TUMERITHI TUWARITHISHE

Similar documents
Ripoti ya Warsha Ya Washikadau Ihusuyo Mpango wa Uendeshaji wa Mazingira Wilayani Rufiji Iliyofanyika Utete Rufiji Juni 2000

BARAZA LA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA (Mawasiliano yawasilishwe kwa MSAJILI)

John Lesson Eighteen Yohana Somo la Kumi na Nane

Pre-Departure Program Swahili Unit 11 Worksheet UNIT 11: LOCATIVES, PREPOSITIONS, AND RELATIVE AND OBJECT INFIXES

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF

MOROGORO JARIDA LA. ISSN Toleo Na.4 Julai 2005 BODI ZA AFYA ZA WILAYA - SAUTI YA WANANCHI

Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya

HOTUBA YA JAJI MKUU MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA SIKU YA SHERIA, DAR ES SALAAM, TAREHE 1 FEBRUARI, 2018

MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA KIRINYAGA YA KATI MWAKA WA 2013

HAKIBulletin RAIS AMTEUA PROF. JUMA KUWA JAJI MKUU WA TANZANIA. Ndani: JARIDA LA MAHAKAMA YA TANZANIA

UWAJIBIKAJI NDANI YA JESHI LA POLISI

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF BOMAS OF KENYA

TAARIFA YA HISTORIA YA MKOA WA MWANZA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA

AHMAD AL-RAYSUNI. SWAHILI VERSION idara ya Lugha na ukalimani ya Chuo Kikuu cha waislamu cha Morogoro. IIIT Mfululizo wa Vitabu kwa Muhtasari

HAKIBulletin JAJI MKUU AWAASA WAHITIMU WA SHERIA KUJIENDELEZA KITAALUMA HALIUZWI! BENKI YA DUNIA USULUHISHI MUAFAKA MAHAKAMA MAWAKILI MAHAKAMA KUU,

KITABU CHA MAFUNZO KWA WATOA DAWA KATIKA MADUKA YA DAWA MUHIMU

February 9, 2017 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 16 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY

Imâm Al-Albâni, Katika Kumsifu Mwanafunzi Wake, Muheshimiwa Sheikh Ali Hasan 1

Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtukufu Mtume

Ahadi za Serikali II. Zimekusanywa na HakiElimu Agosti 2007

Khadija-tul-Kubra. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Published on Books on Islam and Muslims Al-Islam.org (

There is one God Mungu ni mmoja 1

Gazeti la kwanza la Kiislam kutolewa kwa lugha ya Kiswahili - mwaka 1936

Kuishi Maisha Tele. Katika mwanzo wa mwaka mpya, Niliwapa changamoto

MALAIKA: WAJUMBE WA MUNGU

EVANGELISM FOR CHRIST UINJILISTI KWA AJILI YA KRISTO

Rainbow of Promise Journal

HALI YA UISLAMU. Maelezo ya kumsaidia Mkristo aufahamu Uislamu

HAKIKA YA AHMADIYYA. Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania

DINI JE, DINI NI MUHIMU?

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MANDERA CENTRAL CONSTITUENCY, HELD AT RHAMU

Sura al-ahzaab. Tafsiri na Maelezo. Abdilahi Nassir

IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE.

BARUA YA TATU KWA SHEIKH UBAYD AL-JÂBIRĪ [AULIZWA SHEIKH UBAYD] NA Sheikh Sālim at-twawîl (hafidhahullāh)

Ukweli Uliopotea - Sehemu Ya Tatu

Ukoo Wake Na Kunasibika Kwake:

Published on Al-Islam.org ( Home > Mahari ya Damu > Mahari ya Damu. Mahari ya Damu

VACATION BIBLE SCHOOL VBS. Newsletter. #Rebuilding through prayer, hard work & perseverance.

NEW LIFE IN CHRIST MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO

Zanzibar itafutika-mwanasheria

Bismillah ar-rahman ar-raheem SHAHADA 1 YALIYOMO

YA AL HABBIB SAYYEID

ZABURI 91 mstari 1. KJV-lite VERSES

Tawasali. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags:

NEW INTERNATIONAL VERSION

Uwezo Kenya National Learning Assessment 2014

Ujasiri wa Kimaadili. Mojawapo ya madhumuni ya maisha ya duniani

TAUS RETREAT NEWS LETTER # 1

Ukweli wa hadith ya karatasi

NGUO-NYINGI MKOTI: MWANZISHAJI WA MJI WA NGOJI (ANGOCHE)

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS IJARA CONSTITUENCY AT IJARA BARAZA PARK

Je, Umesikia Juu Ya Kanuni Nne Za Kiroho?

