MOROGORO JARIDA LA. ISSN Toleo Na.4 Julai 2005 BODI ZA AFYA ZA WILAYA - SAUTI YA WANANCHI

Similar documents
BARAZA LA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA (Mawasiliano yawasilishwe kwa MSAJILI)

HAKIBulletin RAIS AMTEUA PROF. JUMA KUWA JAJI MKUU WA TANZANIA. Ndani: JARIDA LA MAHAKAMA YA TANZANIA

KITABU CHA MAFUNZO KWA WATOA DAWA KATIKA MADUKA YA DAWA MUHIMU

Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya

TAARIFA YA HISTORIA YA MKOA WA MWANZA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA

HOTUBA YA JAJI MKUU MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA SIKU YA SHERIA, DAR ES SALAAM, TAREHE 1 FEBRUARI, 2018

Ahadi za Serikali II. Zimekusanywa na HakiElimu Agosti 2007

John Lesson Eighteen Yohana Somo la Kumi na Nane

HAKIBulletin JAJI MKUU AWAASA WAHITIMU WA SHERIA KUJIENDELEZA KITAALUMA HALIUZWI! BENKI YA DUNIA USULUHISHI MUAFAKA MAHAKAMA MAWAKILI MAHAKAMA KUU,

UWAJIBIKAJI NDANI YA JESHI LA POLISI

MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA KIRINYAGA YA KATI MWAKA WA 2013

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF BOMAS OF KENYA

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF

AHMAD AL-RAYSUNI. SWAHILI VERSION idara ya Lugha na ukalimani ya Chuo Kikuu cha waislamu cha Morogoro. IIIT Mfululizo wa Vitabu kwa Muhtasari

TUMERITHI TUWARITHISHE

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

Ripoti ya Warsha Ya Washikadau Ihusuyo Mpango wa Uendeshaji wa Mazingira Wilayani Rufiji Iliyofanyika Utete Rufiji Juni 2000

February 9, 2017 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 16 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY

Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtukufu Mtume

Pre-Departure Program Swahili Unit 11 Worksheet UNIT 11: LOCATIVES, PREPOSITIONS, AND RELATIVE AND OBJECT INFIXES

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

BARUA YA TATU KWA SHEIKH UBAYD AL-JÂBIRĪ [AULIZWA SHEIKH UBAYD] NA Sheikh Sālim at-twawîl (hafidhahullāh)

Imâm Al-Albâni, Katika Kumsifu Mwanafunzi Wake, Muheshimiwa Sheikh Ali Hasan 1

JINA KAMILI CHEO SIMU YA OFISINI Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwandishi Mwendesha Ofisi

Kuishi Maisha Tele. Katika mwanzo wa mwaka mpya, Niliwapa changamoto

DINI JE, DINI NI MUHIMU?

Gazeti la kwanza la Kiislam kutolewa kwa lugha ya Kiswahili - mwaka 1936

Sura al-ahzaab. Tafsiri na Maelezo. Abdilahi Nassir

MALAIKA: WAJUMBE WA MUNGU

Ukoo Wake Na Kunasibika Kwake:

Khadija-tul-Kubra. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Published on Books on Islam and Muslims Al-Islam.org (

Zanzibar itafutika-mwanasheria

Bismillah ar-rahman ar-raheem SHAHADA 1 YALIYOMO

ZABURI 91 mstari 1. KJV-lite VERSES

NEW INTERNATIONAL VERSION

Published on Al-Islam.org ( Home > Mahari ya Damu > Mahari ya Damu. Mahari ya Damu

Ujasiri wa Kimaadili. Mojawapo ya madhumuni ya maisha ya duniani

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MANDERA CENTRAL CONSTITUENCY, HELD AT RHAMU

There is one God Mungu ni mmoja 1

HAKIKA YA AHMADIYYA. Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania

Ukweli Uliopotea - Sehemu Ya Tatu

Rainbow of Promise Journal

Tawasali. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags:

NEW LIFE IN CHRIST MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO

HALI YA UISLAMU. Maelezo ya kumsaidia Mkristo aufahamu Uislamu

Uwezo Kenya National Learning Assessment 2014

EVANGELISM FOR CHRIST UINJILISTI KWA AJILI YA KRISTO

YA AL HABBIB SAYYEID

2002 Version of the Basic Talk on "Using African Proverbs, Sayings, Idioms, Riddles, Stories, Fables, Play

Ukweli wa hadith ya karatasi

IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE.

