kuthibitisha bila shaka yoyote kwamba mtuhumiwa ametenda kosa. Kazi ya Jaji au Hakimu ni kuangalia kama ushaidi uliowasilishwa Mahakamani na Mashahidi wa Mlalamikaji unatosha kumtia mtuhumiwa hatiani au la ambapo hukumu hiyo inatolewa mwisho wa kesi, alifafanua Bi. Mpango. Anaongeza kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sura ya pili (2), Ibara ya 13 (6) (b) inasema ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo. Naye; Mkurugenzi Msaidizi wa Malalamiko-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Happiness Ndesamburo anasema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Taratibu za Makosa ya Jinai Sura ya 225, kifungu kidogo cha 4, Mahakama imepewa mamlaka ya kufuta baadhi ya kesi zilizozidi siku 60 bila kusikilizwa na vilevile Mahakama hiyo hiyo haina uwezo wa kufuta baadhi ya mashitaka mfano kesi za mauaji Murder cases, kesi za Madawa ya kulevya drugs cases mpaka upande wa mashitaka ukamilishe upelelezi na kesi ianze kusikilizwa au upande wa mashitaka uamue kufuta wenyewe. Mhe. Ndesamburo anaeleza vilevile kuna mashauri ambayo Mahakama huweza kuyafuta kama upelelezi haujakamilika na kesi kuanza kusikilizwa ndani ya siku 60 isipokuwa pale tu ambapo kuna hati ya Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Mkoa kuomba nyongeza ya siku sitini (60) na baadaye kufuatiwa na ombi jingine la muda kama huo kupitia hati ya Mkurugenzi wa Mashtaka. Sababu za kuchelewa kumalizika kwa kesi Mashauri yanaposajiliwa Mahakamani hutarajiwa yasikilizwe na hatma yake kujulikana kwa wakati. Hata hivyo yapo mashauri yanayochukua muda kufikia tamati, Kuchelewa kwa kesi/shauri Mahakamani kunaweza kusababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo; uchunguzi kuchukua muda mrefu kwa baadhi ya kesi, Uhaba wa Waendesha Mashitaka, Mawakili, Mashahidi kutopatikana kwa wakati na mara nyingine kutopatikana kabisa, umbali kati Wadaawa (wananchi) na Mahakama. Sababu nyingine ni Wafungwa na Mahabusu kutofikishwa Mahakamani kwa wakati mfano; Wilaya ya Karatu, Longido na Monduli hakuna Magereza wote wanategemea Magereza ya Kisongo iliyopo Arusha, hali hii pia inapelekea kesi kuchukua muda mrefu Mahakamani. Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati ameainisha sababu nyingine ambazo zinapelekea kesi kukaa muda mrefu Mahakamani kuwa ni pamoja na utumiaji wa mfumo wa Kianalojia katika uendeshaji wa kesi, upungufu wa Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani (T), pamoja na Watumishi wa Kada nyingine. Katika jitihada za kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, hivi sasa Mahakama ya Tanzania inatekeleza Mpango Mkakati wa miaka mitano (5), 2015/2016-2019/2020 ambao unazingatia nguzo tatu (3) za Utawala Bora na Menejimenti ya Rasilimali, Upatikanaji na utoaji wa Haki kwa wakati na kuimarisha imani ya Jamii na Ushirikishaji wa wadau. alisema Mhe. Revokati. Ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wakati; Majaji na Mahakimu wamejipangia mikakati kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwa na idadi maalum ya kesi ambazo wanatakiwa kumaliza kwa mwaka. Mfano, Kila Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania anatakiwa kusikiliza na kumaliza angalau mashauri 220 kwa mwaka, huku Mahakimu wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya wanatakiwa kusikiliza na kumaliza kesi 250 kwa mwaka na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo wanatakiwa kumaliza kesi 260 kwa mwaka. Hali kadhalika, kila Mahakama ina ukomo wa umri wa