Toleo la kwanza: June, 2007 (Jamaadi Aakhar, 1428) Vitabu ii.

NEW INTERNATIONAL VERSION

REPUBLIC OF KENYA COUNTY ASSEMBLY OF KILIFI THE HANSARD. Wednesday, 29 th March, 2017

Imam Mahdi katika Usunni Na Ushia

Kitabu Changu cha Mistari ya Biblia Swahili

Ezra 3 Lessons Download or Read Online ebook ezra 3 lessons in PDF Format From The Best User Guide Database

2002 Version of the Basic Talk on "Using African Proverbs, Sayings, Idioms, Riddles, Stories, Fables, Play

December 6, 2017 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 6 th December The House met at 9.30 a.m.

JINA KAMILI CHEO SIMU YA OFISINI Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwandishi Mwendesha Ofisi

Yassarnal Quran English

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

Vitendawili Vya Swahili

TALKING ABOUT ONESELF TO ACT IN THE WORLD: A SWAHILI AUTOBIOGRAPHY (SHAABAN ROBERT, MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

2

MRADI WA METHALI (SANALASKUJA PROJEKTI)

NAIROBI CITY COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

Youth and Faith A collection of texts on the subject A collaborative Magazine Content

AND REACTION IN SWAHILI POETRY.

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

WELCOME TO GOD S SERVICE A.C.K. ST. LUKE S PARISH UMOJA & TENA CHURCH QUOTE OF THE WEEK PRAYER OF THE DAY

JUNE 4, Acts 2:1-12 and Offering...Pastor Maromy Samuel All Hail the Power of Jesus Name led by Haitian Congregation Worship Team

In Search of Contact: Rhetorical Questions in the Communicative Frame of the Funeral Sermon

No. Book Name Category Type Price 1 AFYA MARIDHAWA -1 SWAHILI SUBSCRIPTION 2, AFYA NA UZIMA SWAHILI SUBSCRIPTION 8,500.00

Change Your Destiny CONFERENCE

The Lord be with you And with your spirit

(Cell) (Cell) (Cell) (Landline) (Cell)

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MANDERA CENTRAL CONSTITUENCY, HELD AT ELWAK

2

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

MAOMBI YA QUR'AN TUKUFU SHEIKH MUZAFFAR AHMAD DURRANI

I Peter 4:12-19 Suffering with a Blessing

ATONEMENT IN AFRICAN PLURALISTIC CONTEXT: EXAMPLES FROM THE LUHYA OF WESTERN KENYA

MASHAIRI YA WAADHI "VERSES OF ADMONITION": the people of Mombasa rebuked by P J. L Frank! and Yahya Ali Omar

Cultural Considerations Tanzania Excursion

Mashairi ya Masaibu ya Karbala

Innovations and new trends in Small Christian Communities (SCCs) in Africa today By Joseph Healey, M.M.*

ARCHDIOCESE OF DAR ES SALAAM, TANZANIA

Impact of Teaching Civic and Religious Values in the National Curriculum on improving Social Responsibility in Tanzania: The Analytical View

HOLY COMMUNION ACCORDING TO THE KENYAN RITE

WELCOME TO GOD S SERVICE ACK ST. LUKE`S PARISH UMOJA Theme: Endeavoring to touch the heart of God, (Matt 25:40). Kuazimia kumpendeza Mungu

Where is Africa? 2. What is African heritage? 3. What is the African heritage in the Bible? 6. What are African ways of worship?

I Peter 2:9-12 Who Are You?

Mother s Day. Fête des mères 母亲节 母の日 יום המשפחה म त द वस 母親節. Día de la Madre 어머니날. Ημέρα της μητέρας

Who Challenges Whom? Exploring and Responding to Theological Diversities between the Pentecostal-Charismatic Churches and the Lutheran Church

REPUBLIC OF KENYA COUNTY ASSEMBLY OF KILIFI THE HANSARD. Wednesday, 3 rd October, 2018

Transcription:

TUMERITHI TUWARITHISHE

2 3

Kampeni ya kuboresha Utunzaji wa Misitu Misitu ni rasilimali ambayo ina mchango mkubwa katika maisha ya Watanzania wengi lakini matumizi mabaya ya misitu na yaliyopitiliza pamoja na utawala mbovu yanatishia uwepo wa misitu hiyo na mchango wake katika maendeleo. Ripoti ya Mwaka 2007 1 imeonyesha mapungufu makubwa katika biashara ya mbao hususani katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kimazingira. Kampeni ya Mama Misitu inalenga kutatua mapungufu hayo kwa kuboresha utawala na utunzaji wa misitu ili Watanzania waweze kunufaika zaidi kutokana na utunzaji endelevu wa misitu. Kampeni hii ilizinduliwa na Kikundi Kazi Cha Masuala ya Misitu Tanzania kinachoratibiwa na Jumuiko la Maliasili Tanzania kwa lengo la kufanya majaribio mnamo Mwaka 2008. Mwaka 2012, kampeni ya Mama Misitu imezindua mpango wa miaka mitano ili kufikia jamii nyingi zaidi kutokana na uzoefu na mafunzo yaliyopatikana katika kampeni ya awali. Mafunzo yaliyotokana na kampeni ya awali Kampeni ya Mama Misitu ilitekelezwa katika wilaya za Rufiji na Kilwa na ilifanikiwa kutatua vikwazo mbalimbali ikiwemo utawala na utunzaji wa misitu ili kujikimu kimaisha. Kwa kupitia kampeni hii, jamii imeweza kujifunza sheria zinazohusiana na uvunaji wa mbao, nafasi ya serikali katika kutunga sheria na kuzisimamia ili kulinda rasilimali misitu, thamani ya mazao ya misitu yaliyovunwa kihalali na yale yasiyovunwa kihalali na jinsi ya kuwashughulikia majangili wa misitu na kuwapeleka mbele ya sheria. Hivyo kampeni ya Mama Misitu inatarajia kutanua wigo wake wa utekelezaji kutokana na uzoefu uliyopatikana katika kampeni ya awali ili kuweza kufikia jamii nyingi zaidi. 1 Milledge, S.A.H., Gelvas, I.K. and Ahrends, A.2007. Forestry, governance and national development: Lessons learned from a logging boom in southern Tanzania. TRAFFIC East & Southern Africa/ Tanzania Development Partners Group/Ministry of Natural Resources of Tourism, Dar es Salaam 4 5

Kukuza malengo na matokeo Kampeni mpya ya Mama Misitu ya miaka mitano itazinduliwa katika wilaya nne (4) ambazo ni Rufiji, Kilwa, Kisarawe na Kibaha kabla ya kuongezeka na kufikia jumla ya wilaya nane (8). Washiriki kumi na moja (11) wataitekeleza kampeni hii katika ngazi za wilaya na kitaifa. Watekelezaji katika ngazi ya kitaifa ni; LEAT, TNRF, Femina HIP, MJUMITA, JET, Policy Forum na TRAFFIC. Watekelezaji katika ngazi ya wilaya ni, TFCG, MCDI, WWF, WCST 2. Katika kila wilaya hizo, kampeni hii itaongeza uelewa na kuboresha mbinu za utunzaji wa misitu katika jamii. Kampeni ya Mama Misitu kupitia wabia wake imeweza kutambua changamoto katika utawala wa misitu ambayo ingependa kushughulikia matatizo yafuatayo: Wananchi kutofahamu haki na wajibu wao katika masuala ya misitu Utekelezaji hafifu wa sera na sheria mbalimbali zinazohusu usimamizi wa rasilimali misitu Usimamizi mbovu wa sheria za ardhi Udhibiti mbovu wa sekta ya biashara; pamoja na Kuwepo kwa udanganyifu mwingi katika mnyororo mzima wa biashara ya mbao katika ngazi mbalimbali. Kampeni ya Kitaifa yenye muktadha toka kwa jamii Wanajamii wanapaswa kunufaika na rasilimali za misitu na kwa sababu hii mawazo yao ndiyo kiini cha kampeni hii. Kijitabu hiki kinajumuisha shuhuda kutoka katika jamii kuhusu manufaa na vikwazo katika kuboresha utawala wa rasilimali misitu nchini Tanzania. 2 Kuona majina kamili ya washiriki hawa angalia nyuma ya kijitabu hiki. 6 7

Bwana Omari Kijumile ni mzawa na mkulima katika kijiji cha Ruhatwe kilicho katika wilaya ya Kilwa. Amehusika na kampeni ya Mama Misitu kutoka mwanzo ambapo wataalamu walifika na kutoa mafunzo na kuwaelimisha watu mambo mbalimbali kuhusu sera na sheria ambazo zinahusika katika utunzaji wa misitu Tanzania. Mfano, Sera ya Misitu ya mwaka 1998, Sheria ya Misitu ya mwaka 2002, Sheria ya Ardhi ya mwaka 1998 na 1999 pamoja na Sera ya Mazingira ya mwaka 2004. Vifaa vilivyokuwa vikitumika wakati wa kampeni hiyo vilijumuisha maigizo, mashairi na ngoma za asili. Kutokana na hilo kuna mafanikio mengi yamejitokeza kwenye hizi hatua za mwanzo tu za Mama Misitu. Kumekuwa na ongezeko kubwa la jamii kujihusisha ili kujua namna na umuhimu wa miti na misitu na sera na sheria zinazotumika kulinda utunzaji wa mazingira. Jamii imefahamishwa juu ya ukataji miti unaopelekea kuongezeka kwa ukame, kupata mvua kidogo za msimu au kupata mafuriko pindi mvua zinyeshapo na mabadiliko ya hali ya hewa ingawa zinabaki kama changamoto. Changamoto ya muhimu iliyotajwa na Bw. Omari ilikuwa ni mgongano uliopo kati ya sera ya Kilimo Kwanza na utunzaji wa misitu. Kinachotokea ni kwamba jamii inaangalia kilimo kama inavyohamasishwa na sera za Kilimo Kwanza ikimaanisha ukataji wa miti na misitu inayotakiwa kuhifadhiwa ili kupisha shughuli za kilimo. 8 9

Mama Mwanaisha Abdallah Likoko ni mzawa katika kijiji cha Kikole wilayani Kilwa. Ameshuhudia mabadiliko aliyoyaona katika kijiji chake kwa jinsi ambavyo misitu inahifadhiwa. Hapo mwanzoni miti na misitu ilikuwa ikikatwa sana na hakukuwa na aliyekuwa akijishughulisha na shughuli hizi kuona ni nini kinakatwa na kinapandwa na ni nani aliyekuwa akikata miti. Mabadiliko anayoyaona sasa Mwanaisha ni kuwa miti inakatwa kwa kufuata sheria na utaratibu uliopo wa uhifadhi misitu. Ameweza pia kuchangia katika mabadiliko katika misitu ambayo yameletwa na kampeni ya Mama Misitu. Kwa sasa ana matumaini kuwa vizazi vijavyo vitakuta misitu na miti minene. Mwanaisha alieleza kuwa jamii kubwa ya watu wana ufahamu na uelewa juu ya umuhimu wa miti na misitu ingawa kuna baadhi ya watu wanaokataa kusikiliza na kuelewa na pia anaona changamoto inayowakuta wanawake katika suala hili la utunzaji wa misitu. Wanawake wanaathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na miti na misitu. Mwanaisha alieleza kuwa wanawake wanaelewa kwa haraka umuhimu wa miti katika kuleta mvua, vyanzo vya maji na kadhalika lakini wanaume ni watu wa kutafuta fedha kwa hiyo wanaangalia miti kama chanzo cha wao kupata fedha na hivyo hawatakubaliana na suala la kuhifadhi misitu kama ambavyo wanawake wanafanya. Hivyo kuna umuhimu wa kuongeza mkazo zaidi kwa wanaume juu ya uhifadhi wa misitu kwa jamii. 10 11

Bwana Mwalami Ali Kwangaya ni mzawa wa Rufiji na Katibu Muhtasi wa mtandao wa kuhifadhi misitu kijijini kwake. Anashuhudia kuwa kabla ya kampeni ya Mama Misitu jamii haikujua kuwa misitu na miti ni mali yao. Hivyo bila kuelewa suala hilo hawakuona umuhimu wa kuhifadhi miti na misitu husika. Kampeni ya Mama Misitu kutumia nyimbo, maigizo na sanaa imewasaidia wanajamii kuona athari za ukataji miti uliopitiliza ikiwa ni pamoja na kupotea kwa wanyama, ukame na mabadiliko ya hali ya hewa, hivyo wamebadilisha njia zao za utafutaji wa kipato kutoka ukataji wa miti ili kutengeneza mkaa na badala yake kuunda vikundi mbalimbali vyenye shughuli mbalimbali za kujipatia kipato ambazo hazihusiani na uharibifu wa misitu. Mbali na hayo, Bwana Mwalami anaeleza kuwa misitu inapatwa na changamoto kama kuvamia misitu kutokana na udhaifu wa ulinzi katika njia mbalimbali za kuingilia misituni. Kuna umuhimu mkubwa kuwa serikali inabidi kutenga fedha kwa ajili ya ulinzi katika misitu, milango madhubuti na ulinzi dhabiti pamoja na nyenzo mbalimbali za ulinzi ni muhimu. Pia, kunahitajika msaada wa kifedha kutoka serikalini ili kudhibiti makundi hayo kuamua kuingia misituni kujikatia miti ili kupata kipato pindi wakwamapo. Kwa hiyo mkazo utolewe katika uendelezaji wa shughuli zingine za kujipatia kipato. 12 13

14 15

www.mamamisitu.org Kampeni ya Mama Misitu inapokea msaada toka Serikali ya Finland na Norway.