Vitendawili Vya Swahili

VACATION BIBLE SCHOOL VBS. Newsletter. #Rebuilding through prayer, hard work & perseverance.

NGUO-NYINGI MKOTI: MWANZISHAJI WA MJI WA NGOJI (ANGOCHE)

Imam Mahdi katika Usunni Na Ushia

Kitabu Changu cha Mistari ya Biblia Swahili

NEW INTERNATIONAL VERSION

REPUBLIC OF KENYA COUNTY ASSEMBLY OF KILIFI THE HANSARD. Wednesday, 29 th March, 2017

TALKING ABOUT ONESELF TO ACT IN THE WORLD: A SWAHILI AUTOBIOGRAPHY (SHAABAN ROBERT, MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI

TAUS RETREAT NEWS LETTER # 1

Je, Umesikia Juu Ya Kanuni Nne Za Kiroho?

Toleo la kwanza: June, 2007 (Jamaadi Aakhar, 1428) Vitabu ii.

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS IJARA CONSTITUENCY AT IJARA BARAZA PARK

No. Book Name Category Type Price 1 AFYA MARIDHAWA -1 SWAHILI SUBSCRIPTION 2, AFYA NA UZIMA SWAHILI SUBSCRIPTION 8,500.00

2

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

NAIROBI CITY COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

In Search of Contact: Rhetorical Questions in the Communicative Frame of the Funeral Sermon

JUNE 4, Acts 2:1-12 and Offering...Pastor Maromy Samuel All Hail the Power of Jesus Name led by Haitian Congregation Worship Team

December 6, 2017 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 6 th December The House met at 9.30 a.m.

Ezra 3 Lessons Download or Read Online ebook ezra 3 lessons in PDF Format From The Best User Guide Database

MRADI WA METHALI (SANALASKUJA PROJEKTI)

Youth and Faith A collection of texts on the subject A collaborative Magazine Content

Yassarnal Quran English

WELCOME TO GOD S SERVICE A.C.K. ST. LUKE S PARISH UMOJA & TENA CHURCH QUOTE OF THE WEEK PRAYER OF THE DAY

MAOMBI YA QUR'AN TUKUFU SHEIKH MUZAFFAR AHMAD DURRANI

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

Mashairi ya Masaibu ya Karbala

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MANDERA CENTRAL CONSTITUENCY, HELD AT ELWAK

Change Your Destiny CONFERENCE

AND REACTION IN SWAHILI POETRY.

WELCOME TO GOD S SERVICE ACK ST. LUKE`S PARISH UMOJA Theme: Endeavoring to touch the heart of God, (Matt 25:40). Kuazimia kumpendeza Mungu

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

ATONEMENT IN AFRICAN PLURALISTIC CONTEXT: EXAMPLES FROM THE LUHYA OF WESTERN KENYA

2

INSTITUTIONALIZED IDENTITIES IN INFORMAL KISWAHILI SPEECH: ANALYSIS OF A DISPUTE BETWEEN TWO ADOLESCENTS

The Lord be with you And with your spirit

HOLY COMMUNION ACCORDING TO THE KENYAN RITE

Mission, Church and Tradition in Context

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

3 rd of 3 files Appendix and References

AFRIKA FOCUS, Vol.3, Nr.3-4, 1987, PP

MASHAIRI YA WAADHI "VERSES OF ADMONITION": the people of Mombasa rebuked by P J. L Frank! and Yahya Ali Omar

Cultural Considerations Tanzania Excursion

Fifty Years of the Union: the Relevance of Religion in the Union and Zanzibar Statehood Debate