shauri, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ukomo wa kesi kukaa Mahakamani ni miaka miwili (2), Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya ni mwaka mmoja na Mahakama za Mwanzo ni miezi sita (6). Katika uzingatiaji wa ukomo wa muda, Mahakama imefanikiwa kwa kiwango kikubwa hasa kwa Mahakama za mwanzo ambazo zinachukua asilimia 73 ya Mashari yote Mahakamani. Hakuna kesi yenye zaidi ya miezi sita (6) Mahakama za Mwanzo, kwa upande wa Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya, kuna mafanikio isipokuwa isipokuwa kwa yale mashauri ambayo Mahakama hizo hazina mamlaka nayo. Kama mashauri ya mauaji, ugaidi na utakatishaji fedha. Vilevile Mahakama imekuwa ikifanya jitihada za dhati katika kuhakikisha kuwa inashirikisha Wadau wake wanaoambatana nao katika mlolongo mzima wa uendeshaji wa kesi ili kuwa na nguvu ya pamoja kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ili kesi ziweze kumalizika kwa wakati. HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 12

MAHAKAMA YAIMARISHA HAKI ZA WATOTO KWA VITENDO Na Lydia Churi Mahakama Mahakama ni moja kati ya Mihimili mitatu ya dola wenye jukumu la msingi la kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati. Mhimili huu hufanya kazi ya kutafsiri Sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwapatia wananchi haki. Kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (2015/16-2019/20), Mahakama ya Tanzania imeendelea kusimamia haki za Watoto kama zilivyo haki nyingine wanazostahili kuzipata wananchi wa Tanzania. Utekelezwaji wa haki za Watoto zilizoainishwa katika mikataba mbalimbali ya kikanda na Kimataifa na kupewa nguvu ya kisheria kupitia Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009, kunahitaji ushirikiano baina ya Taasisi na wadau wa haki za watoto. Katika kulinda haki za watoto wa Tanzania, Julai 25, 2017, Mahakama ya Tanzania ilizindua Jengo Maalum la Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) katika jiji la Mbeya na kufanya idadi ya majengo hayo kufikia mawili hapa nchini likitanguliwa na lile la Kisutu jijini Dar es salaam. Jengo Maalum la Mahakama ya Watoto lazinduliwa Mbeya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua Jengo Maalum la Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) Julai 25, 2017 jijini Mbeya. Hili ni jengo la Pili kuwapo nchini baada ya lile la Kisutu Jijini Dar es salaam. Jengo hili limejengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) Maendeleo Endelevu hupatikana kwa kuzingatia misingi ya haki za Watoto Kwa kutambua umuhimu wa watoto kuwa ni uhai wa taifa lolote, Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) ilichukua hatua za makusudi 13 HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 kuhakikisha haki za kisheria za watoto zinalindwa kwa kujenga jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya. Akizindua jengo hilo, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema endapo haki za Watoto zitadharauliwa kwa mapana yake sasa, basi azma ya maendeleo endelevu ya nchi hapo baadaye, itakuwa hatarini. Akinukuu andiko la Shirika la Umoja wa Mataifa la

