NGUO-NYINGI MKOTI: MWANZISHAJI WA MJI WA NGOJI (ANGOCHE)

Similar documents
John Lesson Eighteen Yohana Somo la Kumi na Nane

Pre-Departure Program Swahili Unit 11 Worksheet UNIT 11: LOCATIVES, PREPOSITIONS, AND RELATIVE AND OBJECT INFIXES

NEW INTERNATIONAL VERSION

BARAZA LA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA (Mawasiliano yawasilishwe kwa MSAJILI)

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF BOMAS OF KENYA

MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA KIRINYAGA YA KATI MWAKA WA 2013

There is one God Mungu ni mmoja 1

2002 Version of the Basic Talk on "Using African Proverbs, Sayings, Idioms, Riddles, Stories, Fables, Play

YA AL HABBIB SAYYEID

Dhana ya Ndoa ya Mitala na Ndoa za Mtukufu Mtume

Khadija-tul-Kubra. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Published on Books on Islam and Muslims Al-Islam.org (

BARUA YA TATU KWA SHEIKH UBAYD AL-JÂBIRĪ [AULIZWA SHEIKH UBAYD] NA Sheikh Sālim at-twawîl (hafidhahullāh)

MALAIKA: WAJUMBE WA MUNGU

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

Sura al-ahzaab. Tafsiri na Maelezo. Abdilahi Nassir

Published on Al-Islam.org ( Home > Mahari ya Damu > Mahari ya Damu. Mahari ya Damu

HAKIKA YA AHMADIYYA. Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania

IFAHAMU BIBLIA KATIKA UBORA WAKE.

Imâm Al-Albâni, Katika Kumsifu Mwanafunzi Wake, Muheshimiwa Sheikh Ali Hasan 1

ZABURI 91 mstari 1. KJV-lite VERSES

Ukweli Uliopotea - Sehemu Ya Tatu

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) NATIONAL CONSTITUTIONAL CONFERENCE (NCC) VERBATIM REPORT OF

Ukweli wa hadith ya karatasi

DINI JE, DINI NI MUHIMU?

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS, MANDERA CENTRAL CONSTITUENCY, HELD AT RHAMU

Kuishi Maisha Tele. Katika mwanzo wa mwaka mpya, Niliwapa changamoto

Gazeti la kwanza la Kiislam kutolewa kwa lugha ya Kiswahili - mwaka 1936

NEW INTERNATIONAL VERSION

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

HALI YA UISLAMU. Maelezo ya kumsaidia Mkristo aufahamu Uislamu

Tawasali. Author(s): Publisher(s): Translator(s): Category: Topic Tags:

Imam Mahdi katika Usunni Na Ushia

Ukoo Wake Na Kunasibika Kwake:

Zanzibar itafutika-mwanasheria

NEW LIFE IN CHRIST MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO

Kitabu Changu cha Mistari ya Biblia Swahili

Rainbow of Promise Journal

Bismillah ar-rahman ar-raheem SHAHADA 1 YALIYOMO

Toleo la kwanza: June, 2007 (Jamaadi Aakhar, 1428) Vitabu ii.

Ujasiri wa Kimaadili. Mojawapo ya madhumuni ya maisha ya duniani

EVANGELISM FOR CHRIST UINJILISTI KWA AJILI YA KRISTO

February 9, 2017 COUNTY ASSEMBLY DEBATES 16 MOMBASA COUNTY ASSEMBLY

Uwezo Kenya National Learning Assessment 2014

AHMAD AL-RAYSUNI. SWAHILI VERSION idara ya Lugha na ukalimani ya Chuo Kikuu cha waislamu cha Morogoro. IIIT Mfululizo wa Vitabu kwa Muhtasari

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC) VERBATIM REPORT OF CONSTITUENCY PUBLIC HEARINGS IJARA CONSTITUENCY AT IJARA BARAZA PARK

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

2

In Search of Contact: Rhetorical Questions in the Communicative Frame of the Funeral Sermon

TALKING ABOUT ONESELF TO ACT IN THE WORLD: A SWAHILI AUTOBIOGRAPHY (SHAABAN ROBERT, MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI

TUMERITHI TUWARITHISHE

MRADI WA METHALI (SANALASKUJA PROJEKTI)

JUNE 4, Acts 2:1-12 and Offering...Pastor Maromy Samuel All Hail the Power of Jesus Name led by Haitian Congregation Worship Team

Vitendawili Vya Swahili

Je, Umesikia Juu Ya Kanuni Nne Za Kiroho?