A COLLECTION OF 100 MAKONDE (KENYA) PROVERBS AND WISE SAYINGS

I Peter 5:1-4 Good Leaders

Modern Swahili: the integration of Arabic culture into Swahili literature

Mother s Day. Fête des mères 母亲节 母の日 יום המשפחה म त द वस 母親節. Día de la Madre 어머니날. Ημέρα της μητέρας

Proofs Of A Conspiracy Against All The Religions And Governments: The Secret Meetings Of Freemasons, Illuminati And Reading Societies By John Robison

Transcription:

JARIDA LA MOROGORO ISSN 0856-9517 Toleo Na.4 Julai 2005 BODI ZA AFYA ZA WILAYA - SAUTI YA WANANCHI Halmashauri zote nchini zilitakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin William Mkapa, kuhakikisa kuwa ifikapo tarehe 31/12/2004 ziwe zimeansisha Bodi za Afya za Wilaya, ambazo zitasimamia huduma za afya katika Halmashauri husika. Bodi ya Afya ya Halmashauri ni chombo kilichoundwa chini ya sheria Na.7 na 8 (mamlaka za Wilaya na Miji) ya mwaka 1982, iliyoanzisha Mamlaka za Halmashauri za Mitaa. Bodi ina wajumbe 11, kati yao 7 wanachaguliwa na wananchi na 4 ni wataalam ambao huingia katika Bodi kwa nyadhifa zao. Wajumbe hao ni: Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii ya Halmashauri Mganga Mkuu wa Wilaya ambaye anakuwa Katibu wa Bodi Mwakilishi wa Watoa huduma binafsi kwa faida Mwakilishi wa watoa huduma binafsi bila faida Wajumbe 4 wanaotokana na watumiaji wa Huduma za Afya, kati yao wawili lazima wawe wanawake. Mwenyekiti wa Bodi atatokana na kundi hili. Mwakilishi toka Timu ya Uendeshaji ya Huduma za Afya ya Mkoa Wataalam wawili toka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, akiwemo: i. Afisa Mipango/Mchumi wa Wilaya ii. Mwakilishi toka Hospitali ya Wilaya Majukumu ya Bodi: Kifungu cha 86A na 52A cha sheria hii, kinatoa mamlaka kwa Halmashauri kuanzisha Mfuko wa Afya ya Jamii, ambao utakuwa unasimamiwa na Bodi. Majukumu mengine ya Bodi ni pamoja na:- 1. Kushirikiana na Timu ya Uendeshaji ya Wilaya kuhakikisha kuwa huduma Zinazotolewa ni za ubora wa hali ya juu. 2. Kupendekeza kwa Halmashauri watu wanaostahili kusamehewa kuchangia Mfuko wa Afya ya Jamii. 3. Kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko. Utekelezaji Ngazi ya Halmashauri: Hadi tarehe 31 Desemba 2004, kati ya Halmashauri zote 114 nchini, Halmashauri 49 tu zilikuwa zimeanzisha Bodi za Afya. Nyingine 109 zilikuwa zimeridhia kwa kupitisha Sheria Ndogo na Hati Rasmi ya kuanzisha Mfuko wa Afya ya Jamii. Jambo la kutia moyo ni kuwa, kati ya Bodi 49 zilizoanzishwa, 3 ni kutoka Morogoro, ambazo ni Halmashauri za Ulanga, Manispaa na Morogoro. Kati ya Halmashauri 109 zilizoridhia, 2 ni za Morogoro ambazo ni Kilosa