Kuhudumia Watoto (UNICEF), kuwa Maendeleo Endelevu yanaanza na kukamilika kwa misingi ya watoto kuwa salama, wawe ni wenye afya bora na waliopata elimu bora (Sustainable Development starts and ends with safe, healthy and well-educated children- UNICEF, May 2013). Katika neno lake la utangulizi katika andiko hilo, Anthony Lake, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF aliandika kuwa: Haki za watoto na afya yao njema, lazima ipewe kipaumbele katika maandalizi ya ajenda ya maendeleo endelevu ya baada ya mwaka 2015. Uwekezaji kwa manufaa ya watoto ni njia bora ya kufuta umaskini, kuongeza kasi ya kuchanua kwa manufaa kwa wote. Alisema andiko hilo linatukumbusha kuwa ustawi wa Watanzania unaanza na Ustawi wa watoto. Ustawi wa watanzania unaanza na ustawi wa watoto Jaji Mkuu aliendelea kusema kuwa maana ya ustawi wa watanzania unaanza na ustawi wa watoto ni kwamba tayari Katiba imetamka kuwa lengo kuu na jukumu la Serikali ni ustawi wa wananchi na ustawi huo wa wananchi ni lazima ujengewe misingi imara ya ustawi wa watoto wa leo. Alisema jamii ya watanzania bado inayo mengi ya kufanya ili kuendeleza asilimia 50 ya wananchi wake ambao wana umri wa miaka 18 na chini ya miaka hiyo. Alisema, kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwezi Agosti mwaka 2012, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa na idadi ya watu milioni 44,928,923 na kati ya hao, watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi 17 ni asilimia 50.1 Mikataba ya Haki za Watoto iliyoridhiwa na Tanzania Kutungwa kwa Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009 nchini Tanzania kunatokana na mikataba mbalimbali ya kimataifa inayotambua na kulinda haki za Watoto ambayo Tanzania iliridhia. Baadhi ya Mikataba hiyo ni Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto (UN Convention on the Rights of the Child -UNCRC), Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto (African Charter on the Rights and Welfare of the Child-ACRWC). Mikataba mingine ni ule wa United Nations Standard Minimum Rules for the Administration of Juvenile Justice (Beijing Rules) na United Nations Guidelines for the Prevention of Juvenile Delinquency (The Riyadh Guidelines). Matokeo ya Kutungwa kwa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 Tanzania ilitunga Sheria ya Mtoto Namba 21 ya 2009 kwa ajili ya haki, ulinzi na ustawi wa mtoto. Aidha, Sheria hii imekusanya mapendekezo yote ya ndani ya nchi, ya kikanda na ya kimataifa kuhusu maboresho ya haki na maslahi mapana ya mtoto na kutoa nguvu ya kisheria. Baada ya kutungwa kwa Sheria hii, mihimili ya dola imepewa majukumu ya kutekeleza na kuwajibika. Jaji Mkuu wa Tanzania anasema kwa upande wa mhimili wa Mahakama, inategemewa Mahakama ya Watoto isaidie kuwajibika na kutekeleza Sheria ya Mtoto. Alisema kuna maeneo kadhaa katika Sheria ya Mtoto ambayo yanasimamiwa na mamlaka nyingine. Pamoja na ukweli huo, bado Mahakama ya Watoto inaweza kutoa ushirikiano kwa mamlaka hizo au amri za mahakama zikasaidia utendaji wa mamlaka hizo, kwa mfano; mazingira mbalimbali ambayo yameainishwa na Sheria Namba 21 ya 2009 kuwa ni hatarishi kwa mtoto kama vile uyatima, kutelekezwa, kuteswa, kuzurura, kukinzana na sheria ambapo alisema Mahakama ya Watoto inaweza kutoa tafsiri na kupanua wigo wa mazingira hatarishi. Mahakama ya Watoto inaweza kutoa tafsiri na kupanua wigo wa Ulinzi na wajibu wa wazazi kwa matunzo ya mtoto, matibabu na elimu, sifa za mtu kuwa mlezi na uasili wa mtoto; namna gani Mahakama itawasilisha taarifa mbali mbali au kutumia rejista ya watoto walioasiliwa kwa Msajili wa Vizazi na Vifo pamoja na uzuiaji wa kazi za udhalilishaji kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 18. Prof. Juma alisema Mahakama ya Watoto inaweza kutakiwa kutoa miongozo kuhusu mafunzo ya kazi (apprenticeship) kwa watoto chini ya miaka 18 na kuchunguza mikataba ya mafunzo