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

WELCOME TO GOD S SERVICE A.C.K. ST. LUKE S PARISH UMOJA & TENA CHURCH QUOTE OF THE WEEK PRAYER OF THE DAY

NAIROBI CITY COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

MOROGORO JARIDA LA. ISSN Toleo Na.4 Julai 2005 BODI ZA AFYA ZA WILAYA - SAUTI YA WANANCHI

The Lord be with you And with your spirit

No. Book Name Category Type Price 1 AFYA MARIDHAWA -1 SWAHILI SUBSCRIPTION 2, AFYA NA UZIMA SWAHILI SUBSCRIPTION 8,500.00

CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISSION (CKRC)

HAKIBulletin RAIS AMTEUA PROF. JUMA KUWA JAJI MKUU WA TANZANIA. Ndani: JARIDA LA MAHAKAMA YA TANZANIA

Ahadi za Serikali II. Zimekusanywa na HakiElimu Agosti 2007

Ezra 3 Lessons Download or Read Online ebook ezra 3 lessons in PDF Format From The Best User Guide Database

REPUBLIC OF KENYA COUNTY ASSEMBLY OF KILIFI THE HANSARD. Wednesday, 29 th March, 2017

Cultural Considerations Tanzania Excursion

HAKIBulletin JAJI MKUU AWAASA WAHITIMU WA SHERIA KUJIENDELEZA KITAALUMA HALIUZWI! BENKI YA DUNIA USULUHISHI MUAFAKA MAHAKAMA MAWAKILI MAHAKAMA KUU,

Mashairi ya Masaibu ya Karbala

HOTUBA YA JAJI MKUU MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA SIKU YA SHERIA, DAR ES SALAAM, TAREHE 1 FEBRUARI, 2018

HOLY COMMUNION ACCORDING TO THE KENYAN RITE

UWAJIBIKAJI NDANI YA JESHI LA POLISI

Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya

WELCOME TO GOD S SERVICE ACK ST. LUKE`S PARISH UMOJA Theme: Endeavoring to touch the heart of God, (Matt 25:40). Kuazimia kumpendeza Mungu

TAARIFA YA HISTORIA YA MKOA WA MWANZA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA

December 6, 2017 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 6 th December The House met at 9.30 a.m.

MANIFESTATION OF COMMON MAN LANGUAGE IN EPIC POEMS: A CASE STUDY OF UTENDI WA SIRI LI ASRARI

The history of Zaire as told and painted by Tshibumba Kanda Matulu in conversation with Johannes Fabian

Yassarnal Quran English

The Nineteenth Century: Islam

TAUS RETREAT NEWS LETTER # 1

Eastern City-States and Empires of Africa

MAOMBI YA QUR'AN TUKUFU SHEIKH MUZAFFAR AHMAD DURRANI

Ripoti ya Warsha Ya Washikadau Ihusuyo Mpango wa Uendeshaji wa Mazingira Wilayani Rufiji Iliyofanyika Utete Rufiji Juni 2000

Learning by Ear Unce upon a time... in Africa Episode 3: TRADE IN AFRICA. Author: Marta Barroso Editors: Maja Braun, Jan-Philipp Scholz CHARACTERS:

(Cell) (Cell) (Cell) (Landline) (Cell)

VACATION BIBLE SCHOOL VBS. Newsletter. #Rebuilding through prayer, hard work & perseverance.

Youth and Faith A collection of texts on the subject A collaborative Magazine Content

Where is Africa? 2. What is African heritage? 3. What is the African heritage in the Bible? 6. What are African ways of worship?

KITABU CHA MAFUNZO KWA WATOA DAWA KATIKA MADUKA YA DAWA MUHIMU

History. Mid-19 th century Omani residences in Kilwa Kivinje, Tanzania, with original carved doors, balconies and window shutters

MASHAIRI YA WAADHI "VERSES OF ADMONITION": the people of Mombasa rebuked by P J. L Frank! and Yahya Ali Omar

AND REACTION IN SWAHILI POETRY.

Muslims in Kenyan Politics

Indian Ocean Trade. Height C.E.

ATONEMENT IN AFRICAN PLURALISTIC CONTEXT: EXAMPLES FROM THE LUHYA OF WESTERN KENYA

Empires develop in northern, western, and southern Africa. Trade helps spread Islam and makes some African empires very wealthy.

North and Central African Societies

AFRIKA FOCUS, Vol.3, Nr.3-4, 1987, PP

GENERAL CONGREGATION 36 rome // 2016

World History: Patterns of Interaction

Transcription:

AAP 60 (1999). 121-130 NGUO-NYINGI MKOTI: MWANZISHAJI WA MJI WA NGOJI (ANGOCHE) THILO C.. SCHADEBERG The title of this paper gives three variants of what historically is the same name: Koti = the present-day indigenous name of Koti Island; Ngoji = the older form of the same name; Angoche = the official name of the town, adapted from the name of the AKoti people EKoti is the language of Angoche, a town on the coast of Nampula Province, in Mozambique EKoti is in most respects very similar to the neighbouring coastal varieties of Makhuwa, but it also has many lexical and morphological items that are derived from Swahili My colleague F. U Mucanheia, co-author of our forthcoming grammar ofekoti, has recorded a story about the origin of Koti Island and its people. In the present paper, I summarize the text of this oral tradition, and I compar e it to the dynastic traditions from Angoche and to those found in the Kilwa chronicle, pointing out differences but also establishing links Mozam6ique Chinda Maputo!nhambana Quelimane Itu!ian Ocean Hapo zamani, mwishoni mwa krune ya kumi na tano, wakati Wareno walipotokea katika ufukwe wa Afrika ya Mashruiki, kulikuwa na miji miwili ya Waswahili iliyokuwa na enzi na utajiri zaidi kuliko miji mingine: mji wa Mombasa na mji wa Kilwa.. Bandrui ya Mombasa ilikuwa bandari kuu ya biashara baina ya Aflika ya Mashariki na nchi za ng'ambo, hasa Uruabuni na Bara ya Hindi.. Kila mwaka pepo za Kaskazi ziliyaleta majahazi, na baada ya kufanya biashara zao, pepo za Kusi ziliyarudisha.. Majahazi hayo yalileta nguo na shanga, na kupeleka dhahabu, pembe ya ndovu, ngozi, boriti, na vitu vingine Je, vitu hivyo vilitoka wapi? Vingine vilitoka kruibu na Mombasa, lakini vingi vingine vilitoka sehemu nyingine za bara la Afiika, kwa sababu sehemu zilizo kruibu na Mombasa hazikutoa vi tu hivyo kwa wingi. Sehemu kubwa ya bidhaa hizo zilitoka sehemu runbazo Ieo ziko katika nchi za

122 THILO C SCHADEBERG Tanzania, Msumbiji, Malawi, na Zimbabwe Misafara ilileta bidhaa hizo kutoka bara mpaka kwenye bandari mbalimbali za pwani. Lakini Kilwa ilikuwa mji kuu wa biashrua hizo zote Wafanyabiashrua wa Kilwa walinunua vitu kutoka brua na kutoka bandrui nyingine kusini, na kuziuza au kuzileta hadi Mombasa na mahali pengine. Kilwa ilikuwa kruna ni mji mkuu wa bandrui zote upande wa kusini hadi Sofala Mmojawapo kati ya miji-bandrui hiyo iliyoitegemea Kilwa, u1ikuwa ni mji wa Angoche "Angoche" m pna la kisasa la mji, ambao ni mji mkuu wa wilaya, katika mkoa wa Nampula, katika nchi ya Msumbiji Jina la zrunani lilikuwa ni "Ngoji" Bw H. E. O'Neill, Balozi wa Uingereza huko Msumbiji, aliyezuru sehemu hizo za Msumbiji mwaka wa 1882, aliuita mji huo "Angoche", lakini lugha ya mji huo aliiita "Ki-Ngoji".. Matrunshi haya yanafanana na matrunshi ya Kiswahili Katika matrunshi ya Wamakhuwa wanaoishi pande zote za mji wa Angoche, [ngo] hutamkwa [ko], na [ji] hutamkwa [!i] - kama lahaja za kaskazini: [ngia ya nji kwa thi], au "njia ya chini ya nchi".. Wenyeji wa Angoche runbao Ieo hutumia matamshi hayo, wanajiita "AKoti", na lugha yao wanaiita "EKoti". Lakini mane no "Koti" na "Ngoji" yana asili moja.. "Angoche" ni jina la mji kwa lugha rasmi, yaani Kireno; neno hilo vilevile linatokana na neno "Angoji", yaani "watu wa Ngoji".. Siku hizi, "Koti" ni jina la kisiwa, isipokuwa Wakoti wenyewe wanaona kuwa kila kijiji kisiwani ni kama kisiwa peke yake Wanafikiri hivyo kwa sababu huwezi kutembea kwa miguu kutoka kijiji kimoja mpaka kingine, inakubidi usafiri kwa chombo Mji wenyewe, wenyeji huuita "Parapatho", neno ambalo hasa ni jina la kilima katikati ya mji wa zamani Mufai 1 Thamoole 2 Phuuli 3 Wiikuri (lnguri) 4 Mambaasa 5 Nyaakupwa Mpamefa 6 Mitthupani 7 Mshelele 8 Kathamweyo 9 Mlukutthu 10 Khiluwa 11 Mitthepeni 12 Maziwani 13 Yaarupa 14 Kalikhulu 'lv[{jtovoni Quinga 8 0 5 10

MWANZISHAJI WA MJI WA NGOJI (ANGOCHE) 123 Mreno Duarte Barbosa aliandika wasifu wa mji wa Angoche katika mwaka wa 1517 au 1518 1 Indo ha ha diante leyxando-se este Cvama ha cento corenta legoas delle, ha ha longvo da costa, estd hva mvy grande pouoaram de Movros que chamaom Amgoya que tern Rei sabre si Uiuem nella mvytos mercadores qve trataom em ovro, e em marfim, em panos de seda e algodam, e contas de Cambaya; assy coma sohiaom de fazer has de (:ofala has qvaes mercadorias /he trazem has Movros de (:ofala, de Mombara. de Melynde, e Qviloa, em hvvs nauios mvyto peqvenos escondidamente dos nossos nauios, de maneira qve daly leutio mvy gram soma de marfim, e mvyto ovro, neste mesa lvgar Damgoya ha mvyto mantimento, milho, arroz, e mvitas carnes, a gente delle saom homeins pretos, bafos, Mbali zaidi, kutokea mto huo wa Kwama na kuambaa pwani kwa "1egoas" 140 2 ; kuna mji mkubwa sana wa Waislamu 3, wanaouita Amgoya na ulio na mfalme wake Mjini humo mnakaa matajiri ambao biashma yao ni dhahabu, pembe za ndovu, hmiri, nguo za pamba na shanga za Kambay, kama wafanyavyo wafanya-biashara wa Sofala Waislamu wa Sofala, Mombasa, Malindi na Kilwa husafirisha bidhaa hizo kwa vyombo vidogo-vidogo ili visitambuliwe na majahazi yetu. Hivyo huchukua kiasi kikubwa cha pembe, na dhahabu nyingi; katika mji huo wa Amgoya kuna vyakula vingi mno kama mhindi 4, mchele na aina mbalimbali za nyama Wenyeji wengine ni weusi, na wengine ni wa kahawia; andaom nvvs da cinta pera cima, della pera baixo se cob rem corn panos dalgodam e seda, e trazem outros panos sobrarados ha maneira decapas, deles fotas em has caberas, outros trazem huas carapuras de quartos de pano de seda, hawavai kitu sehemu yajuu ya kiwiliwili, na sehemu ya chini huvaa nguo za hmiri na za pamba, terra huvaa nguo za kukimjwa mabegani zinazofanana najoho; vichwani wengine huvaa vilemba, na wengine huvaa kofia zilizoshonwa kwa vitambaa vya miraba minne vya hariri. 1 Kitabu chaduarte Barbosa kilipigwa chapa katika mwaka wa 1812 na kutafsiriwa kwa Kiingereza na Dames ( 1918) Sehemu za tafsiri hiyo zimepigwa chapa tena na Freeman-Grenville (I 966) 2 Mto wa Kwama ni mkono fulani wa delta ya Zambezi, /egua 40 kutokea mji wa Sofala kuelekea kaskazini Katika karne ya 16, Wareno walikadiria /egua I = kilomita 6.2 hadi 6 7 Kwa hivyo, /egua 140 zingekuwa takriban kilomita 900, na /egua 180 zingekuwa takriban km 1160. Kwa kweli, umbali toka Sotala mpaka Angoche si zaidi ya km 720 Nimetafsiii neno la Kireno "Mouros" kama "Waislamu" Wakati kitabu hicho kilipoandikwa, Wareno walitumia neno hila kuhusu Waafrika waliokuwa Waislamu lakini sio Waarabu Namna nyingine ya kutafsiri 3 neno hilo ingekuwa ni "Waswahili" 4 Dames (na Freeman-Grenville) wanatafsiri milho "millet"

124 THILO C. SCHADEBERG falaom ha lingoa natural da terra que he dos Gentios, alguns delesfalaom arauia. Estes Mouros has uezes estaom ha obediencia de elrei N Sr., outras uezes estaom aleuantados par estarem apartados das nosas fortalezas Wanasema lugha ya kienyeji ya nchi, yaani lugha ya makafiri, lakini wako wanaosema Kiambu Pengine Waislamu hao humtii Mfalme mtawala wetu, lakini wakati mwingine, wakiwa mbali na ngome zetu, huasi. Wataalamu wa historia ya Aflika ya Mashariki wanafikiii kwamba usultani wa Angoche ulianzishwa miaka michache tu kabla ya kufika kwa Wareno, yaani 1498 Kufuatana na mapokeo ya mdomo mji wa Angoche ulianzishwa na wahamiaji au wakimbizi kutoka Kilwa, lakini hao hawakuwa Waislamu wa kwanza kuishi sehemu ya Angoche 5 Viongozi wa wahamiaji kutoka Kilwa walikuwa Musa na Hasani Musa akiwa ni Sultani wa Kisiwa cha Msumbiji, alitawala mji huo wakati Mreno Vasco da Gama alipofika mwaka wa 1498.. Hasani akaendelea, akawa ni Sultani wa Quelimane (tamka: kilimani) Sultani Hasani akafia baharini alipokuwa akisafiri kuelekea mji wa Msumbiji, akazikwa katika kisiwa kidogo karibu na Angoche.. Kisiwa hicho kinaitwa Kisiwa cha Mafamedl, lakini wengine bado hukiita Kisiwa cha Sultan! Hasani. Baadaye Sultani Musa akaja kusali kwenye kaburi la rafiki yake Hasani Akaona Angoche inafaa kuliko Quelimane, akamweka Xosa, mwana wa Hasani, kuwa Sultani wa Angoche Sultani Xosa akakaa Koti kisiwani, katika kijiji cha Mshelele. Wakati ule kulikuwa na vmugu nyingi katika mji wa Kilwa; Kilwa ilianza kupoteza nguvu zake, tena biashara yake ya dhahabu kutoka Sofala ilianza kupungua Mambo hayo yalifanya miji mingine kusitawi, mmojawapo ulikuwa ni Angoche Wakati wa enzi ya Kilwa, Angoche ilikuwa ni mji mdogo tu; nguvu ya Kilwa ilipofifia, hasa baada ya kubomolewa kwake na Wareno (1505), mji wa Angoche ulianza kusitawi Wareno walijaribu kutamalaki biashara yote ya bahari, hasa biashara ya dhahabu. Kwa hiyo, anavyotueleza Duarte Barbosa, wenyeji walianza kutumia njia nyingine kwa biashara yao: jahazi ndogo ndogo, na bandari nyingine za miji midogo, mojawapo ni Angoche Basi, tangu miaka michache iliyopita nimekuwa nikifanya uchunguzi wa lugha ya Kikoti (EKoti), pamoja na Bwana Francisco Ussene Mucanheia, ambaye alikuwa akisoma isimu ya lugha katika Chuo Kikuu cha Eduardo Mondlane huko Maputo, Msumbiji Yeye ni mwenyeji wa Angoche, na msemaji wa lugha mbili za wilaya hiyo, yaani Kikoti na Kinlai, ambayo ni lahaja ya Kimakhuwa. Mwakajuzi (1997), Bwana Mucanheia alirekodi hadithi ya mapokeo juu ya asili ya visiwa vya Koti na watu wake.. Basi, nisimulie hadithi hiyo kwa kifupi: Terezento Roopa alikuwa ni mtoto wa Kikoti. Alipopata umri wa miaka ishirini, alimwendea babake na kumwambia "Baba, nimekua, nataka kusafiri Kwa hiyo, nataka uninunulie nguo." 5 Iaz. Newitt 1972 na Lupi 1907 6 Mafamed ni matamshi ya zamani ya Kireno ya jina la Mtume Muhammadi

MWANZISHAJI WA MJI WA NGOJI (ANGOCHE) 125 Basi, babaake alikwenda dukani, akanunua nguo. Kwanza alinunua nguo ya kamafleji, iliyovaliwa na askari katika vita vya ukoloni, lakini Terezento Roopa alipovaa ikapasuka tu. Baadaye babake akanunua nguo ya kaki, halafu nguo ya mpira wa gari na wa lori, lakini hazikufaa. Mwishowe akanunua mpira wa trekta, na nguo zikashonwa kwa kumfaa Terezento Roopa Baadaye Terezento Roopa aliomba jimbo, birika na mkoba wa :;afari.. Akapewa fimbo ya chuma inayotwaliwa na watu elfu, akashonewa mkoba unamoingia mikate elfu, akaletewa birika la!ita elfu za maji. Basi, akafunga safari. Akamkuta mwanamke mzee akitwanga makaa. Akamwamkia. Yule mzee akamwambia "Twanga makaa haya, halafu nitakujibu." Alipomaliza kutwanga, mzee alimwuliza "Unataka kujua nini?" Aka:;ema "Bibi, nani ni mwenye nguvu katika nchi hii?" Naye mzee akauma. "Pole, mwanangu. Shika njia hii, utamkuta mtu mwenye nguvu :;ana Ukitaka kupigana, pig ana naye. " Akaenda, akamkuta mtu ambaye alikuwa akitumia mbuyu kama mswaki. Wakapigana, Terezento Roopa akashinda, akamweka mfukoni, akasema "Wewe ni wa kwanza" Basi, akaendelea, akamkuta mzee mwingine aliyekuwa akitwanga makaa, akamuuliza juu ya mwenye nguvu wa nchi, akaambiwa, akamkuta. Mwenye nguvu huyo alitumia mibuyu kama mite go, Terezento Roopa akamshinda, akamweka mfukoni, akauma "Wewe ni wa pili.. " Na hivyo-hivyo mara ya tatu, akam:;hinda mtu aliyetumia mwamba kama ni mpira, akamshinda, akamweka mfukoni, akasema. "Wewe ni wa tatu " Akaendelea, akaendelea, akakuta nyumba, akasema "Nimefika." Akamweka mwanawe wa kwanza katika nyumba, akamwambia. "Mimi nitakwenda mashambani. Wewe ukae, utengeneze chai, unywe, weka chai yangu katika chupa ya chai uniletee. "Akaondoka Akajika Nankontta, mwenyeji wa nyumba. Akauliza "Anayetoa mo:;hi nyumbani mwangu ni nani?" Akajibiwa "Ndimi, mwana wa Terezento Roopa." Nankontta alisema. "Terezento Roopa ni nani? Si ndugu yangu, si mjomba wangu, si jamaa yangul" Basi akampiga mwana wa kwanza, naye akaruka, akaangukia shambani alipolima Terezento Roopa, akampa habari. Basi, hivyo-hivyo wakapigwa watoto wengine wawili wa Terezento Roopa. Mwishowe Nankontta alikutana na Terezento Roopa. Wakapigana Hay a, tuangalie mistari ya mwisho ya hadithi ya Terezento Roopa kw a lugha mbili, Kikoti na Kiswahili: Khuta, khupiiwa Terezento Roopa, khuvava khulawa akwela okhu, naani, Mitthupani. Khoowelela khuta Khupiiwa Nankontta, khuvava mpakha Matakaaxkare, Akafika Terezento Roopa, akapigwa, akaruka, akaanguka, wapi, Mittuphani. Akaogelea akaja.. Akapigwa Nankontta, akaruka mpaka Bukini,

126 THILO C SCHADEBERG khulawa akwela ottuukho, khoowelela khuta. N'uuta khupiiwa Terezento Roopa, khuvava khulawa akwela Kheleleni Khbowelela khuta. Khupiiwa Nankontta, khuvava khulawa akwela okhu, naani, Kalikhulu. Attaaphale aari okwelaa-vo Nankontta na Terezento Roopa khusala ziiya-mo naani, visura visura, visura epile mwinoonaa-zo, yaari viittha ya Terezento Roopa na Nankontta. Terezento Roopa aari nsimaana w'eekoti, Nankontta aari nsimaana w'eemakhuwa. Epo zaari opattikhana miili novisento. xkensi Leelo apha kinttakhulaa-ye ti-miyo, Asumaani Luzakeero Laasu, naturale te Nlikiwa, lokalitaate te Pweela, Namithoora, Angoxe akaanguka huko, akaogelea akaja Akapigwa Terezento Roopa, akaruka, akaanguka Kheleleni Akaogelea akaja. Akapigwa Nankontta, akaruka, akaanguka, wapi, Kalikhulu.. Popote walipoanguka Nankontta na Terezento Roopa pakawa nini.., visiwa... visiwa, visiwa mnavyoviona, viko [kw a sababu ya] vita vya Terezento Roopa na Nankontta. Terezento Roopa alikuwa mtoto wa Kingoji, Nankontta alikuwa mtoto wa Kimakhuwa. Mambo hayo yote yalitokea mwaka elf\.! moja mia tisa na.. nime-forget. Leo hapa anayetoa habari hii ndimi, Asumaani Luzakeero Laasu, mwenyeji wa Mlikiwa, Localidade Pweela, Namithoora, Angoche Ingawa habmi hii inasimuliwa kwa namna ya kisasa na kw a ucheshi, kiini chake ni cha zamani. Tuangalie majina Jina la shujaa Mkoti, Terezento Roopa, ni la Kireno, na maana yake ni 'nguo mia tatu' (Mpaka sasa hatujafaulu kupata jina lake kwa kienyeji.) Jina la adui au mpinzani wa Terezento Roopa, Nankontta, lina maana yake vile-vile. Neno hilo ni Kimakhuwa, maana yake ni 'mwenye msuli' Kwa namna hii, kila mmoja wa mashujaa hao ana jina mnbalo ni kmna dalili ya kabila lake: Mkoti mnevaa shati na kaptura, yaani nguo za kushonwa, Mmakhuwa amevaa msuli Jina la "Nguo Mia Tatu" Jinaonyeshajambo jingine Waandishi wa zmnani wa Kizungu na wa Kimabu wakizungumzia biashma ya pwani ya Afiika ya Mashmiki, kila mm a bidhaa za kwanza wanazozitaja ni dhahabu na pembe za ndovu, sababu hizo ndizo walizozitamani. Lakini wenyeji wa bara walizozitamani ni nguo. Tena, inafaa kufahmnu maana ya birika (pirikha). Si mtu yeyote anayechukua biiika akienda safari, ni Mwislamu anayeihitaji kw a kutawadha (au kujiosha) kabla ya kusali.

MWANZISHATI W A MJI W A NGOJI (ANGOCHE) 127 Je, habari hizo kutoka 11lii wa mbali, huko Msumbiji, kwa vipi zinahusu mambo ya lugha, utamaduni na historia ya W aswahili? Jibu langu ni kwamba shujaa huyo Terezento Roopa, Mkoti wa kwanza, alikuwa ni Mswahili kutoka Kilwa.. Habari za uanzishaji wa Kilwa Kisiwani zinalitaja jina la Sultani wa kwanza, naye alikuwa akiitwa "Nguo Nyingi".. "Nguo Nyingi" na "Nguo Mia Tatu"- m[\jina haya bila shaka yanahusiana. Tutazame habari za uanzishaji wa Kilwa Kisiwani zilivyosimuliwa na kuandikiwa kwa Kiarabu katika karne ya 16 7 Historians have said, amongst other assertions, that the first man to come to Kilwa came in the following way. There arrived a ship in which there were people who claimed to have come from Shiraz in the land of the Persians. It is said there were seven ships thefir;st stopped at Mandakha, the second at Shaugu, the third at a town called Yanbu, thefourth at Mombasa; the fifth at the Green Island [Pemba], the sixth at the land ofkilwa, and the seventh at Hanzuan They say that all the masters of these [first] six ships were brother:s, and that the one who went to the town of Hanzuan was their father. God alone knows all the truth'[...} When they arrived in the ship that went to Kilwa, they found it was an island surrounded by the sea, but that at low water it was joined to the mainland so that one could cross on foot. Wataalamu wa historia wamesema, pamoja na madai mengine, kuwa mtu wa kwanza kufika Kilwa alifika kwa namna hii Kulifika jahazi na watu waliodai wametoka Shirazi katika nchi ya Uajemi Inasemekana kwamba kulikuwa na majahazi saba: la kwanza lilifika Mandakha; la pili Shaugu; la tatu mji wa Y anbu; la nne Mombasa; la tano kwenye Kisiwa cha Majani; la sita katika nchi ya Kilwa; na la saba Nzwani Wanasema kuwa mabwana wa majahazi hayo sita walikuwa ndugu, naye aliyekwenda Nzwani alikuwa baba yao. Allahu aalim-mungu ndiye mjuzi [... ] Walipofika katikajahazi lililokwenda Kilwa, waliona kuwa ni kisiwa kizungukwacho na bahari, lakini wakati wa maji ya kupwa kisiwa kinaungana na nchi kavu, kunapitika kwa mtguu. 7 Historia ya muswada huu inaelezwa na Freeman-Grenville (1966:34), ambaye aliutafsiri kwa Kiingereza Inaonekana kwamba muswada wa kame ya 16 umepotea. Sir John Kirk alipewa nakala iliyo chanzo cha habari yetu na Sayyid Barghash katika mwaka wa 1872, lakini nakala hii si kamili

128 THILO C. SCHADEBERG They disembarked on the island and met a man who was a Muslim, followed by some of his children It is said his name was Muriri wa Bari. They found one mosque there, said to be the one he is buried in, which is called Kibala. They asked the Muslim about the country and he replied The island is ruled by an infidel from Muli, who is king of it; he has gone to Muli to hunt, but will soon return. After a few days the infidel returned from Muli and crossed to the island at low tide. The newcomer and he met together, and Muriri acted as an interpreter. The newcomer to Kilwa said I should like to settle on the island, pray sell it to me that I may do so. The infidel answered I will sell it on condition that you encircle the island with coloured clothing The newcomer agreed with the infidel and bought on the condition stipulated He encircled the island with clothing, some white, some black, and every other colour besides So the infidel agreed and took away all the clothing, handing over the island and departing to Muli [...} The fir:st king of the island was Sultan Ali ibn al-husain ibn Ali surnamed Nguo Nyingi [Many Clothes] Wakateremka kisiwani, wakamkuta Mwislamu aliyefuatwa na baadhi ya wanawe. Inasemekana kwambajina lake Iilikuwa Muriri wa Bari. Wakakuta msikiti mmoja, inasemekana kwamba ni ule alipozikiwa, unaoitwa Kibala.. Wakamwuliza Mwislamu juu ya nchi akajibu: Kisiwa kinatawaliwa na kafiri kutoka Muli, ambaye ndiye mfalme wake; ameondoka kwenda Muli kuwinda, atarudi karibuni Baada ya siku chache, kafiri akarudi kutoka Muli, akavuka kufika kisiwani wakati wa maji kupwa Mgeni alikutana naye, na Muriri akiwa mtafsiri. Mgeni wa kufika Kilwa akasema: Nataka kukaa kisiwani, naomba uniuzie nikae. Kafiri akajibu: Nitakuuzia kwa sharti uzungushe kisiwa kwa nguo ya rangi nyingi.. Mgeni akakubaliana na kafiri akanunua kwa sharti lililokubaliwa Akazungusha kisiwa kwa nguo, nyingine nyeupe, nyingine nyeusi, na za kila rangi. Basi, kafiri akakubali na kuchukua nguo zote, akatoa kisiwa, akaondoka kwenda Muli. [.. ] Mtalme wa kwanza wa kisiwa alikuwa Sultani Ali ibn ai-husain ibn Ali, najina lake la Kiswahili Iilikuwa Nguo-Nyingi.

MW ANZISHAJI W A MJI WA NGOJI (ANGOCHE) 129 Turudi tuangalie zaidi habari ya asili ya Ngoji au Koti. Mapokeo ya Kilwa ni mapokeo ya watawala wa mji huo. Hao waliona ni muhimu kuwa na nasaba ya Shirazi, huko Uajemi Mapokeo ya watawala wa Angoche yaliandikwa mwanzo wa kame hii (ya 20}. Wao waliona ni muhimu kuwa na nasaba ya ule mji maarufu uitwao Kilwa.. Lakini hadithi ya Terezento Roopa ni hadithi ya watu wa kawaida Tena ni hadithi ambayo inasimuliwa sio na Wakoti tu, jirani zao pia wanaijua na kuipenda. Msimulizi wa habari yetu ya Terezento Roopa, Bwana Asumaani Luzakeero Laasu, si Mkoti bali ni Mmakhuwa ambaye alikuwa akiishi Koti kisiwani kw a muda mrefu Aliposimulia hadithi hii, mwaka juzi, kaiibu na mji wa Angoche, alichagua kutumia lugha ya Kikoti ingawa wasikilizaji wengi walikuwa Wamakhuwa, lakini waliweza kufahamu hadithi hiyo.. Inaonekana kuwa, kwa watu hao, nasaba ya mwanzishaji wa Koti si kitu muhimu Ni mgeni, lakini hatuarifiwi anatoka mahali gani au kabila gani Tukilinganisha habari hiyo juu ya asili ya Koti na mapokeo mengine ya aina hiyo ya kihistmia katika Afrika, tunaweza kutambua tofauti kubwa. Kwa kawaida, mapokeo hayo huanza na mfalme au mtemi au mwindaji hodari, na shujaa huyo humwoa binti na kuzaa watoto na hivyo huanzisha ukoo au kabila jipya. Bali, Terezento Roopa anawashinda na kukamata wanaume wenye nguvu, na baada ya muda wafuasi hao ni kama watotci wake Hatimaye Terezento Roopa, pamoja na kundi lake, anakutana na mtemi mkuu na kupigana naye. Hamshindi, wala hashindwi naye. Kila anapoangushwa Terezento Roopa baharini, kisiwa kinatokea, na kila anapoangushwa Nankontta, kisiwa kinatokea. Visiwa hivi vyote ni visiwa vya Ngoji, na mashujaa wote wawili ni kama mababu wa watu wake.. Ninavyoona, mapokeo hayo ni mapokeo ya kabila ambalo ni muunganisho wa watu wa asili mbalimbali.. Lugha yao pia ina mizizi miwili, mzizi mmoja ni Kimakhuwa na mzizi mwingine ni Kiswahili 8 Marejeo Academia Real das Sciencias 1812; toleo la pili 1867. Collec~tio de notfcia~ para a hist6ria e geografia das naroes ultramarinas que vivem nos dominios portuguezes Juzuu la pili. Lisboa: Typographia da Academia. ("Livro do Duarte Barbosa" kinaanza uk 245.) Dames, Manse] Longworth. 1918. The book ofduarte Barbosa An account of the countries bordering on the Indian Ocean and their inhabitants, written by Duarte Barbosa, and completed about the year 1518 AD. London: Printed for the Hakluyt Society. Freeman-Grenville, G.. S. P 1966 (toleo la pili}. The East African coasl Select documents from the fir:st to the earlier nineteenth century. Oxford: At the Chuendon Press 8 Nawashukuru walimu wenzangu waliosoma makala hii na kutoa maoni ya kuiboresha pamoja na kurekebisha Kiswahili. Ahsanteni!

130 THILO C. SCHADEBERG Lupi, Eduardo do Couto. 1907. Angoche.. Breve memoria sabre uma das capitanias-m6res no Districto de Mofambique. Lisboa: Ministerio dos Neg6cios da Marinlia e Ulttamar; Typographia do Annuruio Commercial Newitt, M. D.. D. 1972. The early history of the Sultanate of Angoche. Journal of African History 13:397-406. Schadeberg, Thilo C.., and Francisco Ussene Mucanheia, fortcoming. EKoti. The Maka or Swahili language ofangoche.. Terezento Roopa Nsimaana w'eekoti Contado por Assumane Luzaquero La~o, editado por Francisco Ussene Mucanheia e Thilo C Schadeberg. Forthcoming.