na Kilombero. Haya ni mafanikio makubwa kwa wananchi wa Morogoro. Hata hivyo, wilaya ya Kilosa ambayo ilikwisha anzisha Bodi tangu mwaka 1999, na kufanikiwa kukusanya zaidi ya Tshs. 72,000,000/- za Mfuko wa Afya ya Jamii, Bodi yake inatakiwa kuanzishwa upya, kwani ilianzishwa kinyume cha sheria, kwani:- 1. Mwenyekiti wa Bodi hiyo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii ya Halmashauri, hatua ambayo siyo sahihi. 2. Bodi ilianzishwa bila kupata Sheria Ndogo iliyosainiwa na Waziri mwenye dhamana, ambaye ni Waziri wa Serikali za Mitaa, kama inavyoagizwa na sheria. Majumuisho: Wakati taratibu za usimikaji upya wa Bodi ya Afya ya Kilosa zinakamilishwa, Halmashauri nyingine nchini zinakaribishwa kutembelea Mkoa wa Morogoro ili kujifunza utekelezaji wa Bodi za Afya na jinsi ya kusikiliza na kupokea Sauti ya Jamii na kiu ya wananchi ya kupata huduma bora za Afya. Bw. Mankambila, JCD Katibu wa Afya Morogoro BODI YA UHARIRI Mwenyekiti Bw. N. Masaoe Afisa Afya Mkoa Katibu Bi. C. Maro Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Wilaya Morogoro Msaidizi wa Katibu Bi. N. Ahmed Afisa Muuguzi Manispaa Morogoro Wajumbe Bw. J. Mankambila Katibu wa Afya Mkoa Dk. G. Mtey Mganga Mkuu Manispaa Morogoro Dk. O. Mbena Mganga wa Meno Wilaya Morogoro Bw. J. Bundu Afisa Afya Wilaya Kilosa Bw. D. Dia Katibu wa Afya Wilaya Kilombero Bw. B. Mbumbumbu Afisa Afya Wilaya Ulanga Bi. M. Tsuda Mshauri, MHP* Mshauri Mkuu Dk. M. Massi Mganga Mkuu Mkoa - Yaliyomo - o BODI ZA AFYA ZA WILAYA... 1 o TAHARIRI... 3 o BODI YA HUDUMA ZA AFYA MANISPAA... 4 o ZANA ZA KUANDAA MPANGO WA AFYA 5 o KIFUA KIKUU KILOSA... 6 o UTARATIBU WA USIMAMIZI KWA KANDA... 6 o CATOON... 8 Bw. N. Masaoe Bi. C. Maro Bi. N. Ahmed Mjumbe Mshiriki Dk. F. Fupi Kamati ya Ushauri Bw. H. Mohamed Mshauri, MHP* Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Bw. J. Mankambila Dk. G. Mtey Dk. O. Mbena *MHP:Mradi wa Afya Morogoro (Morogoro Health Project), JICA Bw. J. Bundu Bw. D. Dia Bw. B. Mbumbumbu 2

JARIDA LA AFYA MOROGORO Bw. N. Masaoe Mwenyekiti Bodi ya Uhariri Wasomaji wetu wapendwa, kwa niamba ya Bodi ya Uhariri wa hili jarida nawakaribisha kwa Toleo la Nne, ambayo ina habari za kipindi cha Julai 2004 hadi Juni 2005. Bodi inawashukuru wasomaji waliotuma habari za kuchapisha. Tunawataka radhi kwa kushindwa kuchapisha habari zote mlizo tuna. Tunawahakikishia kwamba habari ambazo hazikuchapishwa kwenye makala hii, zimehifadhiwa vizuri kwa matumizi ya makala zifuatazo. Aidha tunapongeza wasomaji waliotuma maoni kuhusu toleo la tatu, maoni yao yametumika kuboresha makala hii. Bodi inapenda kuarifu wasomaji wetu kwamba Bw. C. Kakwaya, Mjumbe wa Bodi ambaye pia alikuwa Katibu wa Afya Wilaya ya Kilombero, amehamishiwa Mkoa wa Dodoma kuwa Katibu wa Afya wa Mkoa. Nafasi yake imechukuliwa na Bw. Dia Alliy Dia, aliyekuwa Katibu wa Afya wa Mkoa wa Ruvuma. Bodi inamkaribisha Bw. D.A. Dia na kumpongeza Bw. C. Kakwaya kwa mchango wake katika vikao vya Bodi. Utoaji wa huduma za afya Mkoani Morogoro na Nchini kwa ujumla, umepiga hatua kubwa, pale ambapo wananchi wamewezeshwa Kisheria kusimamia hizi huduma. Halmashauri za Wilaya nne hapa mkoai ambazo ni Manispaa, Ulanga, Kilombero na Morogoro Vijijini, wamezindua Bodi na Kamati za huduma za afya. Bodi na kamati zilizotajwa husaidia kusimamia utoaji wa huduma kwa kusimamia maeneo yafuatayo:- Usimamizi mzuri wa huduma za afya Kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa Afya wa Jamii Kushiriki katika kupanga huduma za afya katika ngazi ya kituo cha huduma za afya Kutafuta/kubuni vyanzo mbadala vya mapato vya kuimarisha utoaji wa huduma za afya Tunaomba wasomaji wetu kuendelea kutoa maoni na habari za kuchapisha kwenye makala zinazofata. Bodi inawataka radhi wasomaji wetu kwamba kutokana na matatizo nje ya uwezo wetu, hatukuweza kuchapisha nakala hii kwa wakati uliopangwa. Bw. N. Masaoe Mwenyekiti Bodi ya Uhariri 3

UZINDUZI WA BODI YA HUDUMA ZA AFYA MANISPAA YA MOROGORO Kuanzishwa kwa Bodi ya Afya ya Manispaa na Kamati za Usimamizi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya katika Manispaa ya Morogoro kulifanywa kwa mujibu wa Sheria Na. 7 na 8 ya mwaka 1982 na sheria ndogo ya Manispaa (bylaw) kipengele na. 52A iliyotungwa mwaka 2002 inayolenga kutekeleza Maboresho katika Serikali za Mitaa (LGRP) na Mabadiliko katika Sekta ya Afya (HSR) yanayoendelea nchini. Uzinduzi wa Bodi ya Afya ulifanyika katika sherehe iliyofana mnamo tarehe 28/9/2004 baada ya mafunzo ya siku 3 kwa wajumbe wa Bodi na wale wa Kamati za Usimamizi yaliyotolewa na Wawezashaji kutoka Wizara ya Afya. Kama ilivyo katika sheria, uzinduzi huo ulifanywa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Mathew Sedoyeka na kuhudhuriwa pia na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mheshimiwa Francis E. Kayenzi, Naibu Meya Mheshimiwa Mohamed Lukwele, Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi wa Manispaa Bw. A.P. Mageka na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Ritha Lyamuya. Wakuu wa Idara na Watendaji wa Kata za Manispaa nao walishiriki. Uzinduzi wa Kamati za Usimamizi wa Vituo vya huduma za afya ulifanyika mwezi Februari 2005, hivyo kukamilisha zoezi la msingi la kukabidhi wananchi jukumu kubwa la kushiriki katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo na kusimamia utekelezaji wa mipango ya afya katika maeneo yao. Kamati zilizohusika ni za Vituo 3 vya Afya vya Sabasaba, Mafiga na Uhuru. Aidha Kamati 4 za Zahanati za Kingolwira, Towero, Mbete na Konga zilihusika katika uzinduzi huo na hivyo kufanya Vituo vyote vya Huduma za Afya vinavyomilikiwa na Halmashauri katika Manispaa ya Morogoro kuwa na Kamati za Usimamizi. Kwa mujibu wa sheria, uzinduzi wa Kamati za Usimamizi ulifanywa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro ambaye alifuatana na Wajumbe wa Bodi ya Afya, Mganga Mkuu na Maofisa wengine mbalimbali wa Manispaa ya Morogoro. Katika uzinduzi huo, Mstahiki Meya aliwapongeza wanakamati wote kwa kuchaguliwa kwao. Aliwaasa kuepuka misuguano na tofauti baina yao na kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kwa kujali matakwa ya wananchi wanaowawakilisha ili, kwa kupitia kwao, wananchi waweze kushiriki katika kupanga, kutekeleza, kusimamia, kufuatilia na kutoa maamuzi yanayowahusu ya maendeleo yao katika Sekta ya Afya. Aliwakumbusha pia kufanya kazi kwa kuzingatia yale waliyojifunza katika semina iliyofanyika mara baada ya kuchaguliwa kwao na kuonya kuwa Kamati sasa ndizo zitakazowajibika kwa huduma nzuri au mbaya za afya katika eneo lake. Aidha aliwaasa wananchi kuzipa Kamati hizi kila aina ya msaada na kuwakumbusha kuwa jukumu la Afya ni jukumu la kila mwananchi. Bw. E. Rugiga Mafiga RHC Morogoro Manispaa 4

ZANA ZA KUANDAA MPANGO WA AFYA Wilaya za Morogoro na Mvomero kama wilaya nyingine za Tanzania Bara huandaa mpango kamambe wa pamoja kwa kila mwaka. Ili kuandaa mpango kamambe wa pamoja ulio boreka Halmashauri huandaa mpango kwa kutumia zana bora za mpango zilizoendelezwa na NUMA zifuatazo: Madhara ya Magonjwa Kila mpango ni lazima uwe na udhibitisho wa takwimu sahihi za magonjwa ili kujua, ugonjwa gani unaoogoza. Taarifa hupatikana kwa kutumia mfumo wa ufuatiliaji idadi ya watu katika Wilaya (Sentinel District Demographic Surveillance System) ambao utafuata ngazi ya kaya kwa wahamiaji wote, waliozaliwa, vifo na sababu ya vifo. Matumizi ya Fedha za Afya Wilaya Zana hii husaidia halmashauri kugawa kwa usawa rasilimali, huku Halmashauri ikiainisha madhara ya magonjwa na mambo mengine kama vile Matibabu ya Magonjwa ya Watoto kwa Uwiano (IMCI), Ukimwi, n.k. Programu inayotumika ambayo ipo kwenye kompyuta inayofahamika kama Uhasibu wa Fedha za Afya Kiwilaya (District Health Accounts Matrix DHA). ilivyoelekezwa katika kabrasha la Mwongozo (Cost Centre or Level according to Prototype Documents). Sauti ya Jamii Kama mpango unavyohitaji uthibitisho wa takwimu endelevu za msingi, kutoka katika mfumo wenyewe pia matumizi ya malengo muhimu ambao hutegemea mtazamo toka Ngazi ya kijiji katika mpango mchakato ambao hutolewa na jamii kwa kushirikishwa katika vitendo na utafiti (Participatory Action Research PAR). Zana hizi hutumika kutambua mikakati ya misingi ya kijamii ambayo huhakiki matumizi na kuongeza ufanisi endelevu katika jamii unaofaa kiafya. Kwahiyo basi humpa mwananchi uwezo wa kuwa na sauti kwa yale yote yanayowahusu. Zana zilizotajwa hapo juu husaidia Halmashauri kugawa raslimali kwa kufuata uwiano wa magonjwa yanayoongoza kwa kuzingatia kipaumbele cha matatizo katika mpango kamambe wa mfuko wa pamoja, na hata kuonyesha matumizi ya fedha wakati wa utekelezaji kwa kuzingatia mgawo wa fedha hizo. Muundo wa Gharama Kiwilaya Zana hii hutumika kuchanganua matokeo ya gharama ya utekelezaji.hivyo zana husaidia katika ufanisi wa kiufundi kwa kuipa Timu ya Uendeshaji Huduma za Afya Wilaya ya Morogoro na Mvomero kutoa mrejesho wa mwaka kwa magonjwa, na gharama ya magonjwa kwa kila kituo cha tiba kama Dk. M. Omari Daktari wa Kinywa/Meno (W) CHMT-Mvomero 5

MUELEKEO WA HALI YA UGONJWA WA KIFUA KIKUU WILAYA YA KILOSA Wilaya ya Kilosa ni kubwa kuliko zote Mkoani Morogoro, ikiwa na wakazi 502,225 (Sensa ya 2002 ya watu). Wilaya hii ni ya pili kimkoa kwa wingi wa wagonjwa wa kifua kikuu waliotolewa taarifa. Mwaka 2004 ilikuwa na wagonjwa 712 wa aina zote za kifua kikuu. Manispaa ya Morogoro inaongoza kwa wingi wa wagonjwa wa kifua kikuu. Mwaka 2004 wagonjwa 1,277 walioripotiwa. Kuwepo wagonjwa wengi wilayani Kilosa kunaweza kusababishwa na mambo yafuatayo: Umaskini unaosababisha jamii waishi kwenye nyumba na lishe duni. Kiwango kikubwa cha maambukizo ya ukimwi. Wateja kuhamasika kufuata tiba mapema, hali inayosaidia ugunduzi wa wagonjwa mapema. Kuwepo rasilimali za kutosha za kugundua na kutibu kifua kikuu kikamilifu. Ugonjwa wa kifua kikuu cha mapafu husababishwa na bacteria aina ya Acid Fast Bacilli waitwao Mycobacterium tuberculosis. Aina nyingine ya hawa bacteria kama Mycobacterium bovis na Mycobacterium africanus husababisha kifua kikuu nje ya mapafu (Extra Pulmonary Tuberculosis). Bacteria wanaosababisha kifua kikuu cha mapafu huenezwa kwanjia ya hewa, mgonjwa anapokohoa, kupiga chafya ama anapozungumza bila kuchukua tahadhari. Kifua kikuu nje ya mapafu huenezwa kwa kula mazao yatokanayo na ngombe kama vile nyama ama maziwa yaliyochafuliwa na hawa bacteria. Hatua za kuzuia kifua kikuu ni pamoja na: Ugunduzi mapema wa wagonjwa pamoja na matibabu sahihi. Kuwapatia chanjo ya BCG watoto wote wanaozaliwa. Kuishi kwenye nyumba zenye mwanga wa kutosha na kuepuka msongamano. Kuwapatia lishe bora watoto chini ya miaka mitano na walioko katika hatari ya kuathirika. Kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa unavyoenea na mbinu za kujikinga. Ukaguzi endelevu wa nyama na maziwa, na kuhakikisha maziwa na bidhaa zake zinatakaswa (pasterurization). Hali ya wagonjwa wa kifua kikuu kwa miaka 5 ya nyuma imeonyeshwa kwa michoro hapa chini. IDADI YAWAGONJWANAVIFO 900 800 700 600 500 400 300 200 100 0 HALI YA UGONJWA NA VIFO MWAKA 2000-2004 00 00 01 01 02 02 03 03 04 04 MIAKA MIAKA 1 2 3 4 5 UGONJWA VIFO Bw. G. Mkoba Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma Kilosa UTARATIBU WA USIMAMIZI KWA KANDA Utaratibu wa kufanya Usimamizi kwa kanda (Integrated Management Cascade - IMC) unaboresha utoaji wa maamuzi wa haraka na ushirikishwaji wa watendaji wa ngazi za chini 6

kwa utekelezaji wa shughuli zilizomo katika Mpango wa Afya wa Wilaya na Mabadiliko katika Sekta ya Afya. Lengo Kuu la Utaratibu huu ni kuwezesha watendaji walio chini ya Ngazi ya Timu ya Uendeshaji ya Wilaya kutekeleza majukumu ya usambazaji wa vifaa, usimamizi, mafunzo, na kuboresha mawasiliano kati ya vituo vya Huduma na Ngazi ya wilaya. Katika hali ya kawaida ni vigumu kwa Timu ya Uendeshaji ya Wilaya kufanya usimamizi ipasavyo kwa vituo 98 vya Huduma kutokana na kutokuwa na muda na watumishi wa kutosha. Pamoja na kutekeleza mabadiliko katika Sekta ya Afya na kuundwa kwa Timu za Uendeshaji za Wilaya, mawasiliano na ushirikishwaji wa vituo vya ngazi ya chini ulikuwa duni. Ili kukabiliana na mapungufu hayo utaratibu wa usimamizi wa Kanda ulianzishwa mwaka 1998, ili kukasimu baadhi ya majukumu ya Timu ya uendeshaji kwa vituo vya Afya ili wasimamie Zahanati zilizopo chini yao. Juhudi za kuimarisha utaratibu huu ni pamoja na kufunga simu za upepo, kutoa Pikipiki, Magari ya wagonjwa na kuwepo kwa watumishi wenye ujuzi. Miongoni mwa majukumu ya Timu ya uendeshaji yaliyo kasimiwa kwa vituo vya Afya ni pamoja na:- Usimamizi na mafunzo ya watumishi juu ya uendeshaji wa huduma za Afya Uagizaji na usambazaji wa vifaa vya tiba, dawa na vyandarua vyenye viuatilifu Ukarabati wa vituo vya Huduma na nyumba za watumishi, kwa mpango wa kutumia nguvu za wananchi Ukusanyaji wa vyandarua vyenye uatilifu kwa ajili ya mauzo, na taarifa za Uendeshaji wa Huduma za Afya Kushughulikia kupeleka wagonjwa wa rufaa katika ngazi ya juu kwa matibabu zaidi Uchambuzi wa takwimu za MTUHA ngazi ya kituo Kushauriana na wilaya juu ya masuali ya kijamii, kupanga ratiba ya likizo na mgawanyo wa watumishi Manufaa ya Mpango huu ni:- Uanzishaji wa Maabara za Kanda ili kuhudumia zahanati zao Kushirikisha Kanda katika kuboresha kupanga Mpango wa Hudumza za Afya Usimamizi wa fedha baada ya kuanzishwa kwa Bodi ya Afya wilaya na Kamati za Afya za Kata na Vituo Utekelezaji wa Kampeni za kitaifa kwa Vitamin A, Surua, na Siku za Chanjo Kutafuta rasilimali kutoka jamii Ili kuimarisha na kufanya Mpango huu kuwa endelevu, yafuatayo ni muhimu yazingatiwe:- Kuwajengea uwezo wa usimamizi Wakuu wa Kanda za Usimamizi Kuimarisha uhamasishaji wa Utaratibu huu ili ueleweke zaidi Kutoa vifaa vya mawasiliano kama simu za upepo ili kuimarisha mawa siliano na rufaa ya wagonjwa Mafanikio ya Mpango huu katika Halmashauri ya Morogoro yamepokelewa vizuri katika ngazi zote na yamezivutia Halmashauri nyingine ambazo zimekwisha anza kuja kujifunza toka ndani na nje ya Mkoa wa Morogoro, na tunazidi kuwakaribisha. CHMT Wilaya ya Morogoro 7

CATOON UMUHIMU WA KUCHANGIA HUDUMA ZA AFYA Mtungaji/Mchoraji: Bw. J. Bundu Kwanini hutaki kujiunga na mfuko wa afya ya jamii? Mbona watoto wangu wanatibiwa Je wewe ukiugua utajigeuza mtoto????????? Tunawaomba wasomaji wetu watoe maoni yao kuhusu jina litakalofaa kuitwa jarida hili. Aidha tunaomba wasomaji wetu watume makala za kuchapisha kwenye toleo la Desemba 2005: zenye maneno yasiyozidi 400, zinazohusiana na afya ama maoni kuhusu huduma za afya zinazotolewa katika mkoa wa Morogoro. Makala au barua za maoni zitumwe kwa anuani zifuatazo:- Mhariri, Jarida la Afya Morogoro S.L.P. 110, MOROGORO au, S.L.P. 1193, MOROGORO, FAX 023-4148 au, Yapelekwe kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya husika:- S.L.P. 166, Morogoro Manispaa S.L.P. 1862, Morogoro S.L.P. 14, Kilosa S.L.P. 47, Ifakara, Kilombero S.L.P. 4, Mahenge, Ulanga LIMECHAPISHWA NA BODI YA UHARIRI JARIDA LA AFYA MOROGORO S. L. P. 110, MOROGORO 8