ya kazi ambayo ni kandamizi au yasiyozingatia maslahi ya mtoto. Mahakama ya Watoto pia inaweza kutoa maamuzi ambayo yatazikumbusha Serikali za Mitaa wajibu wao wa kuboresha ustawi wa watoto walio ndani ya mamlaka za Serikali ya Mtaa husika. Mahakama inaweza kuitahadharisha Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kujenga shule maalum za watoto (shule ya Maadilisho) za kutosha. Hii itasaidia Mahakama ya Watoto kuwa, badala ya adhabu ya vifungo gerezani, watoto waliopatikana na hatia watapelekwa. Hatua ya kuanzishwa na kuendeshwa kwa shule hizi itasaidia Mihimili mingine kuisaidia Mahakama na Magereza kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria Namba 21 ya 2009. Aidha Serikali za Mitaa na Serikali Kuu zitakapoanzisha vituo vya kutunzia na kulelea HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 14

watoto wenye shida ya malezi na Bunge kutoa fedha za kutosha kuendesha vituo hivyo zitaisadia Mahakama kwa kiasi kikubwa, alisema Jaji Mkuu na kuongeza kuwa Mahakama za Watoto pia zinaweza kugundua mapungufu katika Sheria na kupendekeza kuwa Waziri mwenye dhamana ya watoto atunge kanuni stahiki. Sheria ya Mtoto yahitaji Ushirikishi Akizungumzia ushiriki na ushirikishwaji wa Sheria ya Mtoto, Jaji Mkuu alieleza kuwa kuwa sheria hii imesimama katika misingi ya ushirikiano baina ya mihimili yote, ushirikiano na wadau mbali mbali kama UNICEF na NGOs, taasisi ambazo zinashughulika na masuala ya haki za watoto. Alisema, Sheria hii pia inaitaka Mahakama ichukue uongozi, na kuna masuala ambayo mihimili mingine imepewa nafasi ya uongozi hivyo Mahakama inayo nafasi nzuri ya kuipa uhai sheria hii kwa kuwa kwanza, haki zote stahili zilizoainishwa ndani ya Sheria hii zinamfaidisha mtoto, pili, Sheria hii inapotafsiriwa, pale ambapo wanaona kuna kutofahamika, utata wawe na ujasiri wa kuielekeza sheria kufikia malengo mazuri yaliyowekwa na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa kuhusu haki ya watoto. Mahakama pia inayo nafasi nzuri ya kuipa uhai Sheria hii kwa sababu Mahakimu katika Mahakama ya Watoto watakuwa na nafasi ya karibu kabisa kuona namna vifungu mbali mbali vya Sheria hii vinavyofanya kazi, hivyo Jaji Mkuu aliwaagiza Mahakimu wanaosikiliza kesi za Watoto kuorodhesha mapungufu ya Sheria hii na kuyawasilisha kwenye kamati ya Kanuni ya Jaji Mkuu kwa ajili ya kupendekeza kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu mabadiliko ya Sheria. Akisisitiza juu ya kulinda haki za Watoto, Jaji Mkuu aliwataka Mahakimu wanaosikiliza kesi za Watoto wasome taarifa za Utekelezaji zinazowasilishwa na Tanzania na pia zile zinazowasilishwa na mataifa mengine kuhusu Tanzania ili waweze kugundua mapungufu ya kiutekekezaji na hivyo kuweza kupanga namna ya kuboresha utekekezaji. Mahakimu hao pia wametakiwa kufuatilia haki za Watoto pindi wanapofanya ukaguzi kwenye Magereza. Aidha, jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya lililojengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na UNICEF limegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Milioni 415 ambapo Mahakama imechangia kiasi cha shilingi milioni 214 na UNICEF shilingi milioni 201. Jengo hili lilianza kutumika April 18, 2017 na lina ofisi mbili za Hakimu, Ofisi ya Wakili wa Serikali, ofisi ya Afisa Ustawi wa Jamii na chumba cha Mawakili wa Kujitegemea. Jengo hili limejengwa jijini Mbeya kwa kuzingatia upatikanaji wa wadau na huduma zote muhimu za haki kwa mtoto. Huduma hizo ni pamoja na uwepo wa shule ya maadilisho (approved school) ikiwa ni pekee nchini, kuwepo kwa Mahabusu ya watoto mkoani humo, na kuwepo kwa dawati la jinsia la watoto lenye viwango vinavyotambulika lililoanzishwa na Jeshi la polisi. Mahakama hii pia ilianzishwa kutokana na uwepo wa timu ya ulinzi na usalama wa mtoto (child protection team) na kuwepo kwa mfumo wa marekebisho ya tabia kwa watoto (community rehabilitation programme). Inaendelea Uk. 17 Jengo Maalum la Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) lililoko jijini Mbeya lilizinduliwa Julai 26, 2017. Jengo hili limejengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (UNICEF). Jengo hili linakuwa ni la pili nchini kuanzishwa kwa ajili ya kusikiliza mashauri yanayowahusu Watoto. Jengo lingine Maalum la Mahakama ya Watoto liko Kisutu jijini Dar es salaam. 15 HAKIBulletin Julai - Septemba 2017

KITUO JUMUISHI CHA UTOAJI HAKI CHAZINDULIWA MBEYA Na Lydia Churi-Mahakama Mbeya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amezindua jengo la Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya ambapo Mahakama hiyo imekuwa ya kwanza nchini kufanya kazi kama Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki. Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya lilifanyiwa ukarabati mkubwa ambapo baada ya kukamilika kwa ukarabati huo, hivi sasa jengo hilo linajumuisha ofisi za wadau wa Mahakama wakiwemo Polisi, Magereza, na Ustawi wa Jamii ili kurahisisha kazi ya utoaji haki. Akizindua jengo hilo Julai 27, 2017 katika jiji la Mbeya, Jaji Mkuu alisema maboresho ya jengo hilo ni hatua ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015/16-2019/20) wa Mahakama ya Tanzania ambao moja ya nguzo zake ni kusogeza huduma za Mahakama karibu zaidi na wananchi. Alisema pamoja na kuboreshwa kwa huduma za Mahakama bado wananchi watapenda kuona wanahudumiwa na watumishi wanaofuata maadili ya kazi zao hivyo aliwataka watumishi wote wa Mahakama nchini kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao ipasavyo kwa kutanguliza mbele utu. Jaji Mkuu alisema kuzinduliwa kwa jengo hilo ni ishara kuwa Mahakama ya Tanzania inabadilika na kuachana na ujenzi wa kizamani wa majengo yake ambapo alisema sasa Mhimili huo unajenga majengo yanayozingatia matumizi ya Teknolojia ya Habari Imetoka Uk. 7 na Mawasiliano (TEHAMA) pia ambayo yatatoa nafasi kwa wadau wa Mahakama kuweka ofisi zao ili kurahisisha suala la utaoji haki. Aidha, Jaji Mkuu aliiomba Serikali kutenga fedha kwa ajili ya uanzishwaji wa Mahakama pale inapoanzisha maeneo mapya ya kiutawala zikiwemo Wilaya na Mikoa ili kuisaidia Mhimili huo kuendelea kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi. Aliwaomba Wakuu wote wa Mikoa nchini pamoja na wakuu wa Wilaya kuwa sehemu ya maboresho ya Mahakama kwa kuwa wanategemewa kuratibu ustawi wa maendeleo ya wananchi hivyo basi viongozi hao hawana budi kusimamia ipasavyo suala la amani kwa kutatua migogoro katika jamii. Jaji Mkuu pia aliishukuru Benki ya Dunia kwa mchango wake katika ujenzi wa Mahakama nchini, alisema hivi sasa Taasisi hiyo imetoa wazo la kuanzishwa kwa Mahakama zinazotembea (Mobile Courts) ili kutimiza azma yake ya kusogeza karibu huduma za Mahakama kwa wananchi. Jengo la Mahakama Kuu kanda ya Mbeya lilianza kufanyiwa ukarabati mkubwa Februari 2016 na kukamilika Aprili 2017. Aidha, ukarabati huo uligharimu zaidi ya shilingi bilioni 3.4 ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa mifumo ya kisasa (video conferencing) ili kurahisisha utendaji kazi na kumaliza mashauri kwa wakati. Mafanikio katika Usikilizwaji wa Mashauri ya Zamani (Backlog) Kwa Mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, hadi kufikia Desemba mwaka 2016, mlundikano wa mashauri kwenye Mahakama mbalimbali nchini ulipungua kutoka wastani wa asilimia 46 mwaka 2013 na kufikia wastani wa asilimia 21 kwenye Mahakama ya Rufani na kutoka wastani wa asilimia 33 mwaka 2013 na kufikia wastani wa asilimia 9 kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania. Katika Mahakama za Hakimu Mkazi/Mkoa, idadi ya mlundikano wa mashauri ya zamani ilipungua na kufikia wastani wa asilimia 3 kutoka wastani wa asilimia 9 mwaka 2013. Aidha kwenye Mahakama za Wilaya mlundikano wa mashauri ulipungua kutoka wastani wa asilimia 9 mwaka 2013 na kufikia wastani wa asilimia 3 mwaka 2016 wakati kwenye Mahakama za Mwanzo mlundikano ulishuka kutoka wastani wa asilimia 2 mwaka 2013 hadi kutokuwa na mlundikano. Mahakama ya Tanzania haina budi kujivunia mafanikio haya makubwa hasa kwa Mahakama za chini ambako asilimia 80 ya kesi zinazofunguliwa na wananchi zipo kwenye ngazi hizo. Mahakama pia imefanikiwa kupunguza mlundikano wa mashauri yenye zaidi ya miaka miwili kutoka mashauri 10,832 yaani sawa na asilimia 10 mwaka 2012 hadi kufikia mashauri 2,702 sawa na asilimia tano (5%) mwaka 2016. Watanzania pamoja na wadau wengine wa Mahakama kama Jeshi la Polisi, Magereza, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-TAKUKURU, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali,pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali hawana budi kushirikiana na Mahakama ya Tanzania bega kwa bega ili kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati. HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 16

Imetoka Uk. 15 Ushirikiano wa Mahakama na UNICEF Katika kipindi cha takribani miaka mitano yaani tangu mwaka 2012, UNICEF na Mahakama walishirikiana katika kutengeneza kanuni za Mahakama ya Watoto ikiwa ni matakwa ya kifungu cha 99 (1) cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 ambacho kinamtaka Jaji Mkuu kutengeneza kanuni za kutumika katika uendeshaji wa kesi katika Mahakama za Watoto. UNICEF ilitoa msaada wa kitaaluma (technical support) na fedha katika kuandaa kanuni ambazo zilitangazwa katika Gazeti la Serikali No 182/2016. Uandaaji wa kanuni hizo ulihusisha wadau mbalimbali wa haki za watoto kama Majaji, Mahakimu, Mawakili wa Serikali, Maafisa Ustawi wa Jamii, na Mashirika yasiyo ya kiserikali vinayotoa msaada wa kisheria na vyombo vingine vinavyohusika na masuala ya mtoto. Aidha, UNICEF imeshirikiana na Mahakama katika kuandaa mafunzo kwa wakufunzi (TOT) juu ya uendeshaji wa kesi za watoto kwa mujibu wa Sheria na kanuni za watoto.wakufunzi hao walitoka Mahakama ya Tanzania, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Idara ya Ustawi wa Jamii. UNICEF pia imeshirikiana na Mahakama kutoa mafunzo kwa Mahakimu, Mawakili, wa Serikali na Waendesha Mashtaka, Maafisa Ustawi wa Jamii, taasisi zinazotoa msaada wa kisheria na Taasisi zisizo za Kiserikali katika Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, na Iringa. Aidha mafunzo kwa wadau wote yanaendelea kufanyika katika wilaya mbalimbali kwa kutumia wakufunzi waliopata mafunzo yaliyotolewa na UNICEF na Mahakama. Kwa sasa Mahakama na UNICEF wanashirikana katika kutengeneza rejista maalum za mashauri ya watoto, kupitia mwongozo wa mafunzo (Training Manual) kwa kushirikiana na Chuo cha Mahakama Lushoto na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo (Law School of Tanzania). Sambamba na hilo, kwa mwaka huu wa fedha UNICEF wataendelea kushirikiana na Mahakama katika mpango endelevu wa kutoa mafunzo kwa wadau wote wa haki za Watoto. Pia UNICEF imeonyesha nia ya kushirikiana na Mahakama katika ukarabati mdogo wa Mahakama ili kuziweka katika mazingira rafiki kwa watoto. Hata hivyo, bado kuna haja ya kuongeza idadi ya Majengo Maalum ya Mahakama za watoto nchini kutokana na kuongezeka kwa kesi za watoto na nyingine ambazo kwa namna moja au nyingine zinawahusisha watoto katika mikoa mbalimbali nchini ili kutekeleza azma ya kulinda na kutetea haki za Mtoto. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mahakama ya watoto jijini Mbeya, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali aliiomba UNICEF kuangalia uwezekano wa kujenga majengo mengine manne ya Mahakama za watoto katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Tabora ili kuwapatia Mahakimu fursa ya kujifunza kwa vitendo namna Mahakama za watoto zinavyofanya kazi. Mwakilishi wa UNICEF nchini, Stephanie Shanler akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya. 17 HAKIBulletin Julai - Septemba 2017

Habari Katika Picha Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa nne kulia) na Viongozi wengine wa Mahakama pamoja na Chama cha WanasheriaTanganyika (TLS) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mawakili waliokubaliwa na kuapishwa mwezi Julai, 2017 jijini Dar es Salaam, katika Sherehe hiyo jumla ya Mawakili 248 waliapishwa na kufanya idadi ya Mawakili nchini kufikia zaidi ya 6000. Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Mahakama ya Tanzania wakiwa kwenye Kikao Kazi Maalum cha kutathmini Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama(2015/16-2019/20) kilichofanyika Agosti 7-15, 2017 mkoani Morogoro. HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 18

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli akiwa pamoja na viongozi wenzake wa mihimili ya Dola ambaye ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibarhim Hamis Juma na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai mara baada ya Rais kumuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu, jijini Dar es salaam. Majaji wa Mahakama ya Rufani na wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa Ikulu wakati wa kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma 19 HAKIBulletin Julai - Septemba 2017

Viongozi wakuu wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Watatu kushoto waliokaa) alipotembelea Mahakama hivi karibuni na kupokea taarifa ya utekelezaji wa kazi za Mahakama. Anayemfuatia kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, akifuatiwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome. Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bibi Bella Bird akimuelezea jambo Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Khamadu Kitunzi kuhusu ujenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Mahakama ya Tanzania. Katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma walipotembelea ujenzi huo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam. Jengo hilo la kituo cha Mafunzo cha Mahakama litatumika kutoa Mafunzo kwa Watumishi wa Mahakama pamoja na Wadau ili kuboresha huduma. HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 20

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Nachingwea baada ya kuzungumza nao wakati alipoitembelea Mahakama hiyo akiwa katika ziara ya kukagua kazi zinavyofanyika pamoja na kusisitiza juu yya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania katika kanda za Songea na Mtwara. Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Nachingwea pamoja na viongozi wa Mahakama wakimsikiliza Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati alipotembelea Mahakama hiyo akiwa katika ziara ya kukagua kazi zinavyofanyika pamoja na kusisitiza juu yya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania katika kanda za Songea na Mtwara. 21 HAKIBulletin Julai - Septemba 2017

JENGO LA MAHAKAMA YA WILAYA KIGAMBONI MUONEKANO WA MCHORO WA JENGO LA MAHAKAMA KUU KIGOMA NA MARA YANAYOENDELEA KUJENGWA HAKIBulletin Julai - Septemba 2017 22

USINYAMAZE PAZA Sauti yako, Upate Haki yako JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA Mahakama ya Tanzania, 26 Barabara ya Kivukoni, S. L. P. 9004, 11409 Dar es Salaam Email: Info@judiciary.go.tz Blogs: Tanzaniajudiciary.blogsport.com Tovuti: www.judiciary.go.tz TANGAZO KWA WANANCHI WOTE MAONI, MAPENDEKEZO NA MALALAMIKO DHIDI YA VITENDO VISIVYO VYA UADILIFU NA RUSHWA USHIRIKI WA WANANCHI NA WADAU MAPAMBANO DHIDI YA VITENDO VYA KUOMBA RUSHWA, UKOSEFU WA MAADILI NA UTOAJI WA LUGHA ZISIZOZINGATIA STAHA NA UADILIFU YATAFANIKIWA TU ENDAPO; WANANCHI NA WADAU WATATOA TAARIFA ZA KWELI ZA MATUKIO YA KWELI YA WATUMISHI WA MAHAKAMA WANAOFANYA VITENDO HIVYO ILI HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE DHIDI YA UKWELI HUO. MPANGO MKAKATI RUSHWA NA UKOSEFU WA MAADILI MPANGO MKAKATI WA MAHAKAMA WA MIAKA 5 (2015 2020) UMELENGA KUWAFIKIA WANANCHI WOTE ILI WAWEZE KUTOA PONGEZI KWA MATENDO MAZURI; AMA MAONI, MAPENDEKEZO NA MALALAMIKO DHIDI YA VITENDO VISIVYO NA MAADILI KWA KUTUMIA NAMBA ZA SIMU NA ANWANI ZILIZOONYESHWA HAPA CHINI. ENDAPO UNAHISI UNAOMBWA RUSHWA, UNASUMBULIWA AMA KUNA UKIUKWAJI WA MAADILI KINYUME NA UTARATIBU; BILA KUSITA TOA TAARIFA KWA UJUMBE MFUPI WA MANENO, WHATSAPP AMA SIMU KWA MAHAKAMA NA/ AMA TAKUKURU NA WENYEVITI WA KAMATI ZA MAADILI KWENYE NAMBA ZA SIMU HUSIKA NA HATUA STAHIKI ZITACHUKULIWA MARA MOJA. AIDHA, UNAWEZA FIKA NA KUONANA NA MKUU WA DAWATI LA MALALAMIKO AU MKUU WA ENEO HILO. RUSHWA NI DHAMBI, RUSHWA NI ADUI WA HAKI NA HUDIDIMIZA TAIFA. USISHAWISHI, USITOE WALA USIPOKEE RUSHWA MAHAKAMA MAKAO MAKUU Makao Makuu 0744 000790 Mahakama Kuu, Masjala Kuu 0744 000780 Idara ya Ukaguzi na Maadili 0752 500400 (WhatsApp na sms) TAKUKURU (PCCB) MAKAO MAKUU Simu ya bure 113 Makao Makuu 022-2150043 Makao Makuu 022-2150044 Makao Makuu 022-2150045 Makao Makuu 022-2150046 MKOA WA DAR ES SALAAM TAKUKURU (PCCB) DAR ES SALAAM KAMATI ZA MAADILI Kuu Kanda ya Dar es Salaam 0744000740 Takukuru Dar Es Salaam 022-2150043 Utumishi wa Mahakama 0746000200 Mahakama Tume ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu 0744000601 Takukuru Dar Es Salaam 022-2150044 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam 0746000272 Mahakama ya Wilaya Kinondoni 0744000602 Takukuru Wilaya ya Kinondoni 022-2170852 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni 0746000306 Mahakama ya Wilaya Ilala 0744000603 Takukuru Wilayaya Ilala 022-2861088 Mkuu wa Wilaya ya Ilala 0746000307 Mahakama ya Wilaya Temeke 0744000604 Takukuru Wilaya ya Temeke 022-2850633 Mkuu wa Wilaya ya Temeke 0746000308 (WhatsApp na sms) (WhatsApp na sms) Mahakama ya Tanzania 26 Kivukoni Avenue/Ohio, S.L.P. 9004, Dar es Salaam Tanzania. Simu: +255 22 2124187, Nukushi: +255 22 2116 654 Barua-pepe: info@judiciary.go.tz, Blogu: tanzaniajudiciary.blogspot.com Tovuti: www.@judiciary